Kuna habari kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuagiza msako wa kubaini wakazi wa Dar wasiyo na kazi maalum, operesheni km hiyo iliwahi kufanywa na mzee John Mhavile mwishoni mwa miaka 80 na mwanzoni mwa Miaka ya 90.
Wakati huo sisi wengine tulikuwa wanafunzi wa sekondari na nilikuwa nikiishi Kawe operesheni hiyo ilimuwia ugumu mh Mhavile na kumfanya mzee Alhaj Ali Hassan Mwinyi rais wa awamu ya pili kumwondoa mzee Mhavile hapa jijini na kuhamishiwa morogoro nadhani.
Hivi karibuni mkuu wa mkoa ametoa agizo la msako na tayari wajumbe wa Serikali za mitaa wameanza kutaka watu kujaza fomu na kuweka picha kutekeleza agizo la Rc Makonda, ni kweli jiji la Dar ina waalifu wengi sana lakini hawa waalifu wanajulikana na vyombo vya dola.
Nahisi Rc Makonda anataka kuonesha kutopata ushirikiano kutoka vyombo vya usalama vilivyo chini yake na kuomba ushauri vyombo ivyo ngazi za juu.
Mkuu wa mkoa anaongoza majeshi lukuki wenye wataalaam wabobezi ktk fani ya intelligence kimataifa anashindwaje kupata taarifa? Rc anaongoza RSO, DRSO, RIO, RCOs, MI, PCCB, uhamiaji, magereza, zimamoto, taasisi zote hizi zinawatalaam wa upelelezi na ujasusi wanashindwa kweli kumpa RC taarifa?
Huenda RC Makonda anapuuza ushauri wa kitalaam wa vyombo vyake. Nakumbuka wakati wa kuapisha wakuu wa mikoa mh Rais Dr Magufuli aliwaonya wakuu wa mikoa kuacha siasa ktk shughuli za kiutendaji.
Nadhani Makonda atambue ktk jiji hili watoto wasiyo na kazi lkn wanaishi na wazazi wao ukiwaondoa mjini utawapeleka wapi? Pia kuna wanafunzi wamemaliza vyuo wanahangaika kutafuta ajira unataka kuwapeleka wapi? Lkn pia kuna watumishi wa serikali ambao kimsingi hatakiwi ajulikane ht ndugu zake anafanya kazi gani? Sasa unataka kuleta ugomvi kati ya watendaji wa mitaa na wakazi wa jiji.
Mimi ni mwanaCCM, siungi mkono zoezi hili. Halina afya kisiasa km unatafuta wahalifu wasaidizi wako wanawafahamu wote labda awe kaingia mjini Jana.
Kumbuka kabla haujapata ajira UVCCM Mara baada ya kumaliza chuo ulikuwa wapi? Siyo vijana wote wanangekewa kama wewe wengine wanakaa hata miaka mitano wakisota ndiyo wanakuja kupata ajira.