Tetesi: Usajili wa Mabasi ishirini mapya ya Abood

Esther ana
Basi nane rombo dar
Basi nne arusha dar
Huko singida dar sijui idadi yake
 
Unamjua mumiliki wa Esther? Hakuna biashara pake.. ni utakatishaji wa ngawira
Ni nani huyo? Kuna siku korogwe Tanga asubuh nikadamkia mombo, mtu niliekua nakutana nae kwa bahati mbaya akachelewa nikaa kwenye kiosk nikawa namsubiri, zilipita bus 13 za Esther hadi mda naondoka, za kwenda na kurud

Hapo hapo bado zipo za kiomboi huku

Muda uliotumika vs Success n mfupi mno

I think aliwakuta Marangu, Extra Luxury , hata Tilisho pia. Ila kakua kwa speed ya umeme
 
Abood ana mabasi zaidi ya 300 unashangaaje hayo20
Abood alinunua mabasi mawili ya kwanza miaka ya themanini mara to baada ya kumaliza Forest hill kwa kutumiea pesa za mishen town. Hata hivyo inaonekana alikuwa na discipline kubwa sana kwenye hela kwani takriban miaka 40 sasa bado hajateteteleka. Kwa hiyo kutafuta hela ni jambo moja, ila plani nzuri ya kutumia hela hizo ni jambo kubwa sana
 
Ameishika njia ya morogoro -dar hana mpinzani,biashara anaijua
 
mabasi ya kwanza ya Aboud yalinunuliwa nadhani kati ya mwaka 81 na 82 au 83 hivi. Mtaji wa kwanza wa Aboud kwenye mabasi ulitokana na "misheni town" mzee. Ila jamaa ana akili, baada ya kutake off akaachana na hizo misheni town.
 
Wakati huo superfeo kaingiza scania GX sab.G7 angalau scania wamejitahidi finishing japo mchina bado yupo moto kwenye finishing na comfortability
Mchina hana confotability, siti ndogo mno na ukiegemea hupati raha yoyote, basi lina siti nyingi mno kwahiyo zipo karibu karibu zinaumiza miguu, sasa usiombe uwe mnene hizo siti ni changamoto,
 
Ameishika njia ya morogoro -dar hana mpinzani,biashara anaijua
Dar moro hata wewe ukipewa nafasi lazima utoke, ila kuna fitna za chini chini sana hapo ,
Hii ndo ruti fupi sana iliyo busy muda wote , ni kama vile sirari to mwanza ilivyo busy.na basi za kichina zinapenda sana aina hiyo ya route.
 
Aboud anaposikia SGR roho inamuuma sana, huenda aao ndio watakaohujumu SGR kusudi biashara zao zisiathirike.
Mkuu Sgr ipo mombasa to nairobi huu mwaka karibu wa tatu kama sikosei , na basi hazijaathirika, Train ina limitations kadhaa hasa katika ulimwengu wa tatu ! Cha kwanza ni connection zake , Mfano masoko ya mbao yapo buguruni hapo na Tazara ipo hapo hapo , , kule makambako soko la mbao halipo mbali na station ya Tazara na katika njia zake reli ya Tazara inapita uwani kabisa kwenye msitu wa mbao wa serikali ,Sao hill, Ulishawahi juiuliza kwa nini mbao bado inakuja na malori mjini hapo?
Abood hata Sgr wajenge kituo msamvu , bado ataongeza mabasi
 
Ni kama mwendokasi vs daladala. Daladala ilibidi ziwekewe vikwazo katika ruti zake wakati tulitegemea daladala ziachiwe ili zishindwe zenyewe(kifo asilia).
Picha inaanza nauli 400tsh vs 650tsh .
Kwa hiyo SGR labda ITASHINDWA kwenye nauli. Tofauti ya sh 3000 tu itafanya watu wapande mabasi.
 
Mchina hana confotability, siti ndogo mno na ukiegemea hupati raha yoyote, basi lina siti nyingi mno kwahiyo zipo karibu karibu zinaumiza miguu, sasa usiombe uwe mnene hizo siti ni changamoto,
Umepanda mchina ya bei rahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…