Wasalaa wana jamvi.
Kwanza nichukue fursa hii kumpongeza sana Mh Makonda kwakuwa mbunifu na kutafuta kila njia kutatua kero za wananchi wako wa jiji la Dares-salaam kwani umekuwa ukifanikiwa sana na kila mwenye macho hujionea mwenyewe.
Kumeibuka tabia kubwa sana hasa kwa wabunge wawili hasa Mlinga na Msukuma kumvizia Mh Makonda kukokosoa kila jambo na huwa hawana wanalo liona jema kwa kila kinachofanywa na Mh Makonda...
Kwanza lazima watu wajue hakuna anayekataa Makonda kukosolewa lakini tulitarajia ukosoaji uwe wa kuboresha na kujenga na sio kukatisha tamaa kwa kila kinacho fanywa na Makonda....kana kwamba huwa hawaoni jema.
Lakini kinacho shangaza kwa wabunge wetu wao husubiri wenzao waanzishe jambo na wao wakosoe tuu huwa najiuliza siku zote wanakuwa wapi? Hivi kwanini tunasubiri watu waanzishe jambo ndio tuone makosa?
Mh Makonda usiache kuwapa dawa wanapo ingia anga zako kama wao kazi zimewashinda acha waache wewe ufanye na kama wanaona kuna makosa wanajua jinsi na utaratibu mzuri wa kurekebisha au wao waanzishe vya kwao kwa njia nzuri.
Hongera sana Makonda.