Usajili wa Bernard Morrison kurudi Yanga, kuna mvutano mkali unaendelea!

Usajili wa Bernard Morrison kurudi Yanga, kuna mvutano mkali unaendelea!

Lakini haji manara saizi si mshazoea na kum treat kama mwenzenu, kwani bado wale wenye kinyongo naye wakimtazama kua ni mamluki bado wapo?

We kwa upande wako haji unamchukuiaje?

Ni mtu fulani mwenye mapenzi ya kweli na club au yuko hapo kwa ajili ya maslahi tu na sio mshabiki wa kweli?
Haji tunampenda kwa asilimia 100 kwa sababu anawaudhi ninyi, ila hatumuamini kwa asilimia 100 na ndio Mana yupo kwa ajili ya kuwaropokea tu ila hawezi ingia kwenye vikao vya bodi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli maana jamaa kabakiza akili za kuvukia barabara tu. Mtu anapiga picha mbovu mbovu za chupi hadharani,utovu wa nidhami etc hana faida kwa timu
Umeonaee. Na wenyewe pia wanalijua hilo kwamba watu hawamfurahii Manara ni hiyo basi tu.

Tuwaombe wasituangushe kwa kweli hilo pira (morison) wawaachie hao hao 5imba wahangaike nalo. 😀
 
Huyo kiongozi anaelazimisha hilo, amsajili akasimamie biashara zake na sio kurudi Yanga.
 
Lakini kumbuka wametumia almost mwaka mahakamani kuhakikisha wanamrejesha morrison, sasa huoni kwamba hii kwa upande wao ni kama golden chance?

Umetoka home umebeba mapanga na mimbwa kibao kwenda kuwinda sungura , umefika huko machakani umezurura umepoteza muda wako mwingi na hujapata chochote, halafu unafika home unakuta kumbe ulivyotoa uliacha mlango wazi una shangaa unamuona swala anajizungusha zungusha hana pa kwenda, utamuacha?
Yanga haijawahi kuhangaika ili Morrison arudi bali walikuwa wanapambania haki yao kifedha!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli maana jamaa kabakiza akili za kuvukia barabara tu. Mtu anapiga picha mbovu mbovu za chupi hadharani,utovu wa nidhami etc hana faida kwa timu
Ikitokea akaja kwetu naona atakuja kutuvurugia tu vijana wetu ambao kwa 100% akili zao zimetimia.
 
Muache asepe, morrison ni mchezaji mzuri endapo ataacha uchoyo na kupenda kucheza kwa show off

Huko aendako akijirekebisha hayo mapungufu yake atakuwa ni mchezaji hatari na wakuhofiwa na wapinzani
Hawezi kubadilika huyo jamaa
 
Lakini kumbuka wametumia almost mwaka mahakamani kuhakikisha wanamrejesha morrison, sasa huoni kwamba hii kwa upande wao ni kama golden chance?

Umetoka home umebeba mapanga na mimbwa kibao kwenda kuwinda sungura , umefika huko machakani umezurura umepoteza muda wako mwingi na hujapata chochote, halafu unafika home unakuta kumbe ulivyotoa uliacha mlango wazi una shangaa unamuona swala anajizungusha zungusha hana pa kwenda, utamuacha?
Kusema Yanga walitumia mwaka mzima kutaka kumrejesha Morrison siyo sahihi. Si ßhabiki wao lakini nilichokiona ni ule utamaduni wenu wa kutaka kukomoana Simba Vs Yanga.
 
Kipi kinashindikana kwa yanga ? Kama manara walimpokea na Sasa ndie daraja yao na kusahau matusi aliwatukana miaka nenda Rudi lakin leo kawa mwenye yanga na kuwasahau kabisa akina Antonio waliopambana na manara miaka nenda Rudi Ila baada ya kurud nugaz hafai kabisa na wakamtema ,sasainashindiakana Nini kwa Morrison.
Wafanyakazi sio mashabiki wanafanya kazi popote Manara alikua muajiliwa wa Simba
 
Kusema Yanga walitumia mwaka mzima kutaka kumrejesha Morrison siyo sahihi. Si ßhabiki wao lakini nilichokiona ni ule utamaduni wenu wa kutaka kukomoana Simba Vs Yanga.
Basi wamchukue tena ili kutukomoa maradufu
 
Ila Simba SC wenzangu niwaulize: hivi Morrison amekuwa mbaya kuliko Mkude? Pia viongozi wanasema hajaleta matokeo waliyoyatarajia, je Mugalu ameleta matokeo gani?

Tukiachana na mambo ya nidhamu kisha tukaangalia msaada kwa timu; kati ya MORRISON na MUGALU nani ni liability (mzigo)? Au Mugalu yeye pamoja na kukosa magoli ambayo hata mwanangu wa darasa la pili angefunga anaonekana ana thamani kwasababu ana nidhamu? Hii Simba imechanganyikiwa.
Nidhamu ndo kila kitu kwenye kazi yoyote, kipaji bila nidhamu = 0
 
Nidhamu ndo kila kitu kwenye kazi yoyote, kipaji bila nidhamu = 0
Sawa ila hekima nayo inatakiwa unapodeal na watu wa aina hiyo. Unayajua maisha ya ndani na nje ya uwanja ya Edmund wa Brazil (yule aliyewahi kumtwanga makofi Ronaldo De Lima kwenye World Cup 1998, na bado hakufukuzwa kwenye kambi) au Garrincha (siyo Steven Mapunda wa Tz)? Vipi Paul Ince, George Best, Ian Wright na Paul Gascoigne Gaza?
 
Back
Top Bottom