Usaili wa Utumishi: Kipi kilikufanya ufaulu au ulikosea wapi?

Usaili wa Utumishi: Kipi kilikufanya ufaulu au ulikosea wapi?

Nadhani kujiamini na kujibu kwa ufasaha maswali ndo dhana kuu, na yote haya yanakuja kwa maandalizi bora kabla ya interview.

Mara nyingi maswali ya oral hawaendi nje kabisa ya vitu flani basic vya course yako na vile vya job description kwa hiyo mostly wana try kupima kujiamini kwako, dressing, attitude na body language in general.

So wengi wanao ingia oral kupishana marks ni kidogo sana so kitakacho kupa kazi na kuku tofautisha na mwingine ni vitu kama hivyo nilivyo taja hapo juu.

Did my first interview na nilipata moja kwa moja naamini nili practice vyote nilivyo andika hapo.
 
Oral ni Confidence tu mzee nimefanya saili chache za utumishi huku zote nikitoboa, Kwangu niliulizwa maswali matano ambapo Moja lilinitoa knock out ila sikujali niliwaambia panelist waskip ilo na tutarejea wanipe Clarifications nzuri ndio nitoe majibu, Panelist waliendelea kuniuliza maswali huku nikiyajibu with Fully Confidence
 
Soma tangazo la kazi vizuri na ujue kazi hiyo itakuwa na majukumu yapi (job description), hii itakusaidia kujiandaa kujibu maswali yatakayoendana na majukumu tajwa.

Alafu ni kujiamini tu na sio lazima utoe jibu sahihi sana hata ukiweza kutoa majibu yanayoridhisha au kuonyesha ufahamu inatosha Sana tu.

Uwe makini na lugha unayotumia,usitumie maneno magumu ambayo maana yake huifahamu ili kuepuka kuzalisha maswali mengi zaidi kwako.

Ukiulizwa swali nenda kwenye jibu moja kwa moja na usitoe maelezo mengi yasiyo na umuhimu sana, usitumie muda mrefu Sana kujibu swali maana utawachosa wauliza maswali kukusikiliza.

Ikiwezekana jaribu kufanya majaribio ukiwa peke yako mbele ya kioo au na mtu mwingine ili ujenge kujiamini kabla ya siku husika ya usaili.

Usiache kuomba Mungu na ombea siku ya usaili, ombea watakaokufanyia usaili na hata watahiniwa wenzako ili siku iende vizuri.

Kila laheri boss.
 
Na hizo 5 questions ni zimeshiba[emoji28]. Hizi interview ni Mungu kwanza tu halafu ndo personal effort inafata[emoji28].
written interview za utumishi ni kama Assignments, fresh graduates na wale wakali wa copy and pasting kutoboa ni rahisi maana hapo hamna kuweka sense zaidi ya kuonesha ni mzuri wa speed na kukariri materials.. Sasa mimi sitawezana 😁😁
 
Oral Kuna maswali Yale common hupendelea kuuliza
1.your background based on experience and education
2.Mtumishi wa anatakiwa kuwa na sifa zipi au quality of civil servant
3.Responsibilities na duty za kazi izoomba
Maswali 2 ya mwisho yanakuwa ya fani husika
-Kingine kikubwa ni kutokaa kimya kujibu maswali kwa Confidence usiache kujaribu tena kwa Confidence.
-Mwaka Jana mwezi wa kwanza baada ya kupita practical na kwenda Oral nilijiandaa hivyo na nikakutana nayo hayo nikakaa data base miezi 2 nikapangiwa taasisi moja hivi. Tulitolewa wote 9 tulioingia oral
 
Nisikilizeni wajameni vijana wenzangu interview ni confidence na kucheza na kujibu short and clear wacha kuleta maneno mengi kama dalali wa kizaramo

Kingine ukiwa nje andaa muonekano kuliko kukariri ukianza kukariri unajitia hofu na panic siku ya interview sio Bado uko kweny foleni una vikaratasi unasoma sijui unakuja kupoteza confidence mapema

Kuwa free nyanyua na chezesha mikoni sio kama unahojiwa Kwa kesi ya kuua umekaa kama moja .Fanya kujibu usibadili majibu uliyotaja kazania hayo hayo sio unakiwa kigeugeu usirudie sentence
 
huko private maswali 5 mnafanya muda gani
Kwa experience yangu hiyo written ni mara chache kukutana nayo labda kama utakutana na maswali kwenye portal zao za application ambazo huwezi kukutana na maswali ya darasani. Mara nyingi ni Oral na practical ambazo kuwa shortlisted inategemeana na CV yako
 
written interview za utumishi ni kama Assignments, fresh graduates na wale wakali wa copy and pasting kutoboa ni rahisi maana hapo hamna kuweka sense zaidi ya kuonesha ni mzuri wa speed na kukariri materials.. Sasa mimi sitawezana [emoji16][emoji16]

Kabisa, the interview I did tuseme 50% ya waliopata wote ni fresh graduates maana mambo bado yako kichwani.

Ni ngumu sana kwa graduate wa nyuma kidogo ku cope up na speed na requirements za written interview ya utumishi, ile ni vita!!
 
Kabisa, the interview I did tuseme 50% ya waliopata wote ni fresh graduates maana mambo bado yako kichwani.

Ni ngumu sana kwa graduate wa nyuma kidogo ku cope up na speed na requirements za written interview ya utumishi, ile ni vita!!
Hongera mkuu kwa kuingia kwenye payroll ya serikali 👏👏👏
 
Nachokiamini mpaka sasa hata kama interview itakuwa tia maji tia maji kama umeshafanyiwa mchakato we pale ni kuwakilisha jina tu ila kazi ni yako tayari.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom