Usajili wa ‘Kanisa la Neema’ uchunguzwe

halafu wewe unatembelea v8, waumini hata pa kulala hawana na wanakuletea sadaka. na bado unawashika masikio. basi, uchukue sadaka na ufundishe mafundisho ya kweli, shida ni pale unaanza kuwaomba mara walete kucha, mara nywele za utosi (baadaye watakuja na vuzi), mara wakuuzie mafuta, mara wakuuzie chumvi pesa wanaweka mfukoni. hao ni matapeli tu serikali iingilie kati iwaokoe raia wake wanaumizwa.
 
Ni wivu tuu.

Wivu au kasema kweli?. Haya mambo ya kusema ndio yamefanya watu wanyamaze mpaka serikali imebidi kuingilia kati kutokana na kauli kama zako. Huku Zumaridi anajiita mungu, huku Nabii fulani anajiita malaika huku Mzee wa neema anadai hakuna dhambi na kule Suguye anadai njoo na nywele za utosini kesho atasema njoo na kinyesi.

Tusiunge mkono huu ujinga ipo siku litatokea janga ana hatutaweza kulizuia.
 
Usipaniki twende taratibu
Uandishi wako unanifanya nishindwe kukujibu kwa Hoja mujarabu!
1. Barabara ya Morogoro unayoiona Leo haikua hivyo' miaka kadhaa iliyopita ilikua two ways only. Na hizo nyumba za Ibada zilikuepo.

2. Nimekutolea mfano wa hapo KAMATA na pale kongowe mbona hujarespond kwamba ni wrong au right! Badala ya kulalamika na kusema naandika kwa kujifurahisha nakupa mifano hai! Unachotakiwa kufanya ni kupendekeza kwa msajili na wizara ya mambo ya Ndani kwamba waje na masharti ya usajili Pamoja na vibali vya ujenzi kwamba angalau kuwe na Miata mia Moja Kati ya eneo la kanisa na kanisa au kanisa na msikiti! Utaeleweka.

3. Nitaweza kukutajia panapo kanisa la kilokole na la Kiroma na sio kiloma yaliyopo sehemu Moja! Tafuta muda nenda pale mbezi mwisho utakuta Anglican Church wamepakana na Adventists na on the other side Pana kanisa la kilokole tena mawili and upande mwingine Kuna Roman Catholic church st Peter Claver! Kifupi ni eneo la makanisa ya madhehebu anuwai!
 
kuna manabii wameshapiga picha wakatengeneza chupi za wanawake hapahapa duniani, mwanamke akiwa na shida ya uzazi, wanamwambia nunua chupi yenye sura yangu utapata mtoto. hivyo ni kweli, siku mtu akisema anaumwa tumbo ili aombewe wanaweza kusema akalete kinyesi. kama ana shida ya uzazi wataasema akelete zile nywele za kule, wanafanya chochote watakacho kwa jina la uhuru wa kuabudu.

mimi nilifungulia tv yake jana, anasema BIBLIA NI KITABU CHA KAWAIDA KAMA VITABU VINGINE TU. hiyo ni moja, anaongea machukizo mengi ambayo yanaamsha hisia lakini unasema basi kwasababu mimi ni mkristo sitakiwi kujichukulia sheria mkononi ila kiukweli anaamsha hisia za hasira na ule mdomo wake wa kilevi.
 
PETER NYAGA mwenye tv ya urejesho, ana kanisa tabata pia, ni mkenya, tv yake ameunganisha tz na kenya, na watu michango/sadaka huwa wanatoa toka ncho zote mbili. huyu ndio ana upako wa VIP ana kila kitu kulingana na namna ulivyolipa pesa. mkenya kaja kupiga pesa tz na tunamwangalia tu kwa jina la uhuru wa kuabudu. kuna kengine huko morogoro nilikasikia kameenda sijui kwenye mlima gani, Nabii Joshua, kale kalikuwa Tanga. kanasema kameona kuna chemchemi kule morogoro watu waende yale maji ni ya uponyaji. na serikali inaangalia tu. hivi hapo unahitaji elimu au kipimo gano kujua kuwa huyu ni tapeli au la?
 

Acha mentality za kimasikini na wivu wa kike,kwahiyo ulitaka hao manabii na mitume wawe masikini watembelee yeboyebo na suruali zilizotoboka matakoni ndio ufurahie?

Get a job acha wivu wa kike.
 
"Waumini wakianza kuyakimbia makanisa yenu yaliyopoa kiroho na kwenda kwenye makanisa yenye upako sadaka zenu zina pungua na kuanzisha bifu. Hizo conflict of interest baina yenu pambaneni nazo wenyewe." [emoji3][emoji3]

Wengi ya hawa manabii na wachungaji huwa wana bifu zao na kuchongeana kwingi kwa sababu ya sadaka za waumini,wana vita baina yao yote hii ni sadaka za waumini wanagombania.

Unadhani kwanini mzee wa upako alikua ana msemo wa watashindana lakini hawata shinda
 
Unashangaa dhehebu!! Watu wanajiita mitume kabisa .
 
Acha mentality za kimasikini na wivu wa kike,kwahiyo ulitaka hao manabii na mitume wawe masikini watembelee yeboyebo na suruali zilizotoboka matakoni ndio ufurahie?

Get a job acha wivu wa kike.
setikari yenyewe inayaogopa mkanisa wnaogopa kulogwa
 
Iyo dini ni upumbavu mtupu na wanaofuata ni makondoo akili hawana hata .

Yaani hayo masharti ni ya waganga kabisa sema wao wanavaa suti sijui uje na kucha, mara kitambaa cheupe ..Majitu Haina akili ya kudadavua mambo kwamba hao ni waganga kisa wanavaa suti na hapo nyuma Kuna disco na pombe watu wanakunywa huko kweny kanisa.
 

Imamu Ebu punguza hasira,andika vzr ueleweke.
 

Jamaa namuelewa sana nikirudi dsm nitanza kusali pale mana ameruhusu ndoa ya wake wengi safi sana hapa kanipata
 
Haujawa specific ni nini hasa katika biblia kinachopotoshwa na kinapelekea madhara gani jumuishi na mtambuka kwa nchi,jamii na mtu mmoja mmoja. Weka bayana kero zianishwe hapa umepopoma tu kiholela
 

Usihukumu usije kuhukumiwa,acheni magugu yaote pamoja na ngano yatapepetwa siku ya mavuno.
 
Shida YAKO ni nini usajili au aina ya mafundisho
 
Hata Mimi nilipoona kanisa lina night club. Nikapata maswali.
Night clubs na Ukristo wapi wapi.
Pana mmoja aliwahi shauri eti kuwepo na disco la Kikristo.
 
Hii nchi ni kama shamba la bibi.
Kiukweli zama za leo kila kitu kimefunguliwa pasipo hata kuzingatia taratibu. Wapo baadhi wanapotosha na hakina anayejali.

Na si tu kwenye masuala ya imani hata kwenye mambo mengine ya kijamii, hakuna maadili. Wanamuzikinwanimba jukwaani wakiwa nusu uchi na nyimbo hazina maadili ya kitanzania!
 
Hata Mimi nilipoona kanisa lina night club. Nikapata maswali.
Night clubs na Ukristo wapi wapi.
Pana mmoja aliwahi shauri eti kuwepo na disco la Kikristo.
Mi nadhani hawa watu wakalipiwe vikali ili ikibidi watumie dini zao halisi wasijisingizie Ukristo. Ukristo hauko hivyo. Na kama ni mpinga Kristo basi mtu ajitanabaishe kabisa kuwa ni dini ya upinga Kristo or whatever atakavyoamua kujiita mwenyewe, na aruhusiwe kuendesha ibada zake kwa mujibu wa hiyo imani yake. Inakera sana kuona Ukristo unafanywa shamba la bibi kila mtu anajiamulia tu atakavyo! Hata kama ni uhuru jamani hapana, hizi issue zimekuwa too much aisee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…