Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Acha kumfagilia mtu anaepondwa na kila mtu, hivi unadhani wabunge na watu wote hawana akili? Unasapoti ushetani, sisi waafrika mtoto yeyote ni mtoto wako, au hujamskia palamagamba? Huku kwetu mwanaume ambae hawezi kuzaa huwa anapewa safari nyingi ili asaidiwe kuzaa... Umeinyaka hiyo!? Sio mnakaa na kutaka kupakazia watu watoto! Mi simuungi mkono.... Nauliza Tr 1.5 zimeshapatiwa maelezo ni wapi zimetumika!?
 
Kweli kabisa, tatizo nchini kwetu ukifanya kazi kwa bidii na ku show initiative lazima upate maadui tu..
Hii nchi uhusiano kati ya mtu anayefanya kazi kwa bidii na maarifa ni paka na panya. Wewe ukitaka Watanzania walio wengi wa kuthtamini na wa kuheshimu wewe kuwa kibaka tu watakushangilia sana na kukupa heshima yote.
 
Kuna msemo watu huongea "sheria haina macho" hii ina maana huwezi kufanya jambo kinyume hata kama lina msaada kwa mhanga sheria ikatambua jambo lile linafanywa kwa nia njema. Kifupi nia njema haipo mbele ya sheria. Mfano inaweza kutokea mtu akaenda mahakamani kuomba tafsiri ya kinachofanywa na Bashite na mahakama ikatoa zuio. Maana yangu hapa kinachofanyika si kibaya ila taratibu zinakiukwa sababu kuna sheria inayosimamia faragha kwa mama na mtoto jiulizeni huko mlipo kwa nini kesi za udhalilishaji na ubakaji wa mama na watoto zinasikilizwa ndani ya chumba cha mahakama na si eneo la wazi kama inavyozoeleka? ukipata jibu utarejea anachofanya bashite
Nyie waswahili nyie hamna mnachojua zaid ya kubishia tu. Makonda anawasaidia wanyonge, akina mama waliotelekezwa na waume zao pamoja na serikali. Makonda amejitoa mhanga kuwasaidia free of charge. Ukiangalia majority wamepata msaada. Asilimia kubwa sana. Wengine wamekumbushwa tu majukumu yao kama wazazi na wameitika.
Kama ww unadhan ni kinyume na sheria peleka mahakaman, omba mahakama ibatilishe hilo zoez. Ndan ya siku kumi tu makonda atakuwa ameokoa mamia kama sio maelfu ya watoto ambao wangekufa kwa utapia mlo au kukosa matunzo au wangeingia mtaan kuwa ombaomba au watoto wa mtaan ambao baadae wangekuja kuwa vibaka.
Kazi kubwa hiyo inafanyika kwa siku kumi tu.

Nawaza kuwa kama kila mkuu wa wilaya angetenga siku kumi tu kwa mwaka, tatizo la watoto wa mitaan lingepungua kwa asilimia 90%.

Halafu wapuuz, wajinga, washamba wanakuja kupiga kelele et amevunja sheria. Hata Yesu alivunja sheria alipookoa uhai siku ya sabato lakin lilikuwa jambo jema la kukumbukwa vizazi na vizazi.

Wabunge pamoja na haiba yao wanaacha kujadili budget et wanaanza kumtukana Makonda. Upuunzi tu. Yeye anawasaidia masikin wasio kuwa na mbele wala nyuma. Wewe piga kelele kama ilivo kawaida ya mswahili lakin masikin anapata msaada kutoka kwa watu wenye maono..
 
Hii nchi uhusiano kati ya mtu anayefanya kazi kwa bidii na maarifa ni paka na panya. Wewe ukitaka Watanzania walio wengi wa kuthtamini na wa kuheshimu wewe kuwa kibaka tu watakushangilia sana na kukupa heshima yote.
Ni kweli, sisi tunajulikana, tumeshuhudia wawekezaji wakigoma kutuajiri sababu ya kutokufanya kazi kwa bidii au kuiba kila wakati kwenye idara zao, kabla ya Magu, watu walikuwa wanaingia ofisi saa nne asubuhi, lunch wanaenda saa sita, wanarudi saa tisa na kuondoka, au wakienda lunch wanapotelea huko huko, wizi wa kila aina, tunamatatizo, ila wepesi wa kulalamika ajabu..Mwenzetu akifanya kazi yake eti anajipendekeza?! Tunamchukia na kumuanzishia timbwili kama vile kauwa!
Wabongo wanavuna wanachopanda, umaskini kuisha tusahau....
Sheria na tararibu zipo, hata kwenye utapeli wa viwanja na majumba zilikuwepo, hizi za kina baba kuhusika na matunzo ya watoto zipo..
Je zimewasaidia hawa raia kwa kiasi gani?!
Acheni apige kazi, na hata hivyo mbona ustawi na wanasheria wanahusika?!
 
Jamani tusidanganyane bashite kachemshaaaaaaa
Kachemka? Diaspora wameruka na ndege kuja kumalizana na waliowatelekeza wakiogopa kupelekwa kwa Makonda wakiogopa kufutiwa Visa nchi waliko wewe unasema Kachemka? Ndege zimeshusha diaspora kibao wamewanunulia majumba waliowatelekeza na kutoa hela Za matunzo wakati kabla ya zoezi walikuwa hawajali
 
Makonda Ni Zawadi toka Kwa Mwenyezimungu
Mungu gani tena huyo? Kwani naye huyu si mungu Wa dar? Kweli zero kitu kibaya sana msitutoe kwenye hoja za maana si tunataka kuelewesha hela zetu 1.5T zipo wapi huo utoto wenu pelekeni huko. Akimaliza kampeni hiyo awaite wanawake wote wanaoshindwa kupewa mimba na waume zao nao awape msaada wa kisheria.
 
Ni kweli, sisi tunajulikana, tumeshuhudia wawekezaji wakigoma kutuajiri sababu ya kutokufanya kazi kwa bidii au kuiba kila wakati kwenye idara zao, kabla ya Magu, watu walikuwa wanaingia ofisi saa nne asubuhi, lunch wanaenda saa sita, wanarudi saa tisa na kuondoka, au wakienda lunch wanapotelea huko huko, wizi wa kila aina, tunamatatizo, ila wepesi wa kulalamika ajabu..Mwenzitu akifanya kazi yake eti anajipendekeza?! Tunamchukia na kumuanzishia timbwili kama vile kauwa!
Wabongo wanavuna wanachopanda, umaskini kuisha tusahau.
Ukifanya kazi kwa bidii utasikia unafanya kazi kwa bidii kwani kazi ya baba yako hiyo...yaani hakuna nchi ya watu wa hovyo kama hii...duniani hapa
 
Hivi wale panya wa barabarani mkoani kwake ameshawamaliza au bado wanasumbua watu?
 
Mungu gani tena huyo? Kwani naye huyu si mungu Wa dar? Kweli zero kitu kibaya sana msitutoe kwenye hoja za maana si tunataka kuelewesha hela zetu 1.5T zipo wapi huo utoto wenu pelekeni huko. Akimaliza kampeni hiyo awaite wanawake wote wanaoshindwa kupewa mimba na waume zao nao awape msaada wa kisheria.
Taifa linajadili Mafuriko na athari zake hayo mambo ya Miaka ya Nyuma Sio wakati wake huu!
 
Taifa linajadili Mafuriko na athari zake hayo mambo ya Miaka ya Nyuma Sio wakati wake huu!
Hivi ww unajitambua kweli? Au huko kula kwa shemeji kumekuto ufahamu kabisa? Hayo mafuriko unayojadili hiyo miundo mbinu utaboresha vipi kama 1.5T hazieleweki zipo wapi? Fikiri nje ya box kuna siku utatoka hapo kwa shemeji na kuanza kudaiwa kodi utakuja kuona umuhimu wa hizi 1.5
 
Nchi yetu imeharibika kabisa ,kila likianzishwa Jambo Kuna watu wanajitokeza kulalamika kwamba huo sio utaratibu , Sasa wao wanaojua utaratibu mbona hawafanyi ??

Kuna faida gani mtu anajua taratibu zote lakini hamna anachofanya ??

Kama unajua taratibu zote si ufanye Sasa ?

Hao wabunge wanaomkosoa Makonda nao ni viongozi je wanafanya nini kupunguza watoto wa mitaani majimboni mwao?

Au kushangaa shangaa na kuwapa Mia Mia wale watoto mabarabarani ndiyo solution?

Hata swala la madawa ya kulevya walilalamika hivihivi lakini mwisho wa siku Makonda akaibuka kidedea baada ya madawa kupungua mtaani na mateja kuanza kulilia dawa za alosto.

Kampeni ya Makonda imegeuzwa kuwa kampeni ya kupima DNA na kulazimisha ndoa wakati siyo kweli.

Kama kwenye eneo unalotoka Kuna mama amekimbiwa na kuachiwa watoto awalee ndio utaelewa Makonda anamanisha nini.

Piga kazi Makonda na Mungu akubariki Sana ipo siku watakukumbuka tu ,hata Lowasa walimponda Sana na kumtukana lakini Leo ndio boss wao.
Hizi akili angalau zingekuwepo enzi za zinjathropus mabadiliko yasingetokea!
 
Ni kweli kabisa kinachompa Makonda credits kwenye initiatives zake ni laxity ya vyombo vya serikali kushughulikia kero za wananchi. Sote tunafahamu kitengocha ustawi wa jamii ilivyo na uzembe, corrupt, na walivyo outdated
Kama Makonda anapata credits basi zinatoka kwa watu wenye ubongo finyu usioweza kuchambua mambo. Kimsingi hakuna cha maana alichofanya na zaidi amepoteza muda ambao angeweza kufanya kazi zake zinazomhusu. Ameshafukuzana na mambo mengi lakini hakuna hat moja tunaloweza kusema amefanikiwa. Na hafanikiwa kwa sababu mambo anayojaribu kujiingiza yanahita mfumo maalum na wenye wataalam na zana kufanya. Anashika hili anaacha anakimbilia lile anaacha. Hebu sema madawa ya kulevya aliyojifanya kufanya vita ni nani alipatikana na hatia katika wale wote aliowataja. Anapoteza muda wakati kazi zake za msingi zimemshinda. Kwa mfano hali ya usalama jiji la Dar ni mbaya sana. Angeweza kukaa na wadau wa mkoa i.e. wakazi, polisi etc na kubuni mfumo endelevu wa kuhakikisha hali ya usalama ni nzuri.
 
Hivi ww unajitambua kweli? Au huko kula kwa shemeji kumekuto ufahamu kabisa? Hayo mafuriko unayojadili hiyo miundo mbinu utaboresha vipi kama 1.5T hazieleweki zipo wapi? Fikiri nje ya box kuna siku utatoka hapo kwa shemeji na kuanza kudaiwa kodi utakuja kuona umuhimu wa hizi 1.5

Kujitambua maana yake Mie Na Wewe kafanana Mawazo?

Kuna Mambo Mengi ya Kufanya

Acha kwanza Taifa limalize Sherehe ya Ally Kiba then mengine tutajadili

Kama kujadili ndio suluhu tushajadili sana EPA, Richmond, Escrow n.k

Acha Watu wameze Mate Kwa mambo mengine
 
Nchi yetu imeharibika kabisa ,kila likianzishwa Jambo Kuna watu wanajitokeza kulalamika kwamba huo sio utaratibu , Sasa wao wanaojua utaratibu mbona hawafanyi ??

Kuna faida gani mtu anajua taratibu zote lakini hamna anachofanya ??

Kama unajua taratibu zote si ufanye Sasa ?

Hao wabunge wanaomkosoa Makonda nao ni viongozi je wanafanya nini kupunguza watoto wa mitaani majimboni mwao?

Au kushangaa shangaa na kuwapa Mia Mia wale watoto mabarabarani ndiyo solution?

Hata swala la madawa ya kulevya walilalamika hivihivi lakini mwisho wa siku Makonda akaibuka kidedea baada ya madawa kupungua mtaani na mateja kuanza kulilia dawa za alosto.

Kampeni ya Makonda imegeuzwa kuwa kampeni ya kupima DNA na kulazimisha ndoa wakati siyo kweli.

Kama kwenye eneo unalotoka Kuna mama amekimbiwa na kuachiwa watoto awalee ndio utaelewa Makonda anamanisha nini.

Piga kazi Makonda na Mungu akubariki Sana ipo siku watakukumbuka tu ,hata Lowasa walimponda Sana na kumtukana lakini Leo ndio boss wao.
Hajazuiwa kufanya, isipokuwa afuate taratibu tulizojiwekea kupitia sheria zetu. Kama anaona sheria ni kikwazo aombe wabadilishe kwanza sheria ili imruhusu kufanya anachotaka. Huwezi kuendesha nchi kwa kila mtu kufanya anavyojisikia au kuona ni sawa. The end does not justify the means. Walioweka sheria kutaka faragha kwenye mambo haya hawakuwa wajinga au waliokosa uzalendo au wasiopenda watoto. Sasa mtu kama Lowassa na mkewe unawafidia vipi kwa stress alizowapa?

Tatizo langu kubwa na serikali hii ni kuacha mambo ya hovyo namna hii yatendeke ndio wanaanza kujitokeza kupinga. Ilianza lile la madawa, ikaja mabaraza ya ardhi, likaja hili la watoto....yote haya yalivunja sheria kwa namna moja ama nyingine.
 
Chadema wameiba billion 7 unatarajia Nini ?

Hizo taratibu tukajifunze kwa hao wezi ?
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom