Nilienda usaili BOT, tulikua nyomi sana, watu wakawa wanasema sitatoboa maana ni interview ya kwanza. Huwezi amin nilipita interview zote tatu mpaka oral, siku ya oral tukapokonywa simu saa tatu asubuhi tukafungiwa kwenye moja ya yale maghorofa yao juu kabisa. Ni mwendo wa kula vyuku na kwenda toilet tu, nikaja kuingia kwenye interview saa mbili kasoro usiku toka asubuhi. Mule ndani kiukweli mwanzo nilijikanyaga sana hasa kwa maswali hayahusiani na field yangu. Ila kwa maswali ya field wale jamaa walikiri ndani ya chumba cha panel kuwa nipo vizuri. Niliambiwa kuwa nitapigiwa simu ndani ya wiki mbili ila mpaka Leo sijawahi pigiwa nadhani sababu iloniangusha ni mavazi sikua nimewaka sana kama wengine.
Nashukuru mungu kwa sasa nipo chuo kikuu kimoja nchini kama mkufunzi msaidizi na mrija wa asali ni mrefu kidogo zaidi ya ule wa BOT.
Mungu akikupa akuandikii barua, BOT walinipa funzo la kuvaa, tuliofanya usaili chuo kikuu kimoja na tukafika oral nadhani watakua washafahamu. Umaridadi unaongeza marks za kutoboa