Usajili wa Bernard Morrison kurudi Yanga, kuna mvutano mkali unaendelea!

Usajili wa Bernard Morrison kurudi Yanga, kuna mvutano mkali unaendelea!

Ivi Yanga Haioni Wachezaji Wengine, Mbn Wachezaji Wamejaa Wengi Kila Kona Ya Afrika Kuanzia Kusini, Kaskazini, Kati, Magharibi Na Mashariki...Af Wanauwezo Mzuri Wa Kucheza Soka Shida Bado Hamjawaona...Yanga Wafanye Msako Kwenye Ligi Za Sehemu MbaliMbali Hapa Afrika Watapata Watu Wataokaweza Kuwamudu Kuwasajili Na Wenye Uwezo Mzuri Kwa Manufaa Ya Timu... Sio Kila Siku Kung'ang'ania Watu Wale Wale Wakati Wachezaji Wazuri Na Wenye Hadhi Ya Kucheza Yanga Ni Wengi...
usajili wenu mkubwa huo

5118C96B-5F3E-49FA-876D-0003BE213309.jpeg
 
Acha aondoke, tumeotumia kazi ya kuwajambisha gongowazi kwahivyo inatosha.
 
Muache asepe, morrison ni mchezaji mzuri endapo ataacha uchoyo na kupenda kucheza kwa show off

Huko aendako akijirekebisha hayo mapungufu yake atakuwa ni mchezaji hatari na wakuhofiwa na wapinzani
Kutoka Kongo, Afrika Kusini, hadi Tanzania historia inamuhukumu hawezi kubadilika, ni mchezaji mzuri lakini anaweza kufanya kitu mpaka ukashangaa au kuigharimu timu kabisa, kama tukio la kuvua bukta.

Kwa namna Simba SC ilivyo kwa sasa wakiamua wasimuongezee ni sawa.
 
Tunaweza kusema ni upuuzi kufikiria kwamba yanga itamsajili Morison, kuna uwezekano mkubwa wa yeye kubaki hapa Tanzania katika moja ya vilabu vingine.
 
Kwa akili na upoyoyo wa baadhi ya viongozi wetu, lolote linawezekana! Kama Haji Manara na kejeli zake zote zile, alipokelewa! Basi hata kwa BM3, haitashindikana.

Ila binafsi sitafurahishwa hata kidogo na huo ujio wake (kama ni kweli)
Lakini haji manara saizi si mshazoea na kum treat kama mwenzenu, kwani bado wale wenye kinyongo naye wakimtazama kua ni mamluki bado wapo?

We kwa upande wako haji unamchukuiaje?

Ni mtu fulani mwenye mapenzi ya kweli na club au yuko hapo kwa ajili ya maslahi tu na sio mshabiki wa kweli?
 
Tunaweza kusema ni upuuzi kufikiria kwamba yanga itamsajili Morison, kuna uwezekano mkubwa wa yeye kubaki hapa Tanzania katika moja ya vilabu vingine.
Na inaonekana katika nchi alizopita hakuwahi kutengeneza fanbase ya kuheshimika kisoka kama alivyokuja hapa bongo, kiukweli ni kwamba kupitia hizi simba na yanga kumekuwa kunatoa benefit kwa wachezaji wengi sana kuwa maarufu kuliko nyakati zoote walizokuwa wakicheza nchi zingine

Mfano hata mayele, nadhani hata yeye amekuwa suprised na umaarufu ambao amejiongezea since katua hapa bongo land. Hakuna mshabiki yeyote ambaye anaweza kukubali kua mayele huyu alitrend hivi hivi katika club zingine alizochezea yani kiasi cha yeye kutoona utofauti
 
Kama ni kweli viongozi wangu wa Yanga watakuwa ni viongozi wapumbavu kuwahi kutokea wa soka ulimwenguni
Lakini kumbuka wametumia almost mwaka mahakamani kuhakikisha wanamrejesha morrison, sasa huoni kwamba hii kwa upande wao ni kama golden chance?

Umetoka home umebeba mapanga na mimbwa kibao kwenda kuwinda sungura , umefika huko machakani umezurura umepoteza muda wako mwingi na hujapata chochote, halafu unafika home unakuta kumbe ulivyotoa uliacha mlango wazi una shangaa unamuona swala anajizungusha zungusha hana pa kwenda, utamuacha?
 
Mkeo akikupeleka mahakamani kwa ishue za unyumba ambazo mngeweza kuzimaliza ninyi wawili au kupitia wanaukoo, ukafungwa au kulipa fine na yeye akaenda kuolewa na bwana mwinginebaada ya kumaliza kutumikia adhabu ukarudi maisha yakaanza kukunyokea akatamani tena arudi kwako apo ANAKUJA KUICHOMOA ROHO YAKO
 
Kuna muda mkiandika vitu mnatumia akili tu ya kawaida, unapoizungumzia Yanga kwenye issue ya Morisoni unatakiwa utumie akili ndogo tu ya kuzaliwa kabla hata hujamsikiliza mjinga yoyote kumhusisha huyo kichaa na Yanga.
Unathubutu kusema eti Yanga waiumize Simba kwa kumchukua Morison, hiyo sio tu kuwa na bangi bali ni dharau kwa Simba na Yanga yenyewe.
Morison hahitajiki Yanga na wala hahitajiki Simba kama mnataka kumpigia debe mmechelewa
 
Mi naombea aende kwa watani zetu utoh ili waongeze idadi ya mapoyoyo kwenye klub yao (manara +morison+……)
Oya usiseme hivyo, yule Morrison ni mtu mbad ataiumiza Simba round ijayo na wachezaji wale wa umri wa JUWATA Jazz.
 
Kipi kinashindikana kwa yanga ? Kama manara walimpokea na Sasa ndie daraja yao na kusahau matusi aliwatukana miaka nenda Rudi lakin leo kawa mwenye yanga na kuwasahau kabisa akina Antonio waliopambana na manara miaka nenda Rudi Ila baada ya kurud nugaz hafai kabisa na wakamtema ,sasainashindiakana Nini kwa Morrison.
 
Ila Simba SC wenzangu niwaulize: hivi Morrison amekuwa mbaya kuliko Mkude? Pia viongozi wanasema hajaleta matokeo waliyoyatarajia, je Mugalu ameleta matokeo gani?

Tukiachana na mambo ya nidhamu kisha tukaangalia msaada kwa timu; kati ya MORRISON na MUGALU nani ni liability (mzigo)? Au Mugalu yeye pamoja na kukosa magoli ambayo hata mwanangu wa darasa la pili angefunga anaonekana ana thamani kwasababu ana nidhamu? Hii Simba imechanganyikiwa.
 
Lakini kumbuka wametumia almost mwaka mahakamani kuhakikisha wanamrejesha morrison, sasa huoni kwamba hii kwa upande wao ni kama golden chance?

Umetoka home umebeba mapanga na mimbwa kibao kwenda kuwinda sungura , umefika huko machakani umezurura umepoteza muda wako mwingi na hujapata chochote, halafu unafika home unakuta kumbe ulivyotoa uliacha mlango wazi una shangaa unamuona swala anajizungusha zungusha hana pa kwenda, utamuacha?

Mkuu kwa upande wa sakata Morrison ni kujivua nguo kwa viongozi Yanga endapo watamtejesha. Ni sawasawa uwe na demu ambae ni fundi haswa kwenye mambo 6x6 lakini ni muhuni ila umeamua kumvumilia pamoja na uhuni wake. Huyu demu anakuja kupata pedeshee mwenye mapesa anashawishika kuolewa huko. Huyu bwanake kila anapoenda kutafuta suluhu ili mke arejee lakini mke anamkana wazi wazi kuwa huna ndoa na mimi achana na mimi nina mume wangu saivi basi kwavile ndoa ni mpya akahadaika mpaka kumnanga EX kwa maneno ya mauzi eti NAWAKERA. saivi yamemshinda kwenye ndoa mnampokea wa nini? Hili ndio nafasi pekee ya Viongozi wa Yanga kufurahi kuwa alipwe ujira wake kwa nidhamu yake ya hovyo. Malipo ni hapa hapa
 
Back
Top Bottom