Kimsingi kabisa bro nakuunga mkono, Mwanamke anatakiwa kulea Watoto katika malezi mazuri pamoja na usaidizi wa mwanaume, lakini mama akae maskani awalee Watoto alinde Mali za mumewe,na mtafutaji ni Baba. Yeye ndo ambaye ana jukumu la kuhakikisha familia yake inapata Kila mahitaji ya Muhimu. Haya mambo ya mwanamke Asubuhi na Mwanaume Asubuhi wote kazini huu uongo
suala hili ni pana zaidi katika kujadili matokeo ya kuoa mwanamke mwenye ajira na asie na ajira ktk upande wa faida na hasara
faida zake (kwa mwenye ajira)
1.endapo ukakwama na mkawa mnaelewana ndani ya nyumba anaweza kusaidia kwa kipindi umekwama kuziba nafasi japo kwa uchache
2.ukifa ana take responsible sahihi kwa watoto
3.shida hupungua ktk familia kipesa
4.mtakula maisha (kama mpo bond)
hasara zake (kwa mwenye ajira)
1.ukikosea kidogo tu anaanza dharau ni kwasababu anajua hakutegemei moja kwa moja
2.mara nyingi chako chake, ila chake ni cha kwake tu
3.watoto hukosa malezi ya mama hatimae huishia kupelekwa boarding schools
4.mapenzi hupungua kwa sababu kila mtu anakuwa bize mchana mkirudi nyumbani wote mmechoka
5.chance ya kucheat na mahouse girl au maofisini huwa kubwa sana
6.heshima ya mwanaume hupungua kwa sababu uwepo wake hauna nguvu ya moja kwa moja kwa familia
7.ndoa huweza kuvunjika muda wowote kwa kuwa wote ndani wanaweza kujiona wanaume na kitu ambacho mwanaume hakipendi ni dharau au kukosewa heshima
8.watoto hukosa maadili
kwa hivyo kimsingi kuoa mwanamke mwenye ajira kuna faida chache sana kuliko hasara
hasara ni nyingi ila all in all mwanaume uchague kuitekekeza ndoa yako ama kuijenga for future hilo lipo mikononi mwako ila cha mwisho wakuu na cha kuzingatia mwanaume inapaswa kutumia sana akili kufanya maamuzi katika kuliendea suala zima la ndoa kuliko kutumia mihemko na hisia za mapenzi (moyo huponza kicbwa)