Prince Dos Santos
JF-Expert Member
- Nov 23, 2016
- 1,043
- 1,326
We jamaa huwa kuna threads zako unaniboa sana ila to be honest leo umeandika nondo ya nguvu sana , umeonesha Cahngamoto Kubwa zinazolikabili jiji letu hili lakini huyu bwana anakalia kufanya majukumu ya ustawi wa jamii ....................Big up sanaAma hakika Wewe ndiye Mkuu wa Mkoa ambaye yawezekana tokea wawepo Adam na Hawa hapajawahi kuwa na Mkuu wa Mkoa anayejituma kama Wewe hasa Kiutendaji / Kiuwajibikaji ( hasa kwa kuja na matamko ) na nahisi pengine hata huko Mbinguni tukienda na kukuta kuna Mikoa unaweza pia ukaukwaa huu huu Ukuu wako wa Mkoa.
Mimi nawashangaa sana Waswahili jinsi ambavyo hawakuelewi hasa katika mambo yako mengi ambayo huwa unayafanya hasa kwa Mkoa huu wa Dar es Salaam ila bahati nzuri Mimi GENTAMYCINE huwa nakuelewa vyema halafu haraka mno.
Yafuatayo ndiyo mema na maono ambayo mara kwa mara humtokea Binadamu mmoja tu aitwae Paul C. Makonda:
Makonda Wewe piga Kazi tu ' Baba ' kwani uko vizuri sana na tunakukubali hasa Mimi kwani nakumbuka tokea ' Uteuliwe ' kuwa Mkuu wetu wa Mkoa ulishatutolea zaidi ya ' matamko ' kama 20 hivi na kuonyesha kuwa uko vizuri Kiutendaji na aliyekuteua hakukosea kabisa mpaka muda huu umeshaikamilisha 2 huku hiyo 18 iliyobaki ikikungojea Kwanza umalizane na hawa Wanawake waliozalishwa na kuachika na Waume zao.
- Kati ya tatizo la Usafiri kwa Wanafunzi na Wanawake kuachika na Kuzalishwa na Waume zao Kwa Makonda suala la Wanawake hao ndilo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
- Kati ya tatizo la Uchafu katika Jiji la Dar es Salaam na Wanawake kuachika na kuzalishwa na Waume zao kwa Makonda suala la Wanawake hao ndiyo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
- Kati ya tatizo la Vibaka katika Jiji la Dar es Salaam na Wanawake kuachika na kuzalishwa na Waume zao kwa Makonda suala la Wanawake hao ndiyo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
- Kati ya tatizo la Mfumko wa Bei katika Bidhaa hasa kwa Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Wanawake kuachika na kuzalishwa na Waume zao kwa Makonda suala la Wanawake hao ndiyo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
- Kati ya tatizo la Maji kukatika hovyo katika Jiji la Dar es Salaam na Wanawake kuachika na kuzalishwa na Waume zao kwa Makonda suala la Wanawake hao ndiyo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
- Kati ya tatizo kubwa la Foleni katika Jiji la Dar es Salaam ambalo ' Kiuchumi ' linaigharimu sana nchi na Wanawake kuachika na kuzalishwa na Waume zao kwa Makonda suala la Wanawake hao ndiyo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
- Kati ya tatizo kubwa la Wafanyabishara ndogondogo ' Wamachinga ' kunyanyasika na kusumbuliwa na Askari wa Jiji la Dar es Salaam hadi na Watu wa TRA huku na Wao wakiwa wanasaidia Kukuza Uchumi wa nchi na pato lake na Wanawake kuzalishwa na kuachika na Waume zao kwa Makonda suala la Wanawake hao ndiyo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
Mimi nakuelewa mno ila nashangaa sijui kwanini Waswahili hawakuelewi au sijui wana Wivu tu nawe!
Nawasilisha.