Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Ama hakika Wewe ndiye Mkuu wa Mkoa ambaye yawezekana tokea wawepo Adam na Hawa hapajawahi kuwa na Mkuu wa Mkoa anayejituma kama Wewe hasa Kiutendaji / Kiuwajibikaji ( hasa kwa kuja na matamko ) na nahisi pengine hata huko Mbinguni tukienda na kukuta kuna Mikoa unaweza pia ukaukwaa huu huu Ukuu wako wa Mkoa.

Mimi nawashangaa sana Waswahili jinsi ambavyo hawakuelewi hasa katika mambo yako mengi ambayo huwa unayafanya hasa kwa Mkoa huu wa Dar es Salaam ila bahati nzuri Mimi GENTAMYCINE huwa nakuelewa vyema halafu haraka mno.

Yafuatayo ndiyo mema na maono ambayo mara kwa mara humtokea Binadamu mmoja tu aitwae Paul C. Makonda:

  1. Kati ya tatizo la Usafiri kwa Wanafunzi na Wanawake kuachika na Kuzalishwa na Waume zao Kwa Makonda suala la Wanawake hao ndilo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
  2. Kati ya tatizo la Uchafu katika Jiji la Dar es Salaam na Wanawake kuachika na kuzalishwa na Waume zao kwa Makonda suala la Wanawake hao ndiyo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
  3. Kati ya tatizo la Vibaka katika Jiji la Dar es Salaam na Wanawake kuachika na kuzalishwa na Waume zao kwa Makonda suala la Wanawake hao ndiyo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
  4. Kati ya tatizo la Mfumko wa Bei katika Bidhaa hasa kwa Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Wanawake kuachika na kuzalishwa na Waume zao kwa Makonda suala la Wanawake hao ndiyo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
  5. Kati ya tatizo la Maji kukatika hovyo katika Jiji la Dar es Salaam na Wanawake kuachika na kuzalishwa na Waume zao kwa Makonda suala la Wanawake hao ndiyo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
  6. Kati ya tatizo kubwa la Foleni katika Jiji la Dar es Salaam ambalo ' Kiuchumi ' linaigharimu sana nchi na Wanawake kuachika na kuzalishwa na Waume zao kwa Makonda suala la Wanawake hao ndiyo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
  7. Kati ya tatizo kubwa la Wafanyabishara ndogondogo ' Wamachinga ' kunyanyasika na kusumbuliwa na Askari wa Jiji la Dar es Salaam hadi na Watu wa TRA huku na Wao wakiwa wanasaidia Kukuza Uchumi wa nchi na pato lake na Wanawake kuzalishwa na kuachika na Waume zao kwa Makonda suala la Wanawake hao ndiyo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
Makonda Wewe piga Kazi tu ' Baba ' kwani uko vizuri sana na tunakukubali hasa Mimi kwani nakumbuka tokea ' Uteuliwe ' kuwa Mkuu wetu wa Mkoa ulishatutolea zaidi ya ' matamko ' kama 20 hivi na kuonyesha kuwa uko vizuri Kiutendaji na aliyekuteua hakukosea kabisa mpaka muda huu umeshaikamilisha 2 huku hiyo 18 iliyobaki ikikungojea Kwanza umalizane na hawa Wanawake waliozalishwa na kuachika na Waume zao.

Mimi nakuelewa mno ila nashangaa sijui kwanini Waswahili hawakuelewi au sijui wana Wivu tu nawe!

Nawasilisha.
 
Usitulazimishe kumuelewa nyie endeleeni kuelewana

Kumwelewa GENTAMYCINE hasa kwa ' maandiko ' yake yakupasa uwe na IQ kubwa ila ukija kichwa kichwa unaweza ukatoka patupu. Pole sana Mkuu kwa kutonielewa ila naelewa wale ' Great Thinkers ' wa kweli wa JamiiForums watasafiri vyema tu na Mimi ' Kimaudhui '.

Cc: amos eglan, New Nytemare
 
amos eglan Ungana na mwenzio luginyo katika kutonielewa. Nawapeni pole kubwa sana na ningewashauri tu hebu wapisheni ' Great Thinkers ' wenzangu tunaojuana humu wauchangie huu ' Uzi ' in a ' Critical ; mind. Tembeleeni ' threads ' zingine hii nadhani ni kubwa sana kwenu Kiakili na Kimapokeo. Na kupitia ' Uzi ' huu huu leo ndiyo nitazipima kwa uzuri sana IQ za Members humu kisha nifanye zangu ' conclusion '.

Cc: New Nytemare
 
GENTAMYCINE Hongera kwa kiwango cha utendaji wake, ila huwezi kusema tangu adamu na hawa...kuna viongozi wametumia pesa toka mfukoni kwao kuwahudumia wananchi, wengine wamefia kazini ktk kulitumikia taifa...sasa Makonda anayetumia pesa ya serikali huku akitimiza mipango iliyoandaliwa na watangulizi wake.

Unachoshindwa kuelewa ni kwamba Makonda ni mtoto pendwa kati ya watoto wote wa Baba, anasikilizwa na kupewa kipaumbele, mji wake ni strategic na miradi imelengwa kuwekezwa ktk jiji analolisimamia.

Naomba ufute kauli kuwa ni Mkuu wa mkoa bora tangu Adamu na Hawa.

Je, tukisema Chema chajiuza, kibaya chajitembeza ni sawa?
 
Hawa ndio wavuta bhangi wa JF

Mkuu wasamehe bure kwani siyo Kosa lao bali ni dhambi ya Kuzaliwa katika ' Koo ' zisizo na IQ kubwa na wao pia wakazaliwa na kujikuta hawana ' akili ' vile vile. Tunao wengi wengi tu humu na si ajabu kuna wengine pia kadri ' Uzi ' huu unavyozidi kwenda mbele utawaona wakijitokeza.

Ninachofurahi tu ni kwamba kupitia ' Uzi ' huu huu leo taratibu nitaanza kuwatambua ' Great Thinkers ' hasa Mkuu.

Cc: New Nytemare
 
Mkuu GENTAMYCINE Naungana na wewe kabisaa mkuu wa mkoa wetu mpendwa katika bwana mtume na nabii Paul C.Makonda anafanya kazi kubwa sana sijui kwa nini wengine hawataki kumkubali kama mimi na wewe tunavyomkubali, mkuu wachache watakuelewa wengine tuwapuuze tu mradi limetokea jina makonda wanapaniki
 
GENTAMYCINE
Ni ngumu kuwatambua maana watasoma baadhi ya comments hapo juu then watashtuka.....
Ili kuwatambua hawa wafuasi wa Kimambi ulitakiwa unyamaze tu bila kuwashtua...ungewapata wengi sana
 
GENTAMYCINE Wanaoeleweka ni hao wanaotaka umaarufu, kwa maneno, tena ya kuwatukana viongozi wa Serikali, akiwemo Rais, anayebeba maisha ya Watanzania wote, wakiwamo hao hao.

Akili dumavu zitabaki kudidimia kila kukicha.

WAKATI NDIO HUU
 
Back
Top Bottom