Mimi ninadhani hicho ni kiwango cha kawaida tu kwa kampuni kama Abood. Hata alipoingiza hizi zilizopo sasa ni hivyohivyo tu. Ninakumbuka ilikuwa sherehe pale Msamvu, misele ya kufa mtu roundabout wakipokewa na bodaboda.
Ninafikiri kwetu wateja, muhimu sasa ni kuletewa basi zilizo comfortable na rafiki kimatumizi. Yutong tunazoletewa ni za kikuda sana. Pot za kuchajia zinadumu miezi,hazifiki mwaka. AC halikadhalika—ikishabuma mtakoma humo kwenye basi. Siti pia ni ndogoo,ukiwa mrefu ama kibonge imekula kwako.
Ninajua haya ndo huchangia kushusha bei ya basi huko sokoni uchina. Lakini,kwakuwa kampuni ina uwezo, ingia dau kubwa, lete chache za ukweli wenye uwezo wapande kwa bei elekezi. Wateja wapo. Tunaona BM ana zile zenye daraja la kwanza na la pili. Kila siku daraja la kwanza zinajaa fasta.
Halafu Abood kama mnanisoma acheni ubahili. Katikati ya Dar na Moro jengeni kahoteli uchwara ka kupata bites na kujisaidia. Mnahama vihoteli, mnapeleka abiria vihoteli vinanuka choo utasema vyoo vya stend. Bites za kiwango cha chiiini.
Safari ni starehe jamani.