Tetesi: Usajili wa Mabasi ishirini mapya ya Abood

Tetesi: Usajili wa Mabasi ishirini mapya ya Abood

Basi 300 ni ngumu kwa kweli

Dar- moro kama mdau alivyosema after nusu saa basi inatoka. Masaa 14 ya kazi sawa na basi 28 ukizidisha mara 2 ni 56.

Turudi kwenye ruti zake zingine dar tunduma weka basi 5. Dar mbeya weka 5. Dar mwanza weka 5. Moro mwanza weka 5. Moro arusha weka 5.

Weka yaliyo service 30.

Total 120 hizo 300 zinatoka wapi. Story za vijiweni
[emoji1666][emoji1666][emoji106][emoji106]
 
Yani Una Danganya wazi wazi!!... Ukitoka Dar saa 11 alfajiri unafika Morogoro saa 3/4 sasa hebu tupe hii ya kila dakika 30 zinapishana vipi?!
Hahahaaaa mkuu ni sawa na kusema Bus moja kwa siku at maximum litaenda trip 3 (kila trip kwenda, kufika na kupakia masaa 3)...kwa trip za Dar Moro
 
[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]

Alafu Nina swali

Kwann Tankers n nyingi sana kuliko flat bed hz au gari za containers?
Biashara ya mafuta ina mzunguko mzuri na wa uhakika compared to dry cargo bro!

Na inalipa vizuri kuliko dry cargo.
Ndani ya mwezi mmoja tanker inapiga trip nyingi kuliko hao wengine..

Mfano, dar to congo within two weeks tayari gari imesharudi dar so kwa mwezi dereva akikimbiza trip mbili anatoboa kitu ambacho hawa wengine hawakiwezi piga ua!!
 
Majina Mapya na kuona watu wenye umri mdogo wanaendesha makampuni mengi makubwa ndio inaleta ubishani!!...Asas ni zao la kina Abri hawa Wana magari mengi ya mizigo nadhani wanaweza kuwa kwenye Top 5 Kwa Tanzania!!
Mkuu kuna hii kampuni inaitwa Blue Coast, jamaa wana gari nyingi mno nao kila mkoa lazima ukutane na hizi gari.
 
Mimi ninadhani hicho ni kiwango cha kawaida tu kwa kampuni kama Abood. Hata alipoingiza hizi zilizopo sasa ni hivyohivyo tu. Ninakumbuka ilikuwa sherehe pale Msamvu, misele ya kufa mtu roundabout wakipokewa na bodaboda.

Ninafikiri kwetu wateja, muhimu sasa ni kuletewa basi zilizo comfortable na rafiki kimatumizi. Yutong tunazoletewa ni za kikuda sana. Pot za kuchajia zinadumu miezi,hazifiki mwaka. AC halikadhalika—ikishabuma mtakoma humo kwenye basi. Siti pia ni ndogoo,ukiwa mrefu ama kibonge imekula kwako.

Ninajua haya ndo huchangia kushusha bei ya basi huko sokoni uchina. Lakini,kwakuwa kampuni ina uwezo, ingia dau kubwa, lete chache za ukweli wenye uwezo wapande kwa bei elekezi. Wateja wapo. Tunaona BM ana zile zenye daraja la kwanza na la pili. Kila siku daraja la kwanza zinajaa fasta.

Halafu Abood kama mnanisoma acheni ubahili. Katikati ya Dar na Moro jengeni kahoteli uchwara ka kupata bites na kujisaidia. Mnahama vihoteli, mnapeleka abiria vihoteli vinanuka choo utasema vyoo vya stend. Bites za kiwango cha chiiini.

Safari ni starehe jamani.
kuhusu hoteli sahau ndugu yangu......matajiri wote wanaishi kwa masharti kwamba wateja wanatakiwa wakale hoteli mbovu mbovu ...cheki BM , Shabiby etc
 
Hivi watu wanazijua vzuri dakika 30 kweli? Yaan tunapeana kamba za waziwazi kabisa. Huyo jamaa anadanganya waziwazi kabisa.
Hata mm naamini hajafkisha miatatu.,lakin huenda kweli zinapishana kila baada ya dk 30

Mkuu Kwan kila baada ya dk 30 gari kutoka haiwezkan, mfano stand gar hutoka kila baada ya dk 10 pale makambako ....Sasa Kama mtu una gari 50 ndan ya stand moja zitashindwa kupishana ndan ya dakika 30??,

Nilipokuwa nasoma advance njombe Kuna tajir mmoja wa makambako anaitwa mwenda mseke alikuwa kwenye peak kipind hiko, Ila kila nikitoka njombe shule inavofunga au nnavoenda shule inavofungua nlikuwa na pishana na mwendamseke tat had nne na Mimi nipo ndan ya mwendamseke ...huku kutoka makambako njombe ni lisaa limoja tu....inawezekana bos
 
Shida time table na wingi wa abiria wa route hiyo!!..Uongo ni mbaya sana lakini kabla hujapinga uongo inatakiwa uonyeshe ni vipi Haiwezekani!!...Dar/Moro hakuna Abiria wengi namna hii!!..
 
Stand ya msamvu nipo sana hapa. Zinaweza zikapishana hata baada ya dakika kumi na kunawakati zinaweza zikajaa hata mbili kwa mpigo lakini ipo siku zinapishana hata baada ya lisaa na nusu coz lazma ujue kunavisu vingine hapo stand navyo vinacompete na abood
 
Shida time table na wingi wa abiria wa route hiyo!!..Uongo ni mbaya sana lakini kabla hujapinga uongo inatakiwa uonyeshe ni vipi Haiwezekani!!...Dar/Moro hakuna Abiria wengi namna hii!!..
Mkuu , it's possible

Nilikua stand hapo mbezi majuz, sikukaa nusu saa pale, ziliondoka tatu ndan ya huo mda na nyingine ilikua inajaza wakat nasepa.. mbili zilisha ingia ndani zikisubiri folen

Hapo hapo Newforce , al said na wenzao nao wanatoa bus vile vile.. siku uko free katalii mchana pale utaelewa vizur, wako abiria wengi sana route ya dsm moro na dsm dom
 
kuhusu hoteli sahau ndugu yangu......matajiri wote wanaishi kwa masharti kwamba wateja wanatakiwa wakale hoteli mbovu mbovu ...cheki BM , Shabiby etc
Hamna, ni suala la uamuzi tu ndugu yangu. Tena inachangiwa na sisi wateja. Kama mnakuwa kimya, wanafanya watakayo. Tuna mifano kwa waliofanya hivi:

1. Dar express (Dar — Arusha); Korogwe

2. Kilimanjaro express(Dar—Arusha); Korogwe

3.Comfort coach(Dar—Iringa) (imebaki historia); Kitonga

4. Cate hotel (Dar—Dom); Morogoro

Tena Abood hahitaji likitu likubwaa, kwakuwa ruti yake hii Dar—Moro ni fupi. Kasehemu tu kasafi, kanavutia ka watu kujisaidia na kupata refreshments. Kampuni kubwa,kwanini wasinogeshe eneo hili?
 
Back
Top Bottom