Usajili wa Bernard Morrison kurudi Yanga, kuna mvutano mkali unaendelea!

Haji tunampenda kwa asilimia 100 kwa sababu anawaudhi ninyi, ila hatumuamini kwa asilimia 100 na ndio Mana yupo kwa ajili ya kuwaropokea tu ila hawezi ingia kwenye vikao vya bodi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli maana jamaa kabakiza akili za kuvukia barabara tu. Mtu anapiga picha mbovu mbovu za chupi hadharani,utovu wa nidhami etc hana faida kwa timu
Umeonaee. Na wenyewe pia wanalijua hilo kwamba watu hawamfurahii Manara ni hiyo basi tu.

Tuwaombe wasituangushe kwa kweli hilo pira (morison) wawaachie hao hao 5imba wahangaike nalo. 😀
 
Huyo kiongozi anaelazimisha hilo, amsajili akasimamie biashara zake na sio kurudi Yanga.
 
Yanga haijawahi kuhangaika ili Morrison arudi bali walikuwa wanapambania haki yao kifedha!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli maana jamaa kabakiza akili za kuvukia barabara tu. Mtu anapiga picha mbovu mbovu za chupi hadharani,utovu wa nidhami etc hana faida kwa timu
Ikitokea akaja kwetu naona atakuja kutuvurugia tu vijana wetu ambao kwa 100% akili zao zimetimia.
 
Muache asepe, morrison ni mchezaji mzuri endapo ataacha uchoyo na kupenda kucheza kwa show off

Huko aendako akijirekebisha hayo mapungufu yake atakuwa ni mchezaji hatari na wakuhofiwa na wapinzani
Hawezi kubadilika huyo jamaa
 
Kusema Yanga walitumia mwaka mzima kutaka kumrejesha Morrison siyo sahihi. Si ßhabiki wao lakini nilichokiona ni ule utamaduni wenu wa kutaka kukomoana Simba Vs Yanga.
 
Wafanyakazi sio mashabiki wanafanya kazi popote Manara alikua muajiliwa wa Simba
 
Kusema Yanga walitumia mwaka mzima kutaka kumrejesha Morrison siyo sahihi. Si ßhabiki wao lakini nilichokiona ni ule utamaduni wenu wa kutaka kukomoana Simba Vs Yanga.
Basi wamchukue tena ili kutukomoa maradufu
 
Nidhamu ndo kila kitu kwenye kazi yoyote, kipaji bila nidhamu = 0
 
Nidhamu ndo kila kitu kwenye kazi yoyote, kipaji bila nidhamu = 0
Sawa ila hekima nayo inatakiwa unapodeal na watu wa aina hiyo. Unayajua maisha ya ndani na nje ya uwanja ya Edmund wa Brazil (yule aliyewahi kumtwanga makofi Ronaldo De Lima kwenye World Cup 1998, na bado hakufukuzwa kwenye kambi) au Garrincha (siyo Steven Mapunda wa Tz)? Vipi Paul Ince, George Best, Ian Wright na Paul Gascoigne Gaza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…