Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza


Naisoma kwa mara ya tano hii post yako mkuu. You have a point for real. Binafsi naamini unaweza tuhumiwa na tuhuma zingine nzito zaidi ya hizi, na matusi juu, pamoja na nia njema ulio nayo. I can only guarantee you a lot of disappointment on your way to help us, kama ni picha basi halijaanza hilo ni trela.

But Brother we have come a long way to just give up now, naiona kiu ya kweli kutoka ndani ya moyo wako ya kua msaada kwa watu kama sisi, kamwe usiache kiu yako ikakatizwa na watu wapuuzi tu, tena wepesi mno! tangu uzi huu uanze umekua nuru gizani, kwa sisi tulio na ndoto za kufika ughaibuni kusaka maisha. Umekua honest na role model kwa kila alietembelea hapa. Martin Luther Junior alipingwa hata na blacks wenzie, mitume na manabii wa Mungu waliuwawa na kuteswa sababu ya upendo, wakristo watanikumbusha mahali furani paliandikwa kwamba yesu alifanya mambo mengi sana kiasi kwamba dunia haitoshi kuyaandika na kuyahifadhi, lkn binafsi naamini kazi kubwa aliyoifanya ni pale goligota aliposema Ee Baba wasamehe maana hawajui walitendalo. luther junior alisema pia "It's Only When It's Dark You Can See the Star" Its dark brother and you are one of those shining the stars. Please don't give up now. Just hang on there. nitafanya maombi kwa ajili ako, ile taa ya yenye nuru ang'avu ndani yako ambayo Mungu ameiwasha, kamwe isipungue makali wala isizimwe na mpango wowote wa kishetani. Go Bless you Brother. God Bless us all.

Binafsi nashughulikia issue ya Malta I will do may Best every step nitakua nawaupdate hapa kwa kila hatua though uchumi unasumbua kdg lakini Mungu akipenda this December nitakua nawapa updateas nikiwa Malta.
 
Shukrani mkuu.

Ningependa kujua kiasi gani natakiwa kuwa nacho ukitaka kufungua barber shop hapo Jo'burg ama cape town.

- chindo -
 
...ukishatapeliwa fanya kurudi kwenye hii comment ukumbuke nilichoandika! Naona watu povu zinawatoka wanapinga hoja kwa matusi na lugha kali. Hivi hata huko malta, utakwenda kwa miguu?


Hayajatimia tu? Hamjarudi kutizama hii space baada ya kupigwa?
 
Reactions: SDG
Hayajatimia tu? Hamjarudi kutizama hii space baada ya kupigwa?
Nani katapeliwa au unaota?wewe ni mmoja kati ya wafuataoha korosho
1. Mchawi / roho
2. Umeshakata tamaa na maisha
3. Kulakulala
4. Upeo wao ni kama wamtoto mchanga/ hujitambui
5. Huna malengo ya mda mrefu katika maisha yako
6. *******
 
Mkuu naomba mwongozo hizi nchi za free visa for Tanzanians, Haina haja ya kwnda ubalozi ?? ni pasport na tiket tu napanda ndege na kuondoka bila kuulizwa chochote ?? Naomba mwongozo wako mkuu
 

Woow
 
kadi ya kiliniki 5,000/
kadi ya kuzaliwa 30,0000/
Passport express(east africa) 15,000/
Passport 50,000/ ya serikali na 300,000/ ya wasee.
viza uliza wazoefu.

Anyway tanzania kila kitu kinawezekana ila tu uwe na chapaa, kama huna chapaa jamani watanzania wana roho mbaya usipime.
 
Wakuu nilishapitia uzi mmoja hivi unaitwa social path sasa huyu mgaka12 ni social path ni binadamu mjinga sijawai ona muda si mwingi nitachukua ban kwa sababu yake
Mkuu izzo Kuna ku migrate nisehemu ya ndoto zao please reverse uamuzi wako unahitajika zaidi ya unavyo fikiria stay blessed # thoroughGod# you make us achieve#
 
Mkuu naomba mwongozo hizi nchi za free visa for Tanzanians, Haina haja ya kwnda ubalozi ?? ni pasport na tiket tu napanda ndege na kuondoka bila kuulizwa chochote ?? Naomba mwongozo wako mkuu
Kakate tu ticket mkuu sema kuna ambazo ni visa free na zingine ni visa on arrival hapa immigration wa nchi husika watakuchaji kiasi kidogo , but ujiandae kwa maswali tu. mfano utakaa muda gani? shughuli gani imekuleta? Utafikia wapi?
 
Kakate tu ticket mkuu sema kuna ambazo ni visa free na zingine ni visa on arrival hapa immigration wa nchi husika watakuchaji kiasi kidogo , but ujiandae kwa maswali tu. mfano utakaa muda gani? shughuli gani imekuleta? Utafikia wapi?
Umenisaidia hata mm hapa,,,thanks sana mkuu
 
Shida ya WaTz ni kujisikia...yaani sisi ni full "Waswahili". Hili linaleta changamoto kwa wale wenye fikra za kujilipua. Ni lazima mjilipuaji awe na roho ngumu na kuwa na nia hasa. Zaidi ya hapo unawezafika unakoenda ukaishia kujitoa roho. Kuna mtu kazungumzia nauli, nauli sio ishu, mbona ni hela kidogo; ishu ni wapi unafikiria kufikia. Hapa ndipo kwenye kujisikia. Wenzetu (Kenya, Nigeria, nk) huwa ni rahisi sana kukaribishana, lakini sio sisi. Kwa hiyo kwa mjilipuaji hili ni kubwa kuliko nauli. Na pia ili maisha yaanze mahala fulani unahitaji mzoefu (zaidi kama hujawahi ishi huko unakojilipua). Maana hata hizo ajira za kubeba maboksi si rahisi hivyo kupatikana. Ulaya kuna watu kibao, hasa kutoka Ulaya Mashariki, ambao asubuhi wanaamka kuwahi hizo ajira. Hawa jamaa wana roho ngumu sana. Sio smooth kiviile hasa kama unakosa mwenyeji na wewe ndiyo mara ya kwanza kufika....
 
nimepoteza passport nikiwa Namibia je ni taratibu zipi za kufuata niipate nyingine uzuri nina electronic copy yenye particulars ya pass iliyopotea? Je uhamiaji wana database labda ya kudumu haitanihitaji kusubmit viambatanishi vya awali?
 
nimepoteza passport nikiwa Namibia je ni taratibu zipi za kufuata niipate nyingine uzuri nina electronic copy yenye particulars ya pass iliyopotea? Je uhamiaji wana database labda ya kudumu haitanihitaji kusubmit viambatanishi vya awali?

Requrements for replacement of lost or stolen Passport


MAHITAJI YA PASIPOTI ILIYOIBIWA/KUPOTEA/KUUNGUA

Ili kupata Pasipoti mpya baada ya ile ya awali kupotea, kuibiwa, kuharibika au kuungua zingatia yafuatayo:-

Taarifa ya Polisi (Police report)

Tangazo la gazeti

Barua ya maelezo inayoeleza kwa kina mazingira ya Pasipoti kuibiwa, kupotea, kuungua au kuharibika. Barua iandikwe kwa:-

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,

Idara ya Uhamiaji,

S.L.P. 512,

DAR ES SALAAM.

Hati ya kiapo kinachoelezea kwa kina mazingira ya kuibiwa, kupotea au kuharibika kwa Pasipoti (Sworn declaration of the circumstance surrounding the LOSS, THEFT OR DAMEGE of Passport).

Kama mazingira yanatokana na kuungua kwa nyumba ama kuvunjwa inahitajika ulete barua ya Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa kulipotokea tukio hilo na ripoti ya zimamoto kwa wale waliounguliwa na nyumba

Uthibitisho wa safari

Cheti cha kuzaliwa muombaji na cheti/kiapo cha kuzaliwa baba au mama wa mwombaji

Kwa waombaji ambao wamepoteza Pasipoti nje ya nchi anatakiwa alete Shahada ya Dharura (Emergency Travel Document) aliyotumia kuingia nchini

Pamoja na vielelezo hapo juu viambatanishwe na fomu ya maombi ya Pasipoti iliyojazwa vizuri. (Form CT 5(Ai))

NOTE:

Ada ya Pasipoti iliyoibiwa au kupotea ni Tsh. 100,000/= kwa waliopoteza mara ya kwanza, iliyopotea au kuibiwa mara ya pili ada ni Tshs. 200,000/= na malipo kwa Pasipoti iliyoharibika/kuungua ni Tshs. 50,000/=
 
Duuuh aisee safi sana
 
nimepoteza passport nikiwa Namibia je ni taratibu zipi za kufuata niipate nyingine uzuri nina electronic copy yenye particulars ya pass iliyopotea? Je uhamiaji wana database labda ya kudumu haitanihitaji kusubmit viambatanishi vya awali?
Egbert44 naweza kukujia pm km hutajali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…