Ushauri: JWTZ/JKT wajikite kwenye tafiti za kisayansi na teknolojia. Wabuni silaha zao wenyewe

Nimeshangaa sana jeshi kujikita kwenye biashara hadi za fremu, nchi za wenzetu majeshi yana idara za teknolojia na utafiti achilia mbali mambo ya silaha bali hata mambo mengineyo yanayohusisha sayansi na teknolojia. Nilitarajia jeshi liwe na idara iliyojikita kwenye uvumbuzi wa kiteknolojia na utafiti kwenye kilimo, mifugo, uvuvi, misitu, teknolojia za ujenzi, uchimbaji madini, gesi, mafuta, makaa ya mawe, vyombo vya moto, satellite/radar kwa ajili ya ulinzi, utafiti wa anga za juu nk.

Ili kuwezesha haya jeshi linatakiwa liwe na chuo chake cha sayansi na teknolojia ambapo watakuwa wanafundisha taaluma mbalimbali kwa vijana wenye ufaulu mkubwa ambao watakuwa recruited jeshini kuanzia kidato cha nne, kidato cha sita, na vyuo vikuu.​
 
Jeshi linaloonea raia ni jeshi lililokosa ubunifu
 
Chimbuko la tafiti zote za kisayansi katika nchi inayojielewa huanzia kwenye Majeshi yake, sisi kwetu hapa majeshi yetu yamejikita kwenye kunusa nani anakwenda kinyume na matamko ya Rais.

Bado tuna safari ndefu, isitukatishe tamaa.
 
Jeshi La TZ ni la sita duniani ????????

Nahis umekosea
 
Wana kiwanda cha Maji pia,lakini vilevile ni mabingwa wa kupasua vitofa kwa vichwa na kuchapana na mirunda mgongoni wakati wa sherehe za kitaifa.
 
Brand yao ya maji sijui iliishia wapi, wana hadi Pharmacy ya Wholesale Mwenge..

Jeshi na Biashara za uchuuzi..

Tusubiri tuone....
Hivi hizo pesa CAG huwa anakagua mahesabu yake au ndiyo Bakishishi ya Wakulungwa!
 
Uko sahihi mkuu,jeshi letu kuitisha press kwasababu ya nguo binafsi inanisikitisha sana...... Press ya taasisi kama jeshi letu inatakiwa waje na jambo mahususi lenye impact Kwa jamii
Kama kule Gabon na Niger au siyo![emoji1787][emoji1787]
 
Wao hayo hayawahusu Mkuu. Wanathamini zaidi mavazi kuliko mambo ya msingi. Yaani kwa akili zao hizo wako radhi kutetea sare na nembo zao kuliko hata lengo lao la msingi ambalo ni KULINDA MIPAKA YA NCHI IKIWEMO BANDARI, RELI, BARABARA KUU , VIWANJA VYA NDEGE n.k!

Tuna safari ndefu sana kama Taifa kuelekea nchi ya AHADI.

Halafu utashangaa wataanza kuwatafuta kina Burkinabe , Bujibuji Simba Nyamaume et al na kuwafungulia kesi za ajabu ajabu au kuwapoteza kabisa kwa sababu tu ya kuwaambia ukweli!
 
Hawa hapa sasa!!![emoji1787]
Your browser is not able to display this video.
 
Usikariri kazi moja kama mnduku elewa neno kama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…