Ushauri: JKT kwa Mujibu wa sheria ifutwe, badala yake vijana wapelekwe VETA miezi 3 au 6

Mawazo yangu:-

JKT bado ni muhimu, vijana wajifunze UTII, UVUMILIVU, UKAKAMAVU, Mbinu za medani kiasi kisha watumikie kujenga Taifa kwa cheo cha 'Service Man / Woman' kwa muda huo wa miezi mitatu au sita kwenye hizo fani za VETA. (Labour Camps)

Tuna kizazi legelege sana wasiojuwa hata uzalendo.

Niishie hapa kwanza.
 
JKT sio uzalendo,kuna watu wengi tu wamepitia huko lakini ni wezi na wahujumu uchumi wakubwa serikalini!!
 
Habari zenu wanajukwaa?

Ngoja nijikite kwenye lengo la uzi. Naishauri serikali sasa wabadili mwelekeo katika kuelekea serikali ya viwanda.
Vijana wanaomaliza kidato cha sita wapelekwe VETA kwa miezi 3 ili wakapate mafunzo ya awali (basic) ya ufundi mbalimbali.

Kwa kufanya hivi itasaidia kuwaandaa vijana wenye ujuzi mbalimbali mitaani. Kuna kozi nyingi tu ambazo kijana akizipata kwa miezi 3 anaweza kuamka na kujiajiri au hata kuajirika as general helper au fundi mwanafunzi.

Binafsi nimepitia JKT Mujibu wa sheria Ruvu na nilibahatika kupata ajira kupitia gamba la JKT ila wenzangu wengi wamemaliza digrii na hawana kazi mitaani.

Serikali inatumia kiasi kikubwa sana kumrecruit kijana mmoja wa jkt kwa miezi 3 au 6. Ile fedha ingetosha kumlipia ada VETA na akimaliza miezi 3 akapewa kamtaji.

Viongozi natumaini mtalitendea kazi suala hili.
Naunga mkono hoja. Natumaini viongozi wa nchi hii pia huwa wanapekua kurasa za JF. Kama nchi tutasogea hatua zaidi kwenda mbele.
 
Habari zenu wanajukwaa?

Ngoja nijikite kwenye lengo la uzi. Naishauri serikali sasa wabadili mwelekeo katika kuelekea serikali ya viwanda.
Vijana wanaomaliza kidato cha sita wapelekwe VETA kwa miezi 3 ili wakapate mafunzo ya awali (basic) ya ufundi mbalimbali.

Kwa kufanya hivi itasaidia kuwaandaa vijana wenye ujuzi mbalimbali mitaani. Kuna kozi nyingi tu ambazo kijana akizipata kwa miezi 3 anaweza kuamka na kujiajiri au hata kuajirika as general helper au fundi mwanafunzi.

Binafsi nimepitia JKT Mujibu wa sheria Ruvu na nilibahatika kupata ajira kupitia gamba la JKT ila wenzangu wengi wamemaliza digrii na hawana kazi mitaani.

Serikali inatumia kiasi kikubwa sana kumrecruit kijana mmoja wa jkt kwa miezi 3 au 6. Ile fedha ingetosha kumlipia ada VETA na akimaliza miezi 3 akapewa kamtaji.

Viongozi natumaini mtalitendea kazi suala hili.
Wazo zuri sana
 
Kwani jeshi ni utashi wa vijana wote?
Wanapelekwa kwa mujibu wa sheria na huko VETA wapelekwe kwa mujibu wa sheria. Siku amemaliza university hana pa kushika atatua kile alichopewa VETA.
Lengo la jkt Ni kuwa na reserve army, wakati wa Vita vya Kagera jkt ndio waliotangulia vitani na ilikuwa lazima, sioni busara kuwa na mafundi selemala wa akiba
 
JKT Bado inaumuhimu wake Mkuu bora ingekuwa ukimaliza form four unaenda veta kupata technical skills haijalishi ulisoma mchepuo gani yaani hii iwe ni (Basics).

Alafu form six waende JKT sasa.

Then chuo kikuu ukimaliza nenda katumie ujuzi uliuopata kujiajiri au kuajiriwa.

Nawasilisha
 
Kwa maoni yako hujakosea lakini hakuna nchi duniani ambayo inampeleka kijana wake kwenye kujitolea bure bure bila kuwa mtizamo wa mbeleni. Kuhusu kupelekwa veta si kila mtu akili yake ina mwamko wa ufundi.
Thank you sir, sio kila mtu ako na hio maarifa ya ufundi, na ndio unaona kuna vitu wa kutumia tu your mouth na akili, kuna degree kaa human resources, law na vingine ambazo hazihitaji uwe na ujuzi wa ufundi
 
Kozi gani Mkuu unaweza ukaisoma VETA kwa miezi3 ukaelewa au unarahisisha tu mambo?
 
Back
Top Bottom