Wengi hawafahamu kwamba kwasasa "DEREVA" gari limeshamshinda, linayumba yumba barabarani tu (Things Are Out Of His Hands And Out Of Control).
Na kawaida gari linapomshinda dereva basi kila atakachotaka kufanya ili kulikweka sawa na kila anavyopapatua, ndio anapo haribu zaidi na kulitoa nje ya barabara.
Sasa hivi kila mtu anajifanya mjuzi kuliko dereva, na ndio wanazidi kumchanganya na kumptoteza kabisa dereva. Huyu kawasha end-cator, yule kapiga honi, huyu kakunja sight-mirror zote (Waziri Wa Mambo Ya Nje alichokonoa mambo vibaya. AG na SPEAKER leo ndio "WAMECHOMOA BETRI" kabisa).
Kwa tulipofikia, gari linasubiri sababu tu lianguke na kuua abiria. Hakuna hatua yoyote ya kuliokoa gari wala kumsaidia dereva. Zaidi ya kumwomba mungu idadi ya wafu na majeruhi iwe ndogo.
● Kwa wenye akili na maarifa (hata wana CCM wenyewe) ndio maana wamekaa kimya na kujiweka pembeni. Wanatazama tu. Wanajua impact itakayotusibu kama taifa.
● Cha kujiuliza,
1) Kwanini siku ya leo "SERIKALI IMEONESHA INTEREST KUPITA KIASI" kuhusiana na hawa wabunge 19.???
2) Na kwanini bunge (Speaker) ameonesha "INTEREST KUPITA KIASI" kuhusiana na hawa wabunge 19.???
■ Nchi ina mihimili mitatu. Mihimili miwili tayari (Serikali na Bunge) vimeshakuwa "BIASED". Umebakia mhimili mmoja tu "MAHAKAMA".
■■■ Kwanini nasema "KWA TULIPOFIKIA, GARI LINATAFUTA SABABU TU YA KUANGUKA NA KUUA ABIRIA"???
Principle kuu ya utawala,
"Binaadamu ana mahitaji makuu, ambayo ni "Chakula, Matibabu na kuijua kesho yake". Binaadamu hawatawaliwi kwa nguvu bila hayo matatu na utawala ukafanikiwa.
Nature ya binaadamu, akiwa ameshiba basi anakua binaadamu na anatawalika kirahisi, ila akiwa na "NJAA" anakua mnyama na muogope kama Covid-19 au HIV AIDS!!!
JIBU.
Sisi kama taifa, asilimia 98% ya raia wanalalamika hali ni ngumu kupita kiasi (Hawana pesa kukidhi "Kupata chakula, matibabu na hawaijui kesho yao). Serikali nayo haina pesa kujiendesha yenyewe kupelekea kuongeza kodi kwa raia wasio na kipato.
Raia wangekua na pesa ya kukidhi mahitaji yao. Basi dereva angefanikiwa kuliweka gari sawa.
Hili ni "TIME BOMB (BOMU)" linalosubiri muda tu ufike liripuke.
USHAURI KWA CHADEMA.
Wakikaidi "VITISHO VYA A.G NA SPEAKER" na wakafanya maamuzi ya kuwafukuza "UWANACHAMA" hao 19 waliosaliti, kisha wakaongeza "PRESSURE ZAIDI". Dereva watamchanganya zaidi na kupindua gari ndani ya muda mfupi sana.
Wakiamua kufunika kombe ili mwanaharamu apite (Wasipo wafukuza hao wasaliti 19 uwanachama) basi gari litapunguza kasi kidogo, pengine dereva akajitambua na gari litadondoka upande waliokaa wao na kuwaua (Chama kitakufa na kupoteza wanachama kama CUF ya Lipumba).
(Natoka kijiji cha jirani na rafiki yangu kwa miguu hapa, tumetoka kupata kilevi cha kienyeji mubashara, tunaelekea kijijini kwetu mwendo wa masaa 4, tukalale)