Time dilation ipo kote kote, mafhumu ya time fdilation ni kutofautiana kwa muda ndani ya sehemu moja au sehemu mbili tofauti kutokana na tofauti ya mwendo au mvutano. Haya ni mapito ya watu wa Fizikia.
Hii tafsiri ya kuwa ni kutofautiana kwa muda ndani ya sehemu moja ama sehemu mbili tofauti ndio niliuliza huko juu kuwa watu wa pangoni huo muda ulitofautiana baina ya wapi na wapi mkuu ?
Allah mwenyewe kasema kuwa wale hawakulala sehemu ya siku kama walivyodhani,bali ni hakika kuwa walilala idadi ya miaka ile ile ambayo watu wengine wasiokuwa wao walihesabu hivyo.
Utofauti wa muda katika tukio la watu wa pangoni ni baina ya wapi na wapi ndugu ?
Kwahiyo tukio la watu wa pangoni hakuna kusimama kwa muda,muda upo kama kawaida ila umetofautiana kutokana na sababu fulani.
Hizo sababu ni zipi kwa mujibu wa ushahidi wa kisa kile wakati ambapo Allah anathibitisha kuwa wale walilala pale miaka mingi mfano wa miaka ile ile iliyopita kwa wasiokuwa wao ?
Allah aliwaziba masikio na akawalaza humo pangoni kwa miaka kadha wa kadha kisha wewe unasema kulikuwa na tofauti ya muda,hiyo tofauti ilikuwa wapi ?
Allah kataja sababu kuwa wale walizibwa masikio na kulazwa pale miaka na miaka ndio maana wakaona wamelala kidogo.
Watu wa pangoni vivyo hivyo, walipigwa usingizi kwa miaka hiyo aliyoitaja Allah katika Qur'aan, lakini wao wakaona kama wametoka kuamka tu, yaani kama sehemu ya siku lakini kumbe muda ulikuwa ni miaka 309.
Huu muda wa miaka 309 haukuwa tofauti na miaka ya nje ya pango,kwa maana muda ulienda sawa kabisa baina ya pangoni na kusikokuwa pangoni.
Sasa huo utofauti wa muda unaousema sijaelewa ulikuwa wapi ?
Unatakiwa uongeze umakini ukiwa unasoma ninacho kiandika. Nimetoa mifano miwili ya Time Dilation, lakini naona umehitimisha kwa kauli ya uongo kwamba nimehusisha sehemu mbili tofauti. Huku nikukosa kwako umakini. Ule ushauri nilio kupa ufanyie kazi utakusaidia sana. Sas
Pengine wewe ukaona umeeleweka ulichokusudia,lakini waliopokea ujumbe wameelewa tofauti.
Ikitokea hivyo usiwe na kejeli na dharau kwa wengine.
Unaposema nimehitimisha kwa kauli ya uongo ya kuwa wewe umehusisha sehemu mbili tofauti kwani hii ya wewe kuhusisha sehemu mbili tofauti hukuisema ?
Umesema mwenyewe kuwa umetoa mifano miwili na mmoja wao ni huo wa kuwa inaweza kuwa ya sehemu mbili tofauti kama ulivyosema siku moja ni sawa na masiku mengi kwa Allah,hii ulikusudia ni sehemu mbili tofauti.
Sasa mimi kusema kuwa umgusia sehemu mbili tofauti,unaniambia muongo ilhali haya maneno umeyasema wewe mwenywwe.
Labda useme nimekunukuu kwa kauli moja ambayo ni kweli umeisema na ilhali ulikuwa umeweka kauli mbili.
Kusema kuwa ni uongo wakati kauli umeisemamwenyewe nashida kutia neno lolote.
Sasa kijana inakuwaje unahitimisha kwa vitu ambavyo havipo, nikikuuliza unionyeshe wapi nimesema Time dilation inahusisha sehemu mbili tofauti pekee utanionyesha
Mifano yako iliashiria hivyo kuwa time dilation inahusisha sehemu mbili tofauti.ndio maana ulinukuu mfano wa siku moja kwa Allah na siku moja ya duniani utofauti wao.
Sasa mifano uliyotoa inaonesha utofauti wa muda baina ya sehemu mbili.
Watu wa pangoni bado tupo kwenye kueleweshana kama pale palikuwa na tofauti ya muda baina ya sehemumoja(duniani)
Kwa hiyo mifano uliyotoa inaonesha tofauti ya muda baina ya sehemu mbili,watu wa pangoni bado hatujaafikiana kama ilikuwa ni tofauti ya muda baina ya sehemu moja.
Wakati nimetoa mifano miwili tofauti na yote inaonyesha Time Dilation ? Ongeza umakino ili usiwe unapoteza muda kuhoji vitu vya kijinga kwa kutokuwa makini.
Wapi tumekubaliana kuwa kuwa hiyo mifano yote kuwa ni time dilation ?
Unasahau kuwa hapa ndo tunajadili kwamba je mifano yako uliyotoa ni time dilation kweli hasa lile la watu wa pangoni ?
Sasa kutoa kwako mifano ukainasibisha na time dilation unataka na mimi nikubali moja kwa moja kuwa ni kweli time dilation bila kuhoji.
Yani unarudi kule kule kwamba mawazo yako unataka tuyakubali tu moja kwa moja jambo ambalo sio sahihi kabisa.hatujakubaliana katika mifano yako yote kuwa hiyo ni time dilation.
Sasa nani anasema tukio lile muda haukuenda katika utaratibu. Naona pale mwanzo ulikurupuka kwa kufasiri neno kwa mjengeko wake ukahusisha "Dilation" na "Delay".Hivi vitu viwili tofauti. Fanyia kazi ushauri wangu.
Okey sawa Mungu akubariki.
Umeona sasa unavyo jiumbua ? Huko juu umetoa hitimisho kwa mfano mmoja nilio utoa, lakini hapa uajumuisha mifano yote miwili, sasa huoni unavyojichanganya ?
Mfano mwingine tunasoma katika Qur'aan ya kuwa siku moja kwa Allah kwatu sisi ni miaka elfu moja.
Nilichokubaliana na wewe ni mfano wako wa time dilation kuwa ni muda na sehemu mbili tofauti.
Na hatujakubaliana kuwa time dilation kama inaweza kutokea baina ya sehemu moja.
Sasa sijichanganyi kwa sababu bado sijakubaliana na wewe kuwa aswhabu al kahfi ilikuwa time dilation.
Nimeshangaa kuwa vipi watu wa pangoni uwatie katika time dilation wakati mifano uliyotoa inahusisha sehemu mbili tofauti na watu wa pangoni ilohusisha sehemu moja.
Hapa kazi yako iwe ni kunifahamisha mimi kuwa watu wa pangoni ililkuwa kweli ni time dilation .
Ikiwa utanifafanulia juu ya hili ndipo una haki ya kusema kuwa NILIJICHANGANYA.
Ngoja nikusaidie, kwani Time Dilation ni nini ? Jifunze kuhoji
Mimi hapa nahoji kwa mujibu wa maana ulizozitoa wewe.
Wewe umeeleza kuwa time dilation ni utofauti wa muda baina ya sehemu moja ama mbili na ukatoa mifano.
Nahoji kutokea katika maana yako hiyo ambayo mwanzo KIUKWELI SIKUIPATA KUTOKA KWAKO.