Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Duuh...sina uhakika kama Africa tunahitaji Demokrasia hiyo kama ya Wazungu, labda na sisi tuwe na maana tofauti ya Demokrasia au tutafute mfumo wetu wa uongozi... kumbe keyboard yangu nzima haya ngoja nianze............

Kuna tafiti(research) kadhaa zimefanywa na wasomi wa saikolojia kuhusu ufanisi wa mtu akiwa katika situation(hali) mbali mbali, mfano kuna uwezekana mkubwa sana mchezaji mwenye uwezo mdogo kufanya vizuri akiwa anashangiliwa pia kuna uwezekano mkubwa mchezaji mwenye uwezo mkubwa kufanya vibaya akiwa anazomewa au mashabiki wakiwa hawamuamini(wananung'unika).

Imepita muda mrefu sasa tangu ndugu yetu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa
Paul Makonda apate ule mkasa kuwa hili jina analolitumia sio lake kuwa yeye anaitwa Bashite, Pia alifeli masomo yake nafikili wote mnajua sitaki nianze kuelezea mkasa wote ila kwa ninavyo wajua viongozi wa Tanzania kwa sifa na kutopenda kufedheeshwa angekua ameshapinga na kueleza ukweli ila yeye hakufanya hivyo na inapita karibia mwaka.
Kwa mtu muelewa unakua ushajua pasi na shaka Mheshimiwa Paul Makonda hana vyeti!

Lakini nadiliki kusema katika viongozi wa awamu ya tano ukiacha baadhi ya mawaziri Mheshimiwa Paul Makonda anafanya kazi nzuri sana.
Mheshimiwa huyu wanaedai hana vyeti kazi yake inaonekana na ameonekana na uthubutu wa kutatua matatizo ya wananchi kuliko viongozi wenye madigirii mengi sijui wenyewe wasomi mnaitaga maPHD sijui Madokiita aaah..mtajijua wenyewe.
Mheshimiwa huyu inasemekana anawahi sana kazini kwa kifupi ni mtu mwenye nidhamu na kazi pia mara nyingi kiongozi huyu ameonekana kuyaona matatizo yetu sisi watu wa hari ya chini, Hivi ni nani asiyejua kua hapa mjini watu tulikua na migogoro ya ardhi? Kiongozi huyu alituita na akatusaidia sio wote lakini tulio wengi kwa siku chache.

Hili la akina mama, nani asiyejua kuwa watu mmewazarisha dada zetu afu mmewatelekeza?
Nani hajaona kuwa pale Boma walijaa akina mama pote pale hadi hapakutosha? lakini yeye amejibebesha jukumu hili na anadai atawasaidia mi nasema inshallah tunakushukuru sana ingawa tutaumbuka wengi.
Yako mengi ambayo ameyafanya, ila hata asipofanikiwa ule uthubutu wake tuu unatosha sababu ametuonesha ni kwa namna gani wahusika hawajihusishi na hayo mambo au wanalegalega kwenye kazi zao (hili ni tatizo la taifa unakuta watu hawafanyi kitu, Rais akiongea ndo kila mtu anakurupuka).
Ni kweri wapo waliosoma hadi kuwa maprofesa lakini tumewapa uongozi hawatusaidii!! sisi wanini?? tunataka kiongozi atakaye tusaidia shida zetu za muda mfupi na mrefu, kiongozi anaefeel(sijui kiswahili chake) matatizo yetu, kiongozi anae yajua matatizo yetu!.

Ila kuna taarifa zisizo rasmi kuwa mheshimiwa anasifa za kijinga(element bar,seacliff hotel na clouds), sijui kweri eti anataka aogopwe/aheshimiwe kama Mungu kama kweri duuh basi ile elimu ya shule ya msingi imsaidie..

Hayo ni maoni yangu mimi nilie ishia darasa la nne muuza kahawa na kashata huku bonde la jangwani sijui nyinyi tulio wasomesha kwa kodi zetu mnasemaje?
 
KWA HILI NAKUUNGA MKONO MKUU,UTENDAJI KWANZA NA VYETI BAADAE.
 
RC wa Dar unaweza kumuita game changer..., kila leo yeye ni mahili wa kuamua watu wajadili nini katika mkoa anaoungoza kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Na kwa kuwa anajua wengi wa raia hasa hawa watumiaji wa mitandao ya kijamii wanahama na matukio bila hata uchambuzi wa kina.

Athari moja wapo ya hili jambo, kijamii ni kuwa upande wake ni faida, wananchi wa kawaida wanaona ni 'mkombozi wao' maana anawasikiliza kwa kila tatizo lao. Lakini upande wa pili ni kuwa hii ni njia ya kunyamazisha wakosoaji wake kisiasa. Unaweza kuona tukio la huyu dada, takwimu za awali alizotoa na suala zima la Joyce Kiria.

Kisiasa tukio hili linaharufu ya kumjenga na kumuongezea huruma ya "wanyonge"..

Kwa upande wa wakosoaji wa hili ni mambo tu ya kisiasa kuhisi fulani atakuwa na umaarufu wa kisiasa ila hoja yake nzuri. Tumuunge mkono kwa maslahi ya jiji la dar es salam na taifa kiujumla
 
Ukweli ukitolewa kuna watu kazi yao kupika data tu
Ila Mh paul makonda kawasaidia akina mama na mzigo Wa malezi kwani kweli walkuwa wametelekezewa watoto kuna familia moja nilpoipigia kuwasalmia uncle zangu niliambiwa na Bibi yao hadi nilcheka
imi:mama naomba kusalmiana na wajomba zangu
Mama aljibu : hawapo
Mimi: wameenda wapi ? Kucheza au?
Mama;"juzi toka tamko la Mh makonda watu wamekuja kuchukua watoto wao toka mwanza,arusha,etc wakaondoka nao wakisema wakalee watoto wao"
Mimi: wote kabsa hata uncle john? Maana yeye Ana umri kdogo?
Mama:nmesema wote kwa sasa npo na Dada zako tu (yaani Mh katupunguzia mzigo)
Mm:duuuu kumbe wkt mwngne watu wanapga kelele tu mtandaoni ila kumbe tamko ni tamko tu

Nazan mmeona hayo majadliano hapo juu mpigie mtu au ndg yako alieko Dar au Kama upo dar waambie watu ukweli acha uongo yangu ni hayo usibishe bila hoja wanaopelekea siasa ni wapenda siasa tu ila Mh makonda kundi la akna mama linamshukru japo kwnye msafara Wa mamba na kenge wamo
The End
 
Ukweli ukitolewa kuna watu kazi yao kupika data tu
Ila Mh paul makonda kawasaidia akina mama na mzigo Wa malezi kwani kweli walkuwa wametelekezewa watoto kuna familia moja nilpoipigia kuwasalmia uncle zangu niliambiwa na Bibi yao hadi nilcheka
imi:mama naomba kusalmiana na wajomba zangu
Mama aljibu : hawapo
Mimi: wameenda wapi ? Kucheza au?
Mama;"juzi toka tamko la Mh makonda watu wamekuja kuchukua watoto wao toka mwanza,arusha,etc wakaondoka nao wakisema wakalee watoto wao"
Mimi: wote kabsa hata uncle john? Maana yeye Ana umri kdogo?
Mama:nmesema wote kwa sasa npo na Dada zako tu (yaani Mh katupunguzia mzigo)
Mm:duuuu kumbe wkt mwngne watu wanapga kelele tu mtandaoni ila kumbe tamko ni tamko tu

Nazan mmeona hayo majadliano hapo juu mpigie mtu au ndg yako alieko Dar au Kama upo dar waambie watu ukweli acha uongo yangu ni hayo usibishe bila hoja wanaopelekea siasa ni wapenda siasa tu ila Mh makonda kundi la akna mama linamshukru japo kwnye msafara Wa mamba na kenge wamo
The End


makonda mwenyewe ndie aliyeanza geuza zoezi zima kuwa siasa baada ya kuanza kupost majina ya wanasiasa bila kuwa na ushahidi wowote wa DNA. inasikitisha sana mwanasiasa mbabaishaji kama makonda anapogeuza issue ambayo ni national tragedy na victims wote hawa esp watoto kuwa mtaji wake wa kisiasa mbaya sana. zoezi bado lingeweza kufanyika kimya kimya hasa ukizingatia ni mambo ya kifamilia na wausika wangefikishwa mahakamani kwa wale ambao wana dispute baina yao lakini kuanza kutangaza nina majina ya wabunge ni upuuzi kwani anayetenda kosa amefanya kosa na cheo chake isiwe msingi kwani watu wote ni sawa mbele ya sharia kama lilivyofeli zoezi lake la omba omba, rushwa na madawa ya kulevya na ili pia litaelekea huko huko
 
Salam kwenu wakuu, nimejaribu kufuatilia sana kazi za mkuu wetu wa mkoa wa Dsm , ni kweli mara nyingi kazi zinavyotangazwa inaonekana kbs wananchi wana tatuliwa kero zao lkn kadri muda unavyokwenda unagundua kila analo anzisha linakufa mfano kwa uchache vita ya dawa za kulevya, migogoro ya ardhi na sasa hili la watoto walio zaliwa na zingine nyingi,haya yote anayo yafanya Makonda ni masuala ambayo yana taratibu za kuyashulikia ndani ya serikali lkn yeye huyachukulia kama agenda yake binafsi, kama ana nia nzuri kwa nini asikae na hizo organs za serikali angalau wazungumze ili aweze angalau kuja na solutions zinazo eleweka badala ya kuwaita watu kwenye ma tv na kujazana ofis ya Makonda huku wakiwa na matumaini makubwa, mfano binafsi siamini kuwa Makonda kama ametatua tatizo la wanawake walio achiwa watoto zaid ya kuwa dhalilisha, hizi ni siasa zinazo fisha udhaifu wa serikali ya awamu hii, hakuna dhamira ya kweli kwenye hili, hiz ni siasa za kututoa watz katika kuhoji mambo ya msingi, mfano wa jambo moja ni binti mwenye umri wa miaka 31 anayesema Lowassa ni baba yake, ebu mtu kama Makonda atuambie huyu mtu anamsaidiaje? Kama si ujanja wa kumchafua Lowassa, ni watu wana siasa wangapi wenye watoto walio watekeleza nnje?
Watz tusiondolewe kwenye hoja za msingi, kama mtu katelekeza mtoto kuna taratibu zilizopo za kiserikali Makonda asijifanye kuwa anajua matatizo ya watz tuache kudanganyana!
Asalum
Nanini Ashton
Tandale-Dsm
 
Mkuu wa mkoa Paul Makonda bila shaka unaujua vizuri ufukwe wa koko. Kuna eneo maarufu la mihogo ambapo pametengwa pia eneo la kusali. Yote haya ni mambo mazuri yanayoongeza umaarufu wa eneo hili.

lakini kuna tatizo moja kubwa la uchafuzi wa mazingira zaidi katika hoteli/baa inayoendeshwa karibu na tawi la benki ya crdb. Eneo hilo limefanywa dampo. Uchafu kutoka hoteli/baa hiyo huchomwa hapo hapo kwenye ufukwe badala ya kuzolewa na kupelekwa dampo.

Kinachofanyika hapo kinapingana na juhudi zako za kuhakikisha jiji letu linakuwa safi. Je,, hili hujaliona na kama ni hivyo, tuma vijana wako wa mazingira watakuthibitishia hivyo. Kama una dhamira ya kukuza utalii wa ndani na nje kwa jiji la Dar, ufukwe wa koko unaweza kutoa mchango mzuri. Unapaswa kuendelezwa.
 
Kipindi hiki cha Mvua ndio wakati muafaka wa kutembelea vichochoro vyote vya jiji lako Mh Makonda.

Khali kwa ujumla ni mbaya saana, mh Rais aliona huruma na kuruhusu wafanyabiashara ndogondogo wasibughudhiwe mpaka wapatiwe maeneo maalumu.

Dooooh, viongozi ndo kwanza wametua mzigo hawajishughulishi tena, Mbagala rangi tatu wafanyabiashara wameongezeka maradufu barabarani hali ya uchafu ndo usiseme mifereji imeziba maji yanajaa ni hatariiiiii.



Mtaani makorongo kila mitaa ni wakati wa kuwaelekeza viongozi wahamasishe utaratibu bora wa mifereji kusaidia barabara za mitaa isiyoratibiwa vinginevyo jiji liko HOVYOOOO
 
Yupo bize kiki malalamike wapekeeni waliowachagua mbwa nyie
 
Habari za humu wanajamii.

Ule usemi usemao Mungu si athumani ama Mungu hadhihakiwi sasa unaenda kujidhihirisha baada ya Baba Mungu kumwaga majanga ndani ya mkoa wa Rc Makonda Dar es salaam anaejinasibu kama kiongozi mwenye huruma na kusaidia wanyonge.

Sasa tuuone ule moyo au kama ni mnafiki na kutafuta kiki sasa amefika mahali penyewe.

Tunamtaka Rc Makonda atumie nguvu na pesa kama ambavyo anafanya kuokoa, kutoa msaada kwa majanga haya.

Leo imeripotiwa kwa mujibu wa DW 17 aprili 2018., kuwa mpaka saaa vifo vya watu saba vilivyotokana na majanga ya mvua vimetokea.

Onyesha moyo, nguvu na upendo wako RC makonda, achana na vichekesho na maigizo, sasa swala tete ni hili la mafuriko. Tutakuona unafiki wako kwa hili. Mungu amekutia mtihani mwingine tena.
 
Back
Top Bottom