Pre GE2025 Ushauri kwa Mkurugenzi Mkuu wa TISS Kuhusu Kero Sugu ya Uhalifu wa Kiuchaguzi Unaofanywa na Wanasiasa Matapeli Wakati wa Chaguzi tangu 2010 hadi 2024

Pre GE2025 Ushauri kwa Mkurugenzi Mkuu wa TISS Kuhusu Kero Sugu ya Uhalifu wa Kiuchaguzi Unaofanywa na Wanasiasa Matapeli Wakati wa Chaguzi tangu 2010 hadi 2024

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Bara la Afrika ni mahali pekee kabisa hapa duniani ambako kuna Watu na Watawala wengi zaidi ambao hawajastaarabika kabisa katika maisha yao. That's why unaona kwamba sauti za milio ya risasi au milio ya mitutu ya bunduki haikomi kusikika.

The only suitable method of dealing with African Regimes is by means of Guns. Ndio maana unaona kwamba Wazungu wamewekeza pakubwa Sana katika masuala ya kutoa Misaada ya silaha za kupigania Vita ndani ya Ardhi iliyopo katika nchi za bara hili la Afrika.

So you are wasting your time and resources for nothing
Hapana usimkatishe tamaa mleta mada. Ingawa ushauri wake kapeleka kwa Mkurugenzi wa TISS ila tuna uhakika uko TISS bado wapo wazalendo kweli ambao wako tayari kusimamia maslahi mapana ya taifa na kusema No kwa CCM na ufedhuli wake.

I believe ipo siku hawa wazalendo waliopo TISS na hata JWTZ watafanya jambo kubwa la maana sana.
 
Huwezi kuwatenga TISS na madudu ya ccm kila nyanja, wanahusika, na, wanafaidika(kama taasisi, na, mmoja mmoja, baadhi),
Kufikria wizi unafanywa na Hawa jamaa hawajuhi, ni kututukana matusi,au kujaribu kujenga taswila kwamba kuna wana ccm wanaiba kura,samia, ikulu haijuhi,! Na, inafanya kila linalowezekana kuwakamata! Ni matusi ya nguoni kwa wa bongo, kuna methali yq kisomali inasema, "ngamia walioibiwa na mwenyewe, hawa wezi kupatikana! "
Ccm ndio wezi wa kura, harafu wanatafuta mwizi wamfunge! Hatapatikana milele!
 
View attachment 3242826
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akimwapisha Suleiman Abubakar Mombo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Ikulu ya Dar es Salaam , 11 Julai 2024.

I. USULI

Naandika dokezo la kisera, lenye kubeba taarifa za intelijensia ya kisiasa na kijasiriadola, kwa ajili ya kutetea rai ifuatayo:

Kwamba, kwa kuwa uhalifu wa kiuchaguzi unaofanywa na wanasiasa matapeli wakati wa chaguzi zetu umekithiri kwa miaka 15 sasa kutokana na mapungufu yaliyomo kwenye mifumo yetu ya kikatiba na kisheria, basi, tunapaswa kurekebisha ratiba ya uchaguzi mkuu wa 2025, kisha tufanye mageuzi ya kikatiba na kisheria, na hatimaye tufanye uchaguzi mkuu baadaye, na sio kinyume chake.

II. UTANGULIZI


Napendekeza kuanza dokezo hili kwa nukuu muhimu kuhusiana na mtazamo wa Chadema kuhusu Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika 2025.

"Mtu yeyote mwenye akili na macho ya kuona anajua kuwa chaguzi za nchi hii zimekuwa za hovyo sana na kwamba ni za hovyo kwa sababu mfumo mzima wa kiutawala wa nchi hii ni mfumo wa hovyo" -- Tundu lissu, Mwenyekiti CHADEMA.

“Hivyo, hatuzungumzii kususuia uchaguzi, hatutasusia bali tutaenda kuwaambia Watanzania, jumuiya ya kimataifa na walimwengu kwamba kama CCM na Serikali hawako tayari kufanya mabadiliko kwenye mfumo wa uchaguzi ili kuwepo chaguzi huru na haki, uchaguzi wa mwaka huu usifanyike kabisa” -- Tundu lissu, Mwenyekiti CHADEMA.


View attachment 3243758

Huu ndio msimamo ulioibuliwa na Chadema kuhusu kile ambacho baadhi ya vyombo vya Habari, kama vile gazeti la Mwananchi la leo, vinakiita “Njiapanda ya Chadema Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2025.”

Lakini, napendekeza kwamba, kutokana na uzito wa hoja yenyewe, hasa tunapaswa kuwa tunaongelea “Njiapanda ya Watanzania Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2025.”

Kwa njia ya swali, “njiapanda” inayoongelewa kwenye vyombo vya habari, ndani na nje ya Chadema pia, inaweza kusomeka hivi:

Je, kwa kuzingatia uhalifu wa kiuchaguzi ambao umekuwa ukifanyika nchini Tanzania tangu 2010 kutokana na uwepo wa milima, mabonde na makorongo yaliyopo kwenye uwanja wa uchaguzi wa vyama vingi nchini Tanzania, tufumbe macho na kuendelea na utekelezaji wa ratiba ya uchaguz mkuu wa Oktoba 2025 au tusogeze ratiba hii mbele kidogo ili uchaguzi huu ufanyike baada ya mageuzi ya kikatiba na kisheria kufanyika ili kusawazisha milima, mabonde na makorongo yaliyopo?

Kutokana na utafiti nilioufanya, dokezo hili linapendekeza kwamba, tunapaswa kusogeza ratiba ya uchaguzi mkuu mbele kidogo ili uchaguzi huu ufanyike baada ya mageuzi ya kikatiba na kisheria kufanyika ili kusawazisha milima, mabonde na makorongo yaliyopo kwenye uwanja wa kisiasa.

III. UTARATIBU WA UTAFITI (METHODOLOJIA)

Katika utafiti wangu nilikusudia kujibu maswali yafuatayo:
  1. Hoja ya Chadema kuhusu changamoto ya uhalifu wa kiuchaguzi nchini Tanzania inasema kitu gani kimaudhui na inao muundo gani kimantiki?
  2. Je, ni kweli kwamba kuna milima, mabonde na makorongo kwenye uwanja wa siasa za uchaguzi wa vyama vingi nchini Tanzania?
  3. Kama jawabu kwa swali la kwanza ni “ndiyo,” milima, mabonde na makorongo haya yamekuwa na madhara gani katika matokeo ya uchaguzi?
  4. Kutokana na majibu ya maswali haya mawili hapo juu, nah atua gani zichukuliwe tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.
Vyanzo vyangu vya taarifa ni kuona matukio kwa macho, kujadiliana na wadau baki walioona matukio kwa macho, na kusoma nyaraka kama vile sheria za Bunge, Katiba ya nchi, kusikiliza video, na makala nyingine kwa ajili ya kupanua maarifa yangu juu ya suala hili.

IV. MATOKEO YA UTAFITI

Hoja ya Chadema


Maneno ya Tundu Lissu kuhusu msimamo wa kisera wa chama chake juu ya umuhimu na ulazima wa kusogeza mbele ratiba ya Uchaguzi Mkuu ujao yamenukuliwa hapo juu.

Kwa maoni yangu, haya ndio maneno yanayotueleza msimamo rasmi wa Chadema. Maneno haya yanaweza kufafanuliwa katika muundo wa hoja rasmi kama ifuatavyo:

1. Kama tungekuwa na mifumo ya kikatiba na kisheria inayowanyima wanasiasa matapeli fursa ya kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwenye michakaato ya chaguzi zetu basi tungekuwa na sababu nzuri ya kushiriki Uchaguzi Mkuu Ujao kabla ya kufanyika kwa mageuzi ya kimfumo.

2. Lakini, uzoefu wetu kutokana na chaguzi zote za 2010, 2015, 2019, 2020 na 2024 unaonyesha kwamba tunayo mifumo ya kikatiba na kisheria inayowapatia wanasiasa matapeli fursa ya kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwenye chaguzi zetu, kiasi kwamba, kwa kipindi cha miaka 15, tumekuwa tukiongozwa na serikali haramu zilizotokana na mbinu haramu.

3. Hivyo, bila kufanya mageuzi ya kuboresha mifumo ya kikatiba na kisheria inayowapatia wanasiasa matapeli fursa ya kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwenye chaguzi zetu hatuwezi kupata serikali halalai iliyotokana na mbinu halali.

4. Kwa mujibu wa kifungu cha 22 katika Sheria ya Makosa ya Jinai (Sura ya 16, Toleo la 2002), kama ilivyotafsiriwa kwenye Kesi ya Abdallah Zombe na wenzake 12 dhidi ya Ephraim Chigumbi na wenzake wawili, Kesi ya Mahakama Kuu Na. 26/2006, kuna njia nne za mtu mmojawapo kushiriki katika kitendo cha uhalifu wa kiuchaguzi, kabla, wakati na baada ya mchakato wa uchaguzi:

(a) Ama kwa mtu huyo kutekeleza uhalifu wa kiuchaguzi kwa kutumia mikono yake mwenyewe; au

(b) kwa mtu huyo kumpa msaada wa aina yoyote mtu baki mwenye nia ya kutenda uhalifu wa kiuchaguzi na hivyo kumsaidia mtu baki kufanikisha utekelezaji wa uhalifu; au

(c) kwa mtu huyo kumpa ushauri mtu baki ili ajenge nia ya kutenda uhalifu wa kiuchaguzi na hivyo kumshawishi mtu baki kufanikisha utekelezaji wa uhalifu; au

(d) kwa mtu huyo kuficha taarifa muhimu zinazohitajika kwa ajili ya ama kuzuia uhalifu wa kiuchaguzi kutendeka au zinazoweza kusaidia kuwatia hatiani watu waliotenda uhalifu wa kiuchaguzi.

5. Hivyo, kama tunao wajibu wa kupigania ujio wa serikali halali iliyotokana na mbinu halali, basi, tunapaswa kupigania ujio wa serikali halali kwa kufanya mambo yafuatayo:

(a) Ama kujizuia na kumshawishi kila mtu baki kujizuia kutekeleza uhalifu wa kiuchaguzi kwa kutumia mikono yake mwenyewe; au

(b) Kujizuia na kuwashawishi watu baki kujizuia kutoa msaada wa aina yoyote kwa mtu mwenye nia ya kutenda uhalifu wa kiuchaguzi na hivyo kumfanya mtu baki asifanikishe utekelezaji wa uhalifu; au

(c) Kujizuia na kuwashawishi watu baki kujizuia kumhimiza mtu yeyote kujenga nia ya kutenda uhalifu wa kiuchaguzi na hivyo kumfanya mtu baki asifikirie kutekeleza uhalifu wa kiuchaguzi; au

(d) Kufichua taarifa muhimu zinazohitajika kwa ajili ya ama kuzuia uhalifu wa kiuchaguzi kutendeka au zinazoweza kusaidia kuwatia hatiani watu waliotenda uhalifu wa kiuchaguzi.

6. Kwa hakika, tunao wajibu wa kisheria na kimaadili wa kupigania ujio wa serikali halali, jambo linalomaanisha kwamba tunao wajibu wa kisheria na kimaadili wa kuzuia ujio wa serikali haramu, kwa sababu zifuatazo:

(a) Kisheria, ibara ya 28(1) ya Katiba ya Tanzania (1977) inampa kila raia “wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha uhuru, mamlaka, ardhi na umoja wa taifa.”

(b) Kimaadili, sheria ya maadili asilia inatupa jukumu la kutekeleza matendo mema na kuzuia matendo maovu, kwa kuhakikisha kwamba, kisiasa, inasimikwa serikali iliyotokana na wapiga kura halali, inayofanya kazi kwa niaba ya watu wote, na yenye kutekeleza majukumu yake kwa faida ya watu wote.

7. Kwa hiyo, raia wa Tanzania tunao wajibu wa kupigania uchaguzi utakaofanikisha ujio wa serikali halali na kupinga uchaguzi utakaofanikisha ujio wa serikali haramu. Hii ndio mantiki ya kaulimbiu isemayo kwamba “Bila Kufanya Mageuzi Kwanza Hakuna Kufanya Uchaguzi,” yaani “No Reforms, No Elections.”

Kwa ujumla, ni wazi kwamba hitimisho hili lisemalo linawaweka njiapanda baadhi ya wanachama wa Chadema wanaotaka kugombea Udiwani, Ubunge na Urais kwa tiketi ya Chadema.

Pia, ni wazi kwamba vyama vingine vinaweza kuendelea na maandalizi ya uchaguzi, maana hii sio sera yao. Na wanachadema wanaopinga sera hii wanayo hiari ya kutafuta jukwaa jingine la kisiasa lisilotambua sera hii ili wapewe fursa ya udhamini wanaoutaka.

Milima, mabonde na makorongo ya kisiasa

Tuhuma kwamba chaguzi zote za 2010, 2015, 2019, 2020 na 2024 unaonyesha kuwa tunayo mifumo ya kikatiba na kisheria inayowapatia wanasiasa matapeli fursa ya kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwenye chaguzi zetu, kiasi kwamba, kwa kipindi cha miaka 15, tumekuwa tukiongozwa na serikali haramu zilizotokana na mbinu haramu, nazi zinao ushahidi wa kuziunga mkono kama ifuatavyo:

(a) Uchaguzi unaosimamiwa na ma-WEO, ma-DED, ma-DC, ma-DAS, na ma-RAS unakosa uhuru, uwazi na ushindani wa kweli, kwa sababu wao ni watumishi wa serikali ya chama tawala, na hivyo kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwa faida ya chama tawala.

(b) Sheria za uchaguzi zinawaruhusu Watumishi wa umma kuvaa kofia za Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati w auchaguzi na hivyo kufungua milango ya uhalifu wa kiuchaguzi.

(c) Tume ya Taifa ya Uchaguzi imo kwapani mwa Rais wa nchi, ambaye ndiye huteua wajumbe wake, na hivyo kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria pekee kwa sababu ya kuyumbishwa na maagizo kutoka Ikulu.

(d) Tume ya Taifa ya Uchaguzi haina uwezo wa kisheria wala kifedha wa kusimika watumishi wake kwenye kila jimbo la uchaguzi kwa mujibu wa sheria.

(e) Katiba inamruhusu Rais wa nchi aliye madarakani na ambaye ni mgombea kuendelea kutekeleza majukumu yake ya Urais wakati wa kampeni za uchaguzi ilihali yeye ni Amiri Jeshi Mkuu, Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, na Msimamizi Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Jambo hili linafungua mianya kwa baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama, kama vile Jeshi la Polisi na TISS, kufanya uhalifu wa kiuchaguzi ili kumsaidia “bosi” wao kushinda.

(f) Katiba inaruhusu Rais wa nchi kushika nafasi ya mwenyekiti wa chama cha siasa, kabla na wakati wa uchaguzi, na hivyo, kufungua mlango wa Rais huyu kuvitumia vyombo vya ulinzi na usalama kwa faida ya chama tawala.

(g) Katiba na sheria zetu vinazuia matokeo ya uchaguzi wa Rais yanayobishaniwa kupingwa mahakamani kisheria. Hivyo, uhalifu wa kiuchaguzi kuhusiana na kura za urais hauwezi kukosolewa kimahakama.

(h) Sheria na Katiba havijapiga marufuku tabia ya uhalifu wa kiuchaguzi wa kugeuza mchakato wa uchaguzi kuwa mashindano ya kujaza fomu za wagombea, jambo ambalo linazalisha wagombea wa kupigiwa “kura za ndio au Hapana,” na hivyo kukiuka kanuni ya uchaguzi wenye ushindani.

Kwa sababu hizi zote, hitimisho la kimantiki ni kwamba ma-WEO, ma-DC, ma-DAS, ma-DED, ma-DSO, ma-OCD, ma-RSO, ma-RAS na ma-RC walioshiriki kwenye uhalifu wa kiuchaguzi ni wanasiasa matapeli waliotenda jinai na kuachiwa watembee huru mitaani kana kwamba hakuna kosa la kisheria wametenda.

Lakini baadaye kidogo watu hawa hawa ndio wanaonekana kusimamia amani na utulivu ("law and order") kwa kuhakikisha kuwa watenda jinai wanaadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

Undumila kuwili huu umeleta dharau kubwa kwa serikali tulizo wahi kuwa nazo tangu 2010.

Madhara ya milima, mabonde na makorongo haya

Makorongo haya kwenye uwanja wa siasa za vyama vingi yamekuwa na madhara ya kisiasa tangu zamani, hata kabla ya hayati Magufuli hajakanyaga Ikulu. Mfano:

(a) Mwaka 2010 na 2015 enzi za Kikwete

Katika zama hizi kulikwa na “vikosi kazi” vya kukomboa majimbo yaliyo hatarini.

Kwa kila jimbo ambalo tayari lilithibitika kuanguka mikononi mwa wapinzani, vikosi hivi vilikuwa vinashirikiana na baadhi ya ma-WEO, ma-DC, ma-DAS, ma-DED, ma-DSO, ma-OCD, ma-RSO, ma-RAS na ma-RC kufanya “ukombozi.”

Mfano mmoja ni ule wa Jimbo la Karagwe mwaka 2010. Mgombea wa CCM, Gosbert Blandes Begumisa, alipoteza jimbo hilo kwa tofauti ya kura zipatazo 500. Mgombea wa Chadema alishinda.

Kikosi kazi kikafika Karagwe haraka. Kiongozi wa kikosi kazi kile alikuwa ni Afisa Usalama aliyeitwa “Haule.” Wakachakachua takwimu Blandes akatangazwa mshindi.

Niliambiwa kuwa, Kila kikosi kilikuwa kinapewa magari, fedha taslimu na wakati mwingine helikopta. Na kwa kila jimbo lililokuwa linakombolewa “malipo ya kazi maalumn” yalikuwa fedha ipatayo TZS 100,000,000 (soma milioni mia moja).

Hivyo, wajumbe wa “vikosi kazi” hivi enzi za Kikwete walifanikiwa kujenga majumba, kununua magari, na kuanzisha biashara kubwa. Kwao, wakati wa msimu wa uchaguzi wajibu wao ulikuwa ni kuiba majimbo na ulikuwa ni msimu wa “mavuno” makubwa.

View attachment 3242827
Gosbert Blandes Begumisa, Mbunge wa zamani wa Karagwe

(b) Mwaka 2019 na 2020 enzi za Magufuli

Wakati wa JPM idadi ya “vikosi kazi” iliongezeka, kiasi kwamba uhalifu wa kiuchaguzi ikawa sera rasmi ya kila jimbo la uchaguzi. Ma-WEO, ma-DC, ma-DAS, ma-DED, ma-DSO, ma-OCD, ma-RSO, ma-RAS na ma-RC wote walipewa maagizo rasmi ya kusimamia ushindi wa wagombea wa CCM.

Uliotegemewa kuwa uchaguzi haali uligubikwa na uhalifu wa kiuchaguzi wenye sura zifuatazo:
  • Kutoandikisha wapiga kura kwenye ngome za wapinzani,
  • Kuwaengua wagombea wao wengi,
  • Kutowaruhusu mawakala wa vyama vya upinzani
  • Kuingiza kura feki (premarked ballots) kwenye sanduku la kura, na
  • Kutowatangaza wapinzani hata pale walipoonekana kushinda.
Hatimaye wapinzani hawakuambulia kitu.

(c) Mwaka 2024 enzi za Samia Suluhu Hasan

Wakati wa SSH utaratbu wa hayati Magufuli ulifufuliwa na kutekelezwa kikamilifu. Ma-WEO, ma-DC, ma-DAS, ma-DED, ma-DSO, ma-OCD, ma-RSO, ma-RAS na ma-RC wote walipewa maagizo rasmi ya kusimamia ushind wa wagombea wa CCM. Wapinzani hawakuambulia kitu pia.

Kwa mara nyingine tena, uliotegemewa kuwa uchaguzi haali uligubikwa na uhalifu wa kiuchaguzi wenye sura zifuatazo:
  • Kutoandikisha wapiga kura kwenye ngome za wapinzani,
  • Kuwaengua wagombea wao wengi,
  • Kutowaruhusu mawakala wa vyama vya upinzani
  • Kuingiza kura feki (premarked ballots) kwenye sanduku la kura, na
  • Kutowatangaza wapinzani hata pale walipoonekana kushinda.
Kwa mara nyingine tena wapinzani hawakuambulia kitu.

View attachment 3242833
Jakaya Mrisho Kikwete

Ni katika mazingira haya, kijana Afisa Usalama mmoja ambaye kwa sasa bado anafanya shahada yake ya kwanza ya Sheria katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania alibuni falsafa ya "R" nne, yaani "4Rs philosophy."

Hii ni falsafa yenye kumaanisha "Reconciliation, Resilience, Reforms and Rebuilding." Yaani, "Upatanisho, Ustahimilivu, Ukarabati wa mifumo, na Ujenzi wa Mifumo mipya," kwa maana ya "4U" kwa Kiswahili.

Katika falsafa ya "4R/4U" maneno "Upatanisho" na "Ukarabati wa mifumo" yanahusika zaidi kwenye changamoto za uchaguzi tulizoshuhudia kwa miaka 15 sasa.

Kunahitajika "Upatanisho" kati ya watu waliotangazwa washindi isivyo halali na washindi halali ambao hawakutangazwa na kisha wakadhulumiwa ushindi wao, wakapoyeza fedha zao za kampeni, na wakati mwingine kufulisika kabisa mara tu baada ya dhuluma hizo.

Aidha kunahitajika "ukarabati wa mifumo" ya uchaguzi ili kuziba mianya ya uhalifu wa kiuchaguzi unaofanywa na vyombo vya dola kama vile ma-WEO, ma-DC, Ma-DED, ma-DAS, ma-RAS na ma-RC.

Nje ya hatua hizi za kimakusudi, "falsafa ya 4R" au tuseme "falsafa ya 4U" itabaki ni ukasuku mtupu.

Na bahati mbaya kijana aliyeibuni hana uwezo wa kuidadavua zaidi maana bado ni "denti" na wakubwa zake wanampuuza kwa sababu hiyo.

Na kubwa zaidi ni kwamba wale wakubwa zake walioipokea hawaielewi vema maana wao hawajui vema mwasisi wa wazo alikuwa anafkiria nini.

View attachment 3243761
Albert Chalamia, RC wa Dar es Salaam, rafiki yake Joseph Selasini wa NCCR Mageuzi

V. MAPENDEKEZO YA HATUA ZINAZOPASWA KUCHUKULIWA

Kutokana na yaliyojadiliwa hapo juu, napenda kutoa wito na mapendekezo yafuatayo kwa Serikali, Bunge, Makanisa, Misikiti, Azaki, Wanazuoni wa Vyuo Vikuu na watu wote wenye mapenzi mema kwa Tanzania:

1. Kwa kuwa Tanzania sio dola ya Kiimla, wala Himaya ya Kifamle wala Taifa la Kijeshi, bali ni Dola ambayo ni Jamhuri ya Kikatiba na Kidemokrasia, inayofuata demokrasia ya vyama vingi vya siasa tangu mwaka 1992;

2. Kwa kuwa, sifa kuu ya dola ambayo ni Jamhuri ya Kikatiba na Kidemokrasia ni uchaguzi unaofanyika kwa uhuru, uchaguzi unaofanyika kwa uwazi, uchaguzi unaofanyika kwa haki na uchaguzi unaofanyika kwa ushindani wa hoja za kisera;

3. Kwa kuwa chaguzi za 2019, 2020 na 2024 zilifanyika kwa njia ya udanganyifu ulioratibiwa na matapeli wa kisiasa waliokuwa wanafuata nyayo za Hayati JMP;

4. Kwa kuwa udanganyifu wa kisiasa katika chaguzi za 2019, 2020 na 2024 ulitekelezwa na ma-WEO, ma-DED, ma-DC, ma-DAS, ma-DAS na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya sasa;

5. Kwa kuwa udanganyifu wa kisiasa ulifanikiwa kwa sababu ya uwepo wa mifumo mibovu ya kikatiba na kisheria;

6. Kwa kuwa sheria na Katiba ya sasa vinasabaisha kuwepo kwa uwanja wa uchaguzi usio tambarare bali uwanja wenye milima, mabonde na makorongo yanayowakandamiza wagombea wa vyama vya upinzani;

7. Na kwa kuwa serikali inayoingia madarakani kwa njia za udanganyifu inakuwa haina uhalali ikiwa ni sawa na serikali zilizokuwepo enzi wa ukoloni chini ya wazungu na serikali zilizokuwepo enzi za utumwa chini ya waarabu;

8. Hivyo basi, natoa wito kwamba, Serikali na Bunge vinapaswa kuandaa vikao maalum vya Bunge kwa ajili ya kupitisha Mabadiliko ya 15 ya Katiba ya Tanzania (1977) pamoja na marekebisho stahiki ya sheria za uchaguzi ili mambo yafuatayo yawezekane kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025:

(a) Sheria na Katiba vikataze ma-WEO, ma-DED, ma-DC, ma-DAS, ma-RAS kusimamia chaguzi.

(b) Sheria na Katiba vitamke kuwa chaguzi zote nchini zitasimamiwa na Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyo huru.

(c) Tume ya Taifa ya Uchaguzi iondolewe kwapani mwa Rais wa nchi kusudi iweze kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria pekee bila kuyumbishwa na maagizo kutoka Ikulu.

(d) Tume ya Taifa ya Uchaguzi iweke watumishi wake kwenye kila jimbo la uchaguzi kwa mujibu wa sheria.

(e) Katiba ikataze Rais wa nchi aliye madarakani na ambaye ni mgombea kuendelea kutekeleza majukumu yake ya Urais wakati wa maandalizi na uendeshaji wa kampeni za uchaguzi.

(f) Katiba ikataze Rais wa nchi kushika nafasi ya mwenyekiti wa chama cha siasa.

(g) Katiba na sheria zetu viruhusu matokeo ya uchaguzi wa Rais yanayobishaniwa kupingwa mahakamani kisheria.

(h) Sheria na Katiba vipige marufuku tabia ya udanganyifu wa kugeuza mchakato wa uchaguzi kugeuzwa mashindano ya kujaza fomu za wagombea.

(i) Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anayejua vizuri sana haya "mambo mambo" alisaidie Taifa kuondokana na hii Kero Sugu ya Uhalifu wa Kiuchaguzi, hata kama chama chake cha CCM kitangoka madarakani kwa sababu hiyo. Tanzania ni kubwa kuliko vyama vya siasa.

(j) Wanasheria wa Tanganyika Law Society watusaidie kuandaa miswada ya sheria zinazopaswa kuwasilishwa Bungeni muda wowote kwa ajili ya kutekeleza mapendekezo hapo juu. Washirikiane na Wizara ya Sheria na Katiba. Tumechelewa sana, hivyo inabidi tukimbie.

(k) Padre Charles Kitima akae na muumini wake mmoja Joseph Selasini ili kumkanya na kumwongoza kwenye sala ya toba. Huyu jamaa alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Walei Taifa, chini ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC).

Lakini anayoyafanya sasa hivi sio sawa kabisa. Anahujumu jitihada za kuimarisha siasa za vyama vingi nchini Tanzania. Tangu ampindue James Mbati wa NCCR-Mageuzi kazi yake ni kuhakikisha NCCR-Mageuzi wanatekeleza sera za CCM kwa moyo mkunjufu.

Mara nyingi vikao vyake na RC Chalamila vinafanyika pale Kisuma Hotel Magomeni. Kwa sasa Selasini amekuwa kama Lyatonga Mrem katika siku zake za mwisho. Anajikomba CCM hadi inatisha.

Joseph Selasini akiw anaongea na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

View attachment 3243765
Padre Kitima wa TEC ambaye ni Mlezi wa kiroho wa Joseph Selasini wa NNCR-Mageuzi

VI. MAPINGAMIZI NA MAJIBU YAKE

Mapendekezo yangu hapo juu yanaweza kupingwa na watu kadhaa kwa njia mbalimbali. Baada ya mapingamizi ninayoyatarajia na ambayo nataka kuyajibu kabla hayajaibuka ni kama ifuatavyo:

Pingamizi: “Hoja ni nzuri, utafiti mzuri, ila sio realistic, kwa maana kuwa hayana uhalisia kama tukiangalia muda uliobaki. Tuachane na utopian politics”

Majibu: Naamini kuwa hoja yangu inatekelezeka kwa kuwa kazi ya kuandaa miswada kwa hati ya dharula inawezekana. Bajeti ya kuitisha Bunge maalum kwa ajili ya kupitisha miswada hiyo iko ndani ya uwezo wa serikali. Wabunge bado wapo maana Bunge halijavunjwa.

Pingamizi: “Uchaguzi is a process inayosimamiwa na serikali. Hakuuna siku serikali iliwahi kuahirisha uchaguzi mkuu kwa kuusogeza mbele kwa sababu ya kurekebisha jambo lolote.”

Majibu: Ukweli kwamba huko nyuma hatujawahi kufanya jambo Fulani hakumaanishi kuwa leo au kesho hatuwezi kufanya jambo hilo. Tukumbuke kuwa uchaguzi upo kwa ajili ya watu na sio watu kuwepo kwa ajili ya uchaguzi. Pia, ratiba ya uchaguzi sio msahafu.

Pingamizi: Tundu Lissu na Chadema yake hawana uwezo wala mamlaka ya kusema “no reforms no election” na kauli yake ikatekelezwa na serikali. Kwa hiyo, hakuna mageuzi yoyote na uchaguzi utafanyika.

Majibu: Mawazo hayo yana-personalise hoja yangu. Lissu ameanzisha hoja. Mie nimejielekeza kwenye hoja na kumweka pembeni. Tujiepushe na tatizo hilo la ARGUMENTUM AD HOMINEM. Yaani tutofautishe hoja na mleta hoja. Tufikirie juu ya uwezekano kwamba hoja ni nzuri, serikali itaweza kuipenda, Bunge litaweza kuichagamkia. Let us think positively. Namna hiyo, tutakuwa na mchango ambao sio biased sana.

Pingamizi: Tukifanya mageuzi ya kimfumo kwa ajili ya kuondoa mabonde, milima, makorongo na miiba kwenye uwanja wa siasa, Wapinzani wa Chadema watapata fursa ya kukiangusha chama tawala cha CCM, wakati bila CCM nchi inaweza kuyumbishwa na Chadema kwa sababu ya ukabila wao.

Majibu: Tulipoanzisha mfumo wa vyama vingi tulikubaliana kwamba uchaguzi wa chama kimoja dhidi ya vyama baki ndio mtindo wa maisha yetu ya kisiasa. Hiyo maana yake ni kwamba tulikubali kwamba, kwa kuwa sauti ya wengi ni kama sauti ya Mungu, basi chama kitakachopata kura nyingi ndicho kinapaswa kuongoza nchi.

Chama hicho kinaweza kuwa Chadema au chama kingine. Na kuhusu tuhuma kwamba Chadema inaumwa ugonjwa wa ukabila wa kichaga, tuhuma hiyo sasa umepatiwa tiba.

Ujio wa Timu Lissu umekivua chama cha Chadema gamba la ukabila wa kichaga uliokuwa unaelezwa kwa njia ya maneno kwamba "CHADEMA maana yake ni Chagga Development Manifesto."

Nawasilisha.

View attachment 3243764
James Mbatia wa NCCR Mageuzi aliyepinduliwa na Joseph Selasini
Andiko nzuri sana...hongera mkuu.
 
Mwiko kusema ukweli katika bara la Afrika,maana watu hawaangalii nguvu ya hoja bali nani kaleta hoja.

Uko kwenye serikali kumujaa wachumia tumbo hivyo mageuzi ya kimfumo ni adui wa taifa kwa tafsiri Yao.
 
Hoja nzuri, utafiti mzuri, ila sio realistic!.

Uchaguzi is a process, kuna siku Uchaguzi mkuu uliwahi kusogezwa mbele kwassbabu ya kurekebisha jambo lolote?.

TAL anayo the capacity & capability yoyote kusema no reforms no election?.

Hana!.

There will be no reforms, na uchaguzi utafanyika!. TAL na Chadema has no capacity wala capability kuzuia uchaguzi usifanyike!.

Nashauri watu wenye uwezo wa kusaidia, tumsaidie TAL, tuisadie Chadema iachane na Utopian politics and come to face with the real polititcs, TAL wala Chadema hawawezi kuzuia uchaguzi mkuu.
P
Naam Kuna siku uchaguzi mkuu ulishawahi kusogezwa mbele, labda wakati huu wewe ulikuwa hauishi Tanzania, ulikiwa ile nchi uliyofanyia Fungate honeymoon.

Alipokufa DR Omary Ali Juma uchaguzi ulisogezwa mbele.
 
Nimekuja hapa kupongeza na kushukuru sana Mungu kwa kukuumba na kukupa uwezo mzuri sana lakini zaidi kukushukuru Dr. Mama Amon kwa kutumia vizuri uwezo wako na muda wako. Wewe ni mzalendo kweli kweli. Pamoja na kuipenda CCM naipenda Tanzania zaidi. Na andiko hili watalielewa zaidi wanaoipenda Tanzania na wanaoona kesho yenye mashaka tusipoutizama ukweli ulivyo na kulazimisha ukweli tunaoutaka. Anyway, Ubarikiwe,ujaliwe afya njema na wanaopaswa kutekeleza hili wajaliwe unyenyekevu na ujasiri wa kufanya haya.
 
Nitarejea 😃

Nimesoma andiko na kulielewa

Labda mleta Hoja utufafanulie " Mpiga Kura ni nani?

Je, Tanzania tunao Wapiga Kura Kwa maana Halisi ya Kupiga Kura?

Katika kunijibu unaweza kutumia mfano wa uchaguzi wa Chadema kuchagua Mwenyekiti kama akina Yeriko na Ntobi ndio sample ya Wapiga Kura wa Tanganyika specifically

Nimekaa pale 🐼

Kupiga kura ni kitendo cha aina gani na mpiga kura makini ni nani?

Ndugu, umekaa hapo bado?

Naona umeandika:

“Nimesoma andiko na kulielewa. Labda mleta hoja utufafanulie:
  1. Kupiga kura ni kitendo cha aina gani na mpiga kura ni nani?
  2. Je, Tanzania tunao Wapiga Kura kwa maana halisi ya kupiga kura?
Katika kunijibu unaweza kutumia mfano wa uchaguzi wa Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema, ambapo akina Yeriko na Ntobi ndio sample ya wapiga Kura (ambao ninaowafikiria).”

Majibu yangu:

Kulingana na “sample ya wapiga Kura” uliyoitaja, nahitimisha kwamba tatizo lako ni kuona kuwa watu waliodhaniwa watakuwa “rational” wameonekana wakifanya maamuzi ambayo ni “irrational,” kwa kuchukulia kwamba wapiga kura rational ni wale ambao maamuzi yao yalishinda.

Kwa hiyo, unaonekana kujiuliza: Tunatoa jawabu gani kwa kituko hiki?

Napendekeza kwamba jawabu ni ugonjwa wa akili uitwao “dogmatism” maana walisikika wakisema kwa ujasiri mkubwa habari ya MBOWE NI ALFA NA OMEGA.

Kwa mujibu wa Professor Saul Kripke (2011), kwenye Makala yake iitwayo “On Two Paradoxes of Knowledge,” kama ilivyochapishwa kwenye kitabu, Philosophical Troubles: Collected Papers, Vol I (Oxford: Oxford University Press), ugonjwa wa akili uitwao “dogmatism” ni tatizo sugu katika ulimwengu wa leo. Anasema:

“A paradox or contradiction is an argument whose elements, including explicit premises, implicit premises and conclusion, constitute an incoherent set, meaning that, they cannot be true simultaneously.

"Based on how contradictions are generated in a given set of claims, we can identify three types of contradictions, namely: explicit contradiction, formal contradictions and implicit contradictions.

"A set of assertions is explicitly contradictory if and only if at least one member of the set is the direct negation of at least one member of the same set. For example: "Africa has 54 countries including Tanzania"; 'therefore, Tanzania is in Africa'; and 'Tanzania is not in Africa'." The second and third statements are contradictory.

"A set of assertions is formally contradictory if and only if at least one member of the set is an indirect negation of at least one member of the same set, where an explicit contradiction can be derived from its members by using the rules of ordinary logical inference only. For example: "'All Tanzanians speak Kiswahili', 'Juma is a Tanzanian', 'Juma does not speak Kiswahili.'"

"A set of assertions is implicitly contradictory if and only if at least one member of the set is an indirect negation of at least one member of the same set, where an explicit contradiction or implicit contradiction can be derived from its members by using the rules of ordinary logical inference after adding some necessarily true propositions to it.

"For example:

(1) The God is Triune;
(2) Neither the Son nor the Holy Spirit is Triune;
(3) Thus, neirhwr the Son nor the Holy Spirit is God."

This set has neither explicit nor formal contradictions.

But, if the set is expanded by adding the following orthodoxy statement, a contradiction emerges:

“(4) Each of the Son and the Holy Spirit is God.” Now, the third and fourth claims are contradictory.

"Another example of a paradox is "the paradox of dogmatism," which is relevant here, and is explained next.

“Person A is dogmatic with respect to a proposition that P is true if and only if person A believes that proposition P is true, and, moreover, person A has resolved not to be influenced by any future evidence against the proposition that P is true. Formally stated, the paradox of dogmatism has the following structure:

“(1) At time T1 I know that proposition P is true.

(2) At time T1 I know that if evidence E is against proposition P, then evidence E is misleading.

(3) At time T1 I know that evidence E is against proposition P.

(4) Therefore, at time T1 I know that evidence E is misleading.

(5) At time T1 misleading evidence must be avoided.

(6) Thus, I must avoid evidence E at time T2, at time T3 and at any future time Tn.

“The fallacy in this sort of reasoning emerges once an explicit reference to time is analyzed. Specifically, the conclusion at No (6) does not follow from premises. Here is the reason:

"If I know at time T1 that proposition P is true, then I know at T1 that any evidence against proposition P is misleading. However, if at a later time T2 I acquire new evidence E against proposition P, I may well not have known at T1 that E is misleading. For, given my new body of total evidence accumulated between T1 and T2, I may be justified in believing that proposition P is true at T1 and that proposition P is false at T2, and vice versa.

“Thus, knowledge and justified belief may shrink, as well as grow, with the acquisition of new evidence. Despite our finite mind, deciding when we chose dogmatism and when we chose skepticism is what matters most for the modern mind in the third millennium where human knowledge is changing daily.”


Hivyo basi, sasa hebu tuone jinsi majibu ya kitendawili hiki yanavyohusika kwenye uchaguzi.

Kupiga kura ni uamuzi wenye pande mbili kama shilingi. Kuna upande wa “Ndiyo” na upande wa “Hapana.”

Yaani Kupiga kura ni uamuzi wa kusema “Ndiyo na Hapana” kwa mpigo.

Mfano, waliomchagua Lissu walimkataa Mbowe. Na waliomchagua Mbowe walimkataa Lissu. Kila aliyeamua alikuwa na sababu zake.

Baadhi, wakiwemo kina sie, tuliukataa “ukale” na kukumbatia “usasa,” baada ya kupima sababu za kuunga mkono ukale na kuzikataa, na hatimaye tukashinda.

Wengine, wakimwemo kina Yeriko na Ntobi, waliukataa “usasa” na kukumbatia “ukale,” bila kujali uzito sababu za kuunga mkono usasa, na hatimaye wakashindwa.

Kwa mujibu wa “kitendawili cha Kripkian dogmatism,” walioshindwa waliponzwa na tatizo la “unwarranted dogmatism.”

Waliamini kuwa Mbowe ni “Alfa na Omega” bila kuzingatia uzito wa Ushahidi mpya, maana walikwishazifunga akili zao. Kiakili hawakuwa tayari kwa mabadiliko.

Walihitaji “shock-therapy” ili kuuona ukweli mpya.

Yaliyotokea kwenye uchaguzi wa Chadema hutokea kwenye kila uchaguzi. Nasi wenye kukataa ugonjwa wa akili uitwao “dogmatism” tusichoke kuwakomboa wagonjwa hawa kwa kuwapa dozi stahiki.
 
Hoja nzuri, utafiti mzuri, ila sio realistic!.

Uchaguzi is a process, kuna siku Uchaguzi mkuu uliwahi kusogezwa mbele kwassbabu ya kurekebisha jambo lolote?.

TAL anayo the capacity & capability yoyote kusema no reforms no election?.

Hana!.

There will be no reforms, na uchaguzi utafanyika!. TAL na Chadema has no capacity wala capability kuzuia uchaguzi usifanyike!.

Nashauri watu wenye uwezo wa kusaidia, tumsaidie TAL, tuisadie Chadema iachane na Utopian politics and come to face with the real polititcs, TAL wala Chadema hawawezi kuzuia uchaguzi mkuu.
P
Mkuu, nakushauri usome Sir. Isaac Newton's second law of motion, ni lazima kitu kifanyike ili kuwe na mabadiliko ya aina yoyote, external force ni lazima.
Hoja nzuri, utafiti mzuri, ila sio realistic!.

Uchaguzi is a process, kuna siku Uchaguzi mkuu uliwahi kusogezwa mbele kwassbabu ya kurekebisha jambo lolote?.

TAL anayo the capacity & capability yoyote kusema no reforms no election?.

Hana!.

There will be no reforms, na uchaguzi utafanyika!. TAL na Chadema has no capacity wala capability kuzuia uchaguzi usifanyike!.

Nashauri watu wenye uwezo wa kusaidia, tumsaidie TAL, tuisadie Chadema iachane na Utopian politics and come to face with the real polititcs, TAL wala Chadema hawawezi kuzuia uchaguzi mkuu.
P
Mkuu, wewe ulifikia hitimisho kuwa TAL hawezi kushinda uenyekiti CDM, akashinda! Watu wengi wana underestimate uwezo wa TAL. Wanamwona yuko peke yake, sio hivyo.

Sujui kama ni Mungu au ni 'mfumo', ila kuna nguvu kubwa tena tukufu nyuma ya TAL. Mimi ningekuwa mwenyekiti wa CCM nisingeweza kupata usingizi.
 
Back
Top Bottom