Ushauri kwa walio Chuo Kikuu na vyuo vya kati GPA matters

Kwa Upande Wangu Kipindi Kile kulikuwa na Advantage zaidi ya Wakati huu,

Advantage ya Kipindi Kile Cha kikwete, ajira ilikuwa ni Uhakika Mkubwa Sana ukilinganisha na Wakati huu,

Wakati Ule waalimu wanafanya interview wanapita wote, Unaenda kwenye interview ukiwa na kujiamini kwakuwa uwezekano wa kupata Kazi ni mkubwa,

Saizi Hali sio Kama Ile ya zamani.
 
Walimu wa kiswahili wanahitajika 90+ walioitwa ni 24,000 na ushee aloooh
 
Sema huwa najiuliza sana hivi haya mashirika ya watu binafsi yapo vipi.

Kuna sehemu nilienda an kila naemgusa ni form 4 anasema alipofika alifanya practical test basi.. mpaka leo yupo na kati ya kumi wawili tu ndo wansema wametokea chuo
Hapa sijajua umeongelea mashirika binafsi ya International au local?
Kama ni local hapo ni ukabila pamoja na ushemeji unatumika na kama ni International wanaangalia uwezo wako binafsi(reasoning capability) na general understanding ukiachilia mbali na makaratasi.
Mtu anaweza akawa na GPA ya 4.5 lakini akiitwa kwenye interview hajui hata kujieleza nilishawahi kusoma na watu wa aina hii ila walichelewa sana kupata kazi na hata kazi walizopata ni zile za ili mradi kazi zenye mishahara midogo na mazingira mabovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…