USHAURI: Halima Mdee na wenzake wafukuzwe CHADEMA

USHAURI: Halima Mdee na wenzake wafukuzwe CHADEMA

yaani hizi spana haziingii kwenye vichwa vya vijana wa kitanzania,sijui wanakula chakula gani!!!!
 
Halima akibaki atatumika na mfumo kuwasumbua sana Chadema

Mbowe simama kiume, weka urafiki wako na Halima pembeni, Mfukuze kwa maslahi ya chama lakini urafiki wenu binafsi uendelee.

Halima sasa hivi ni kama nyoka aliyejeruhiwa, Hana imani tena na chama kuwa ni sehemu salama pa kuaminika tena, kwa hiyo egemeo lake litakuwa ni sytem, wakimalizana naye ataunga mkono juhudi kwa sababu hana nafasi tena kwenye siasa za upinzani.

Mbowe, Piga nyungu braza, piga sanitizer tuondoe hawa Covid-19, huku uraiani wananchi wana hasira kinyama dhidi ya tendo la usaliti walilofanya hawa watu.

Sasa the ball is in your court ama uiue Chadema mazima kwa kuwakumbatia hawa wasaliti au ulinde heshima na imani ya taasisi ya Chama ili chama kizidi kujisimika katika mioyo ya wananchi

Ligeuze hili tukio kama blessing in disguise ili kuzidi kupata heshima ya umma, na kuigeuzia kibao CCM ionekane ni chama cha hovyo na cha udanganyifu
 
Mabibi na mabwana ku kikao cha kamati kuu kesho, dalili za kuhujumiana na kutishiana nyau hapa na pale zimeshaonekana.

Mambo ya msingi sana kuzingatiwa kwa kesho:

1. Hapa tulipo ni katika yatokanayo na uchaguzi haramu ambao proceeds zake haziwezi kuwa halali. Si zaidi wala si pungufu ya hapo.

2. Hayupo mtu awaye yote katika CHADEMA ambaye ni indispensable. Ukweli mchungu, makaburi yamejaa watu ambao walikuwa so much indispensable!

3. Maridhiano kama ambavyo CHADEMA imekuwa inaitisha kila uchao na mahasimu wake, ni muhimu pia yakafanywa kwa vitendo ndani ya CHADEMA yenyewe. Kama kina Halima wanatubu na kuomba kusamehewa, chonde chonde ndugu zangu.

4. Jitihada zifanyike kumwezesha Mh. Lissu kushiriki kesho kamati kuu hata kama ni kwa voice link. Ushauri na maono ya Mh. Lissu kwenye hili ni muhimu sana.

Wadau na wakaongezee kwa mustakabala mwema zaidi wa CHADEMA.

Hili ni letu. Si la chama mboga mboga. Wasituingilie tunaposafisha nyumba yetu. Nia na uwezo wa kulikabili hili vilivyo tunao na hatuhitaji msaada wao.

Amandla!

Mungu ibariki CHADEMA.
 
Halima mdee Mbunge wa viti maalum [emoji23][emoji23][emoji23]

Mbowe mjanja sana hapo anataka kula cammision Kama wakala wa Tigopesa no way....

WABUNGE WOTE 19 KWA MWENZI ATAKUSANYA IZO PESA KWA MIAKA 5....
 
Yani CHADEMA nilikuwa nakiamini na kukipigania, but sasa ni chama cha hovyo kabisa. Nitakaa tu bila ufuasi wowote ule
 
Yani CHADEMA nilikuwa nakiamini na kukipigania, but sasa ni chama cha hovyo kabisa. Nitakaa tu bila ufuasi wowote ule
Wenye akili waliondoka alipokaribishwa Lowassa, mtu yeyote aliyeshuhudia Lowassa akitukanwa na viongozi wa CHADEMA majukwaani enzi za Dr Slaa na bado akashuhudia Lowassa akipitishwa bila kupingwa kugombania Uraisi kupitia UKAWA na bado akaendelea kuwa CHADEMA ni wa kupimwa akili yake. Hii ya Halima Mdee ni cha mtoto. Tumewaambia siku zote hicho chama kipo kimaslahi hamkuelewa, na kesho hafukuzwi mtu. Kwa hilo naweza kubet hela yoyote niliyonayo.
 
Kama Halima alipewa baraka na Mbowe katika mchakato wa uteuzi uliogubikwa na sintofahamu,kiasi cha Kamati kuu ya chama kutoweza kuteua majina ya 19 na kuyawakilisha NEC.
Sioni kwa nini anaweweseka, zimebaki saa chache akaielezee kamati kuu ni utaratibu gani ulitumika mpaka wakaapishwa.
Bila shaka kamati kuu itafikia uamuzi muafaka baada yakuwasikiliza wadau wote.
 
Lissu ni mkimbizi wa hiyari huko Ubelgiji. Hawezi kushiriki siasa za Tanzania, ndio masharti ya ukimbizi wake.
 
Lissu ni mkimbizi wa hiyari uko Ubelgiji. Hawezi kushiriki siasa za Tanzania, ndio masharti ya ukimbizi wake.

M-CCM unawahi seat ya mbele pamoja na kuwa hili haliwahusu? Uliona angalizo hili:

"Hili ni letu. Si la chama mboga mboga. Wasituingilie tunaposafisha nyumba yetu. Nia na uwezo wa kulikabili hili vilivyo, tunao na hatuhitaji msaada wao."

Kusema ukweli kuwashwa, mnawashwa. Siyo siri.

Habari mbaya kwenu ni kuwa, msiyemtaka wala kumpenda atakuwapo mkutanoni.
 
WAFUKUZWE? Mbona fresh tu,wamekamilisha misheni walizotumwa,wanarudi 'nyumbani' na maisha ya kisiasa yanaendelea kama kawaida.Wale hawana cha kupoteza hata wakifukuzwa
 
Wengi hawafahamu kwamba kwasasa "DEREVA" gari limeshamshinda, linayumba yumba barabarani tu (Things Are Out Of His Hands And Out Of Control).

Na kawaida gari linapomshinda dereva basi kila atakachotaka kufanya ili kulikweka sawa na kila anavyopapatua, ndio anapo haribu zaidi na kulitoa nje ya barabara.

Sasa hivi kila mtu anajifanya mjuzi kuliko dereva, na ndio wanazidi kumchanganya na kumptoteza kabisa dereva. Huyu kawasha end-cator, yule kapiga honi, huyu kakunja sight-mirror zote (Waziri Wa Mambo Ya Nje alichokonoa mambo vibaya. AG na SPEAKER leo ndio "WAMECHOMOA BETRI" kabisa).

Kwa tulipofikia, gari linasubiri sababu tu lianguke na kuua abiria. Hakuna hatua yoyote ya kuliokoa gari wala kumsaidia dereva. Zaidi ya kumwomba mungu idadi ya wafu na majeruhi iwe ndogo.

● Kwa wenye akili na maarifa (hata wana CCM wenyewe) ndio maana wamekaa kimya na kujiweka pembeni. Wanatazama tu. Wanajua impact itakayotusibu kama taifa.

● Cha kujiuliza,

1) Kwanini siku ya leo "SERIKALI IMEONESHA INTEREST KUPITA KIASI" kuhusiana na hawa wabunge 19.???

2) Na kwanini bunge (Speaker) ameonesha "INTEREST KUPITA KIASI" kuhusiana na hawa wabunge 19.???

■ Nchi ina mihimili mitatu. Mihimili miwili tayari (Serikali na Bunge) vimeshakuwa "BIASED". Umebakia mhimili mmoja tu "MAHAKAMA".

■■■ Kwanini nasema "KWA TULIPOFIKIA, GARI LINATAFUTA SABABU TU YA KUANGUKA NA KUUA ABIRIA"???

Principle kuu ya utawala,

"Binaadamu ana mahitaji makuu, ambayo ni "Chakula, Matibabu na kuijua kesho yake". Binaadamu hawatawaliwi kwa nguvu bila hayo matatu na utawala ukafanikiwa.

Nature ya binaadamu, akiwa ameshiba basi anakua binaadamu na anatawalika kirahisi, ila akiwa na "NJAA" anakua mnyama na muogope kama Covid-19 au HIV AIDS!!!

JIBU.

Sisi kama taifa, asilimia 98% ya raia wanalalamika hali ni ngumu kupita kiasi (Hawana pesa kukidhi "Kupata chakula, matibabu na hawaijui kesho yao). Serikali nayo haina pesa kujiendesha yenyewe kupelekea kuongeza kodi kwa raia wasio na kipato.

Raia wangekua na pesa ya kukidhi mahitaji yao. Basi dereva angefanikiwa kuliweka gari sawa.

Hili ni "TIME BOMB (BOMU)" linalosubiri muda tu ufike liripuke.

USHAURI KWA CHADEMA.

Wakikaidi "VITISHO VYA A.G NA SPEAKER" na wakafanya maamuzi ya kuwafukuza "UWANACHAMA" hao 19 waliosaliti, kisha wakaongeza "PRESSURE ZAIDI". Dereva watamchanganya zaidi na kupindua gari ndani ya muda mfupi sana.

Wakiamua kufunika kombe ili mwanaharamu apite (Wasipo wafukuza hao wasaliti 19 uwanachama) basi gari litapunguza kasi kidogo, pengine dereva akajitambua na gari litadondoka upande waliokaa wao na kuwaua (Chama kitakufa na kupoteza wanachama kama CUF ya Lipumba).

(Natoka kijiji cha jirani na rafiki yangu kwa miguu hapa, tumetoka kupata kilevi cha kienyeji mubashara, tunaelekea kijijini kwetu mwendo wa masaa 4, tukalale)
 
Back
Top Bottom