Ushauri kwa Wakili Mwabukusi kuelekea maandamano ya kitaifa

Tuwe makini sana na fitina za Slaa imekuwaje ghafla Mwabukusi amekuwa na Bifu na CHADEMA yule Babu sio...
 
Mimi kama Mwanachama wa CHADEMA nitasikiliza viongozi wangu wa Chama na msimamo wa Chama bado na hapo hapo ninaweza kutoa ushauri wangu kuwa tusiwe Chama cha Matukio tujikite kwenye Manifesto yetu.

Kwamba mambo yanakwenda kombo:

"Umeme hamna, mafuta bei kama hivyo, ajira hakuna, wizi wa kura kama kazi, katiba subirini kozi ya miaka 3, kodi lipeni na nyongeza za tozo juu, bambikiziweni kesi, uliweni, nk nk ushauri Kwa chama chako: tujikite kwenye manifesto."

Hii ndugu itakuwa akili au matope?
 
Ni mada uliyotumia muda vizuri.

Kuna mambo mazuri uliyoongelea, na kuna mengine huko mbali sana na hisia kama zinazomsukuma Wakili kuziwasilisha kama anavyofanya.
Wakili hayupo mbali sana na ukweli, anaposema hayo juu ya vyama vya upinzani, pamoja na kwamba umetoamifano ya akina Mbowe na wengine walivyo dhurika juu ya misimamo yao. Hiyo haiwezi kuondoa sura nyingine inayojitokeza kwa viongozi hao wanapoonekana kugeuka nyuma na kuwa kama zigo la chumvi.
Inaeleweka sana kwa mtu kama wewe kuleta mada hii hapa, kwani ni sampuli nzuri sana ya watu wanaogeuka sura kila mara hali inaporuhusu kuonyesha uhalisia wao ulipo.

Ninakubaliana nawe kuhusu 'moderation' anayotakiwa kuwa nayo Wakili katika kuwasilisha mambo.

Naomba niseme, sijachambua kiundani hoja zako ulizowasilisha humo moja baada ya nyingine. Huu ni muono wangu tu wa jumlajumla baada ya kupitia andiko haraka.
 
Siku Wananchi wakichoka hakuna cha Mwabukusi wala Slaa wenyewe wataingia Mabarabarani so far wako bize na YANGA SIMBA mchana usiku VIGODORO.


Hebu tazama maandamano ya YANGA
 
Dunia hiyo haioni huko Cameroon, Rwanda, Uganda, Russia, Ivory coast, n.k. Macho ya dunia yanaona Tanzania tu??
Kizazi hiki Cha maovu hakitogharikishwa Kwa mvua ,moto au upepo ila viongozi madhalimu ndio itakuwa adhabu Yao.
Badala ya maandamano labda National Istighfar day.
 
Kufa wakati huu kwa ajili ya maandamano ya Chama cha siasa Chenye lengo moja tu la KUSHIKA DOLA ni kuikosea NAFSI YAKO, FAMILIA YAKO NA JAMII KWA UJUMLA!!!!

Hakuna guarantee that CHADEMA will be better off kuliko hawa waliopo....

Tunayaona KENYA na kwingineko.....

Tupinge maovu lakini lazima tutambue CHARITY BEGINS AT HOME
 
Dunia hiyo haioni huko Cameroon, Rwanda, Uganda, Russia, Ivory coast, n.k. Macho ya dunia yanaona Tanzania tu??
Wanajua kuwa Tanzania ikiingia kwenye Vita vya sisi kwa sisi hao wanyama pori waliojaa Serengeti Selou na Burigi wote watachomwa mishikaki.
 
Siku Wananchi wakichoka hakuna cha Mwabukusi wala Slaa wenyewe wataingia Mabarabarani so far wako bize na YANGA SIMBA mchana usiku VIGODORO.


Hebu tazama maandamano ya YANGA
View attachment 2769566

Lissu hasubiri miaka 1000 wananchi watakapochoka. Kuchoka wananchi hakutoki kwa mungu ndugu. Kulikoni kutaka kuvuna mahali bila Kupanda?

Kwani Kenya maandamano Yale ni spontaneous? Mbona leo au Jana hayapo? Kama wako ndiyo msimamo wa chadema huo umekaa kufukuzia ruzuku tu hauna lolote.

Msimamo kama huo lazima kuungwa mkono na ma CCM na WA aina ya kina johnthebaptist
 
Chadema na Ruzuku ni kama Wali na Maharage
 
Kwani Kenya maandamano Yale ni spontaneous? Mbona leo au Jana hayapo? Kama wako ndiyo msimamo wa chadema huo umekaa kufukuzia ruzuku tu hauna lolote.
Nimeishi na kusomea Kenya mindset ya Mtanzania iko tofauti sana na Mkenya mpaka huwa najiuliza Artificial Borders zinawezaje kubadilisha tabia za watu kiasi hicho Mkenya anajitambua zaidi na yuko active kwenye mambo yanayomhusu iwe kwenye kabila lake au jamii yake.

Mtanzania wa Kilimanjaro Arusha Manyara anaweza kufanana kidogo na Mkenya hata CCM wenyewe hupata tabu sana kwenye maeneo hayo.

Mkenya aneweza kuingia barabarani hata wakiwa watano.
 
Wanajua kuwa Tanzania ikiingia kwenye Vita vya sisi kwa sisi hao wanyama pori waliojaa Serengeti Selou na Burigi wote watachomwa mishikaki.
Unataka kusema dunia Ina uchungu sana na rasilimali zilizopo Tanzania kuliko zilizopo DRC na kwingineko??
 
Kwa hiyo sababu watu wanakufa hivyo wasiandamane ?

Una miaka mingapi dogo ?
 
Huyo Mzee huenda katumwa na CCM kwa sababu aliwahi kusema kwamba hajarudisha kadi ya uanachama wa CCM.

Hatuwezi kufanya siasa kwa hisia. Ndiyo maana CCM wanatutaka tuwe hivyo. Kama yeye anaweza kuwa katumwa kwanini usiwe na wewe pia hapo ulipo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…