Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Mkuu Maono Makuu, kwanza asante kwa mchango huu, na kweli wewe ni maono makuu!, nimeguswa sana na mchango wako, haswa ulipozungumzia Vietnam, hili neno "for others to survive, others must die!", kitaaluma mimi ni mtangazaji, uandishi ni kwa kujitolea tuu for the love of it!, kama ni kuandika humu, nimeandika sana, wenye macho wameona na amini usiamini hao viongozi tunaowaandika humu wanaona na wanasoma, wengine wana change for the better kutokana na michango ya jf, lakini hawana ujasiri wa kusema asante!, hivyo we are doing something!.

Kwa vile mimi ni mtangazaji, bado najipanga kuzivurumisha hoja zangu kwenye talk show program, kitu cha kwanza ni kujenga kwanza mazingira bora ya familia, kuhakikisha whatever happens to you, usimtese mke na watoto by dying for others to survive, nakaribia kusimama imara, na baada ya kusimama, kiukweli nitawalipua vilivyo ili kuhakikisha Tanzania ni nchi ya katiba inayoheshimiwa inayofuata the rule of law na sio utashi wa viongozi wenye viashiria vyote vya udikiteta na utawala wa kiimla!.

Pasco
 
Wazalendo wote hutakiwa kujitoa muhanga kulinda uhuru wao au kutetea haki, hata ikibidi kumwaga damu na kupoteza uhai wao.
Nchi nyingi zimekombolewa kwa namna hiyo na Tanzania tulikuwa mstari wa mbele.

Tatizo la sasa na hawa Ukuta, ni kuwa viongozi wanataka kuwatoa kafara wafuasi wap pasipo kuwa na malengo thabiti ya wanachokitafuta zaidi ya umaarufu wa kisiasa wa muda mfupi. Cheap political gains, tena za viongozi vigeugeu wasiosimamia maneno yao.
Wasiomaliza jambo lolote. Watu wasioamini na kusimamia maneno yao wenyewe.

Ni kweli kama unavyosema, wale waliotolewa kafara Arusha ilizaa matunda gani zaidi ya kutafuta umaarufu wa kisiasa?
Wameshasahauliwa na hakuna anayejali chochote. Hii ni dhambi ya kisiasa na kijamii.
 
Na wana mwanasheria nguli kuliko wote Tanzania.
Mkuu Ibambasi, kwa upande wa wanasheria nguli, kimajina, ni kweli Chadema ina washeria nguli ki vyeti tuu vya sheria na majina makubwa, lakini hawana lolote wala hawana msaada wowote wa maana kwa Chadema!.

Infact, kuna baadhi ya madudu, Chadema inayafanya kutokana na kuwategemea wanasheria hawa!.

Hebu soma hapa
Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele ...
Ushauri wa Bure kwa CHADEMA: Heri Nusu Shari Kuliko Shari Kamili ...
CHADEMA Haina Mamlaka kumzuia yeyote Kuhudhuria BMK! UKAWA ni ...
Tundu Lissu kutoishukuru JF na Pasco maana yake nini ...
Vurugu za Bungeni: Mhe.Tundu Lissu, Anastahili Adhabu Kali?!. Ni ...
Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu!, Unammaliza ...

Pasco
 
Mkuu Jozi, usemayo ni kweli, ndio maana nimewashauri wana Chadema, wasikubali kuburuzwa kama nyumbu!, kwanza waangalie jinsi Chadema ilivyo wa take care wale wahanga wa yale maandamano ya mwanzo, na wakiishajiridhisha, ndipo nao wajitoe kuifia Chadema!.

Pasco
 
Safi Sana Pasco
Wakati Unaongea hayo mkumbuke pia Ferdinand Marcos Dikteta wa ufiilipino kilichomtoa madarakani usidhani ni rahisi Sana Kama akili yako ndogo inavyokutuma
 
Ni kweli Rais anaonekana kuwa na nia nzuri. Ila means za kuachieve sidhanI kama anazo. Priorities zake zinanipa mashaka. Kama unataka kuondoa umaskini vitu muhimu ni chakula, mavazi na malazi. Ndiyo maana hata nchi zilizoendelea wasio na kazi hupewa malazi na pesa za kujikimu kwa ajili ya chakula na mavazi.

Kuwaambia wananchi kuwa hawatapata misaada ya chakula wakati hujawawezesha kupata pembejeo za kilimo ni kuwaonea. Wakati huo huo wote tunajua hali ya hewa ya sasa kidunia ilivyotuadhiri. Vilevile nilitegemea bidhaa za ujenzi kushuka bei ili watu waweze kujenga walau nyumba za tofari na mabati. Lakini tumeamua kununua ndege kwanza na kuhamia Dodoma!!

By the way sidhani kama kuna Rais yeyote aliyepita ambaye hakuwa ba nia njema. Cha kujiuliza ni kwa nini hawakufanikiwa. Na ni kwa vipi huyu atafanikiwa .... Maana Watanzania ni wale walewale!!!
 
Amen Mungu u nawe Kwa kusimamia ukweli
 
Unajua kwa tanzania elimu ya siasa na uraia kuna mapungufu sana ………
Kiukweli wapinzani pamoja na serikali wote wana maeneo wanakosea pia wanapatia …………
Tukianza na wapinzani…………… blah blah blah…………
???????!!!!!!
Ccm???!!!
 
Tofauti na Pasco alivyokujibu mimi nasema huyu raisi tulienae bado hajafika kiwango cha udikteta wa kweli kama madikteta wengi wa kweli walioacha alama katika dunia hii walikuwa nacho.

Kifupi tu magufuli bado anajifunza udikteta na sasa hivi ni sahihi kumwita dikteta uchwara, na hii ni kwasababu amekubali kumezwa na mfumo wa chama chake ambacho kimsingi ndio kimelea au kufuga hao mafisadi anao deal nao leo hii.

CCM ndio kichuguu cha mafisadi katika nchi hii ni nani anaepinga hili?

Ni ndani ya CCM utamkuta Chenge ambaye kila kashfa nzito ya kifisadi iliyoitikisa nchi yupo na kuna ushaidi wa kutosha kabisa!!... sasa tangu humjue Magufuli wewe binafsi ni lini uliwahi kumskia hata akiongelea ufisadi wowote wa change ?
Ni ndani ya CCM utakutana na mtu mwenye majivuno prof.Muhongo na amewahi kutuhumiwa kwa ufisadi mzito hadi kufikia hatua ya kujiudhuru, lakini cha ajabu mtu huyo huyo baadae anakuja kuteuliwa kwenye nafasi ile ile, katika wizara ile ile aliyokuwa akiisimamia na ikakumbwa na ufisadi tena na mtu ambae anajinasibu kuwa ni adui namba moja wa ufisadi...!! sasa haya si maajabu?? Only in rotten country like Tz.

Hiyo ni mifano miwili tu niliyokupa kuonyesha huyu mkuu sio dikteta wa kweli kama wengi wanavyomchukulia, udikteta wake una mipaka na hana uwezo wa kuwagusa elites wa nchi hii ambao ufisadi wao tunaujua..!!
Kama kweli anataka kukomesha ufisadi nchii hii, baasi humo humo ndani ya chama chake aanze kupapiga deki sababu ndio store ya mafisadi na muda wote pana vumbi ya mafisadi subiri chaguzi ndogo zifike ujionee.

Umesema kuwa anaonekana kuwa na uchungu na maisha ya kimaskini wanaoishi wanainchi anaowaongoza, sawa kwa hilo anastahili pongezi nyingi lakini tatizo lipo kwenye strategies, je ni mbinu gani sahihi zitumike hili kuleta hiyo economic justice pasipo kuwepo na athari zozote hapo baadae!!?

Hapa ndio tunakuja kuona athari kubwa za huo udikteta bandia alionao, Magufuli anajifanya yeye ni fascist kwamba kila kitu anaamua yeye na hao washauri wake hawana maana tena kwake... na kwa bahati mbaya sana hana utalaamu wowote katika maswala ya kiuchumi na hili swala la kuleta economic justice au poverty reduction lina hitaji wabobezi wa hali ya juu mno kiuchumi.

Sasa basi kwa sababu maamuzi katika kila jambo yanatolewa na mtu mmoja pekee tu hilo halitokaa liwezekane.. badala yake tutegemee kuona hasara na mipango mingi ya kutatua matatizo ya kiuchumi ikifeli huku wanaoumia wakizidi kuumia zaidi.
Tutegemee kuona bidhaa mbalimbali zikizuiliwa kuingizwa nchini na kuruhusiwa tena baadae huku zikisababisha mfumuko wa bei, tutegemee kuona kuzorota kwa soko huria kwa sababu ya ongezeko la kodi sizikokuwa na ulazima, tutegemee kuona uhaba wa ajira sababu ya kukosekana kwa mipango mathubuti inayotekelezeka mfano waalimu hadi leo haijulikani hatima yao ni nini.

Mwisho kabisaa tutegemee kuona nchi kufika mahali kusikojulikana ambako hata dereva wake mwenyewe hapajui, na hata hivi ninavyoandika hapa maelezo haya muda huu tayari nchi hii iko safarini kuelekea huko kusikojulikana.
Yangu macho.
 

Sasa huu mkwara aisee ,,,kama tu kuito ccm madarakani mmeshindwa leo kumng'oa huyuu
 
Mkuu Pasco nafikiri huu msemo wa "mwenye nguvu mpishe" hauna mashiko kwenye siasa. Na sio tu kwenye siasa hata ktk maisha ya kawaida. Mwenye nguvu kabiliana naye, pambana naye hata ufe ukipambana. Ni heri kufa ukipigania haki yako kuliko kuishi ukiwa mtumwa. Kama wenye nguvu tutakuwa tunawapisha wafanye wanavyotaka basi tukubali kuwa watumwa maisha yetu yote.
 
Mimi ninavyo Ona ni kwamba Raisi Kama ameliingilia muhimili mwingine iwe bunge au mahakama ni on administrative matters na sio katika decision making hivyo haina impact kwenye decision making zao to the extent ya kusema Raisi ni dictator au anaingilia mihimili mingine katika utekelezaji wa majukumu Yao ya maamuzi, kwani hizo safari nyingine hazihusiani na kufanya maamuzi
 
Umesoma ulichoandika na kujiridhisha? Sijakuelewa kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…