Ngoja tuone ila nitakutag usikasirike tu.
Mawazo kama yako ni ya kusikitisha sana. Mnasubiria USA? Hata Ukraine siyo mazezeta hivyo ..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ngoja tuone ila nitakutag usikasirike tu.
Kiukweli kabisa CAG kazi yake kuwatangaza Vibaka.Si tulisha kubaliana Kibaka ni kibaka tu hata awe kwenye V8?
Ukraine bila msaada leo wangekuwa wamekimbilia PolandMawazo kama yako ni ya kusikitisha sana. Mnasubiria USA? Hata Ukraine siyo mazezeta hivyo ..
Nimeanza kumdharau Mwabukusi kwa matamshi yake. Kumbe alikuwa chadema akahama, akawa NCCR akahama, sasa anatafuta kick tu. Nimeanza kumdharau!
Ngoja tuone maandamano atapata watu wangapi........
View attachment 2769818Waacheni watu wa enjoy kahawa zao na kubishana YANGA SIMBA siku wakichoka watachukua hata silaha za jadi.
Generation mbili mbele.Ni ushauri wako kuwa tusubiri tu hata miaka 2,000 mingine?
Generation mbili mbele.
Nenda kwa Wagogo halafu useme unataka kuandamana dhidi ya Serikali ya CCM, uone kama atatoka mtu, hata kama Mgogo anaishi kwenye Nyumba ya Tembe na anashindia mlo wa Viwavi jeshi.Kwanini mbili si tatu, sasa au 80 mbele? Kigezo chako nini au ramli tu?
"Kama ni ramli hudhani labda tujikite kujadili ugaga wa kienyeji tu ndugu?" -- Mwigulu.
Nenda kwa Wagogo halafu useme unataka kuandamana dhidi ya Serikali ya CCM hatoki mtu hata kama Mgogo anaishi kwenye Nyumba ya Tembe na anashindia mlo wa Viwavi jeshi.
Si uhamie Kenya ndugu ambako unakutamani!! Tuache sisi hivihivi na uzoba wetuNimeishi na kusomea Kenya mindset ya Mtanzania iko tofauti sana na Mkenya mpaka huwa najiuliza Artificial Borders zinawezaje kubadilisha tabia za watu kiasi hicho Mkenya anajitambua zaidi na yuko active kwenye mambo yanayomhusu iwe kwenye kabila lake au jamii yake.
Mtanzania wa Kilimanjaro Arusha Manyara anaweza kufanana kidogo na Mkenya hata CCM wenyewe hupata tabu sana kwenye maeneo hayo.
Mkenya aneweza kuingia barabarani hata wakiwa watano.
Na nyinyi na Movement yenu ya Sauti ya Mtanzania+NCCR tunawatakia kila kheriIla ruzuku na ubunge mnavitaka kweli kweli. Yaani hamuoni wala hamsikii.
Ama kweli:
View attachment 2769833
Wito kujitathmini ni real ..
Na nyinyi na Movement yenu ya Sauti ya Mtanzania+NCCR tunawatakia kila kheri
Mimi niko hapa JAMBO TV Slaa yuko live.
Mimi ni CHADEMA na ninatii viongozi wangu na mara nyingi I speak my mind huwa sina herd mentality.Siko NCCR mkuu. Hivi vyama having mwenyewe. Tutabanana humu humu ila u chawa wa ki CCM wengine haituhusu ...
Tutasimama haki bila kujali inatokea CCM.
Kwa hapa Mwabukusi 💯%!
Habari ndiyo hiyo.
Hiyo ni point Mwakubusi ameongelea kwamba wanasiasa ni wabinafsi hadi wananchi hawana hamasa. Unadhani watu wanaingia barabarani sababu ya vyama?Kufa wakati huu kwa ajili ya maandamano ya Chama cha siasa Chenye lengo moja tu la KUSHIKA DOLA ni kuikosea NAFSI YAKO, FAMILIA YAKO NA JAMII KWA UJUMLA!!!!
Hakuna guarantee that CHADEMA will be better off kuliko hawa waliopo....
Tunayaona KENYA na kwingineko.....
Tupinge maovu lakini lazima tutambue CHARITY BEGINS AT HOME
Mbona anaendelea na harakati zake. Pia ana haki ya kukosoa. Chadema ni chama cha Umma na wananchi wana haki kukisoa kama vyama vingine.Kwanini huyo mwakubusi asiendelee na harakati zake kwani chadema wamemkataza kila mtu atumie mbinu anayojua yeye
Hili jambo la maandamano la kina Dr Slaa, Mwambukusi, Mdude Nyangali na wenzao linaonekana kwa haraka haraka kama lina sura na lengo jema sana - kushinikiza upatikanaji wa katiba mpya na kupinga mkataba wa bandari ambazo pia hizi ndizo ajenda kuu za CHADEMA...Mbowe, Lissu tunawapa pole za kupigwa risasi na kufilisiwa lakini hii struggle siyo ya watu binafsi sababu kuna watu wamekufa kabisa kwa ajili ya mapambano ya kuitoa CCM. Je hao utawambia nini familia zao? Viongozi wa sasa hawana mbinu, ari wala mikakati ya kiuhalisia wakuitoa CCM. Wakina Mwakubusi wanajaribu kuratibu maandamano na civil disobedience na hiyo ndio lugha CCM wanaelewa na kuogopa. Hivi nyie mnawezaje kuwa waastarabu kwa watu wanaoiba kura mchana kweupe huko Zanzibar na mkaamini watabadilika na kuwa waastarabu? Eti unaongelea vyuo vya Uongozi, Diplomacy una akili kweli wewe? Unapambana na mhuni wa Mbagala kwa technique za Oysterbay.
Salaam wana jukwaa, nimekutana na interview ya Wakili Mwabukusi na Maria Sarungi probably kutoka Maria spaces/clubhouse. Cha kushangaza Wakili msomi alikua busy kushambulia wapinzani kuwa ni wawaza ubunge, wapenda vyeo n.k. Hivi kweli hajui struggle za lissu hadi kumwagiwa risasi, hajui mbowe alivyofilisiwa na kufungwa kisa kudai katiba mpya na democracia nchi hii?
Pia kalaumu wapinzani kutosupport maandamano yake akiwaita waoga? Hivi siasa za maandamano wapinzani hawajui? Amesahau maandamano ya Arusha 2011 hadi watu wakauwawa? Amesahau maandamano ya pale Kinondoni hadi kina Mbowe wakahukumiwa kifungo na faini ya 300 Million? Yeye Leo ndio anajifanya ni pro-protest kuliko kina Hajji Duni au lissu?
Sio hivyo tu kaongelea suala la wake za viongozi kulipwa posho!! Yes ni kitu cha ajabu lakini Mwabukusi amekiadress kana kwamba tunalipia tendo la ndoa la viongozi yaani "we are paying for that thing.... we are paying for sex". As if wake za viongozi ni vyombo vya ngono tu. Kauli za namna hii ni unnecessary maana badala ya hoja kuwa bandari utaanza kujibu makelele ya feminists na UWT!!
Ushauri naoweza kumpa Mwabukusi ni kwamba atafute PR manager ajue namna ya kujenga mahusiano na umma. Ana hoja nzuri ya Bandari pamoja na katiba mpya ila lazima ajifunze kuwa na shabaha moja kwa wakati. Ni hatari sana kupambana na CCM, CHADEMA na wanawake kwa wakati mmoja utaondoka kwenye limelight in no time....
Kingine kuna haja ya vyama kama CHADEMA au ACT kupitia TCD kuanzisha chuo cha uongozi, diplomacy na political science ili wanasiasa/wanaharakati wote vijana wapitie huko kabla ya kupewa teuzi/uongozi hasa kwenye vyombo vya uwakilishi au kuongoza taasisi/jumuiya ya vyama.
Hili litasaidia kuondoa mihemko, kuleta utulivu wa akili kwenye mijadala, na kuwa na mawasiliano mazuri na jamii. Sasa mtu kawa maarufu juzi tu kaanza kumshambulia Mbowe out of nowhere! haya mambo hayapendezi especially tuliopo opposition maana tukikwaa madaraka si yatajirudia ya sabaya na Makonda!
View: https://youtu.be/78Gi9mXZWwA?si=YMXW0PFJ-jpAesu9
Stop overthinking. Strategy ya Chadema kwasasa ni mbovu mno, wataishia kuwa kama Sharif. CCM na TISS wapo tayari kuua na kutumia nguvu kubaki madarakani. Uniamini watu wa namna hiyo wataondoka kwa maridhiano na kura? Msipoanzisha maandamano na civil disobedience CCM haitatoka.Hili jambo la maandamano la kina Dr Slaa, Mwambukusi, Mdude Nyangali na wenzao linaonekana kwa haraka haraka kama lina sura na lengo jema sana - kushinikiza upatikanaji wa katiba mpya na kupinga mkataba wa bandari ambazo pia hizi ndizo ajenda kuu za CHADEMA...
Lakini ukweli ni kuwa, ukifikiri na kuliangalia Kwa jicho la pili la ndani, moja Kwa moja utagundua kuwa huu ni mtego wa CHADEMA ambao umesukwa ndani ya TISS kuinasa CHADEMA na kuipeleka mahali TISS na wapinzani wao wakuu CCM wanataka iwe - kuifutia usajili..
Binafsi nimemwelewa vizuri sana mwamba Freeman Mbowe vizuri leo. Na nawasifu sana CHADEMA kuwa wana akili sana kuukwepa mtego huu. Na operesheni zao zinazoendelea kupita Jimbo Kwa Jimbo, mkoa kwa mkoa na wilaya kwa wilaya na kwenye kata na vijiji vyote ni more effective than tukio la siku moja...
USHAURI WANGU NI;
Dr Slaa, Mwambukusi, Mdude Nyangali na Sauti ya Tanzania wafanye Kwa kadiri wanavyoona inafaa. Tukiona yanaendelea na wamekomaa kwelikweli, wataungana nao huko mbeleni
By the way, Mimi najiuliza;
1. Hawa Sauti za wananchi/Watanzania ni kina nani? Wamesajiliwa kisheria? Malengo yao ni nini
2. Waliwahi kukutana na CHADEMA - chama cha siasa registered chenye programs na mipango yake ya muda mfupi na mrefu wakajadili namna wanavyoweza kuwashirikisha kwenye mpango wao huo?
## Ni kweli huwezi kukaa huko ukapanga mambo yako na kisha out of nowhere ukawaita watu wasiojua hili wala lile juu ya shughuli yako ili waje kushiriki tu..!
## Hata sherehe ya harusi hutumia muda mrefu na WA kutosha kuandaliwa kwa kusambaza kadi za kuomba michango na baadaye kuwaalika watu kwenye sherehe yenyewe..
## CHADEMA wana akili sana kuepuka mtego huu..