Heshima kwenu wana jamvi! Niende moja kwa moja kwenye mada husika,
Niliweka utaratibu kuwa kila siku nikirudi kazini nampa 10000 mwanamke wangu ambaye naishi nae na nilimkuta ana mtoto, mdogo wa kiume mwenye kama miaka minne hivi na tunaishi wote watatu,hiyo hela haitumiwi hadi mwisho wa mwezi ambayo inakuwa 300k
Cha ajabu mwezi wa kwanza tunapiga hesabu nakuta 240k namuuliza ananiambia pacha wake alimwazima akampa,kumbuka hapo hakunishirikisha,nikakausha japo haikurudi, mwezi unaofuata katikati nikiwa kazini ananipigia simu na kuniambia sujui kuna chuma ulete humu ndani maana sioni jela na kuna 20tu sikumjibu kitu nimerudi nyumbani, na kuoga, kula na kuingia kitandani alipokuja na kuanzisha ule mjadala nikamwambia kuanzia kesho sitakupa hela yeyote utunze zaidi y kukupa hela ya kula,usuka na Ziad, maana kiweka hela wewe naona huwezi,
Cha ajabu nipo zangu huku JF bado ananiomba game km hamna kilichotokea, tuna miezi nae mitatu tangu tuanze kuishi wote, hela ya kula huwa naacha tena ya wiki, kusuka,sijui wi fi vyote najali je wakuu mbele yetu mnaionaje?
Naombeni ushauri bila matusi,kebehi, tupo hapa kujifunza na kuelimishana! Karibuni wakuu;