Salam kwenu wakuu, nimejaribu kufuatilia sana kazi za mkuu wetu wa mkoa wa Dsm , ni kweli mara nyingi kazi zinavyotangazwa inaonekana kbs wananchi wana tatuliwa kero zao lkn kadri muda unavyokwenda unagundua kila analo anzisha linakufa mfano kwa uchache vita ya dawa za kulevya, migogoro ya ardhi na sasa hili la watoto walio zaliwa na zingine nyingi,haya yote anayo yafanya Makonda ni masuala ambayo yana taratibu za kuyashulikia ndani ya serikali lkn yeye huyachukulia kama agenda yake binafsi, kama ana nia nzuri kwa nini asikae na hizo organs za serikali angalau wazungumze ili aweze angalau kuja na solutions zinazo eleweka badala ya kuwaita watu kwenye ma tv na kujazana ofis ya Makonda huku wakiwa na matumaini makubwa, mfano binafsi siamini kuwa Makonda kama ametatua tatizo la wanawake walio achiwa watoto zaid ya kuwa dhalilisha, hizi ni siasa zinazo fisha udhaifu wa serikali ya awamu hii, hakuna dhamira ya kweli kwenye hili, hiz ni siasa za kututoa watz katika kuhoji mambo ya msingi, mfano wa jambo moja ni binti mwenye umri wa miaka 31 anayesema Lowassa ni baba yake, ebu mtu kama Makonda atuambie huyu mtu anamsaidiaje? Kama si ujanja wa kumchafua Lowassa, ni watu wana siasa wangapi wenye watoto walio watekeleza nnje?
Watz tusiondolewe kwenye hoja za msingi, kama mtu katelekeza mtoto kuna taratibu zilizopo za kiserikali Makonda asijifanye kuwa anajua matatizo ya watz tuache kudanganyana!
Asalum
Nanini Ashton
Tandale-Dsm