Ushauri: Mdee na wenzake wafungue shauri waombe Mahakama Kuu izuie jaribio la kuwafuta Ubunge

Ushauri: Mdee na wenzake wafungue shauri waombe Mahakama Kuu izuie jaribio la kuwafuta Ubunge

Tume na bunge hawajawafukiza uanachama
Wanachoenda kushtaki ni kupinga kufukuzwa uanachama kinyume cha sheria na katiba ya Chadema

Wamefoji matokeo ya kura hadi wakajisahahu kanda nne hazipo kwenye matokeo yaliyotangazwa!!! Huo ni uhuni
Mkuu, sababu za kuwafukuza uanachama, zinatokana na namna walivyofika bungeni kinyume na vikao vya chama chao. Kwa hiyo Tume ya uchaguzi na bunge lazima litahusika kwenye lolote ambalo hao 19 wataliendeleza kuanzia sasa.

Hapo ndipo watatakiwa waseme nani aliwajazia form, kusaini na kuzipeleka tume ya uchaguzi, ilihali form alizopewa katibu mkuu wa CDM John Mnyika bado anazo na hazikufanyiwa kazi.
 
Hawa waliteliwa kwa vikao halali, kwa barua ya CDM, na wakaapishwa, waende mahakamani kesho kwa hati ya dharura!
Na kwa sababu wanampenda sana Mbowe na Mnyika hizo nyaraka wameshindwa kuzitoa mpaka leo? Na wmahakamani wataenda kuomba zuio dhidi ya Bunge? Chadema haina mamlaka yeyote ya kuwanyang'anya ubunge. Mamlaka yao yameishia kwenye uanachama wao.

Amandla...
 
Mchakato mzima wa uchaguzi uliingiliwa kwa madai yao na huo ndio wanauita "uhuni".
uliingiliwa kivipi?kama walijiteua wenyewe wakajipeleka bungeni bila ridhaa ya chama nani ataamini huo ugoro wanaosema sasa hivi
 
Mimi naona waende tu mahakamani ili ukweli ujulikane nani yupo sahihi kati ya CHADEMA na wakina Halima. Mimi nimewamiss sana Kibatala, Mtobesya, Mallya, Kihwelo, Matata, Nkungu na mawakili wenzao. Toka kesi ya Mbowe iishe nikiingia mitandaoni sioni zile amsha amsha za mahojiano ya hao mawakili na mashahidi wa upande wa serikali.

Kwa hiyo wakina Halima wakienda mahakamani walau tutakuwa na kitu cha kujifunza kwenye mambo ya "forgery" kama ilivyokuwa kwenye ugaidi mpaka nikajua baadhi ya vifungu vya GPO.
Hii forgery ilifanywa kwa amri ya watu wa level ya juu sana, hivyo huwezi kuisikia hii kesi.
 
Umejuaje mkuu kama walipewa barua na Chadema? Chadema walikana kufanya hivyo since day one, ushahid wao pia walizungumzia issue ya Husna aliyekua magereza; so na wewe kwa akili yako unaamini kwamba Chadema wangeweza ku influence Husna atolewe magereza, tena USIKU!? Tutumie ubongo kufikiri, hivi viungo vingine tuviache vifanye kazi yao na ubongo pia ufanye kazi yake!
Tena hapo kwa Husna, waliocheza huu mchezo walikosea kuficha nyayo zao. Hili liliwaumbua. Lakini kuna watu wana akili ndogo hawawezi hata kufikirisha bongo zao.

Cc chinembe YEHODAYA
 
Ubora wa mwanasiasa ni kuwa muadilifu. Nazidi kutilia mashaka maandiko yako kama unashabikia wanasiasa wasio waadilifu na kuwaita asset bora ya kisiasa. Mwanasiasa anayeweza kulaghaiwa na kuikana itikadi yake na ya chama chake unamuita asset! Kwelinimeamini mtu kadri anavyozeeka na akili yake huzeeka.
Ndiyo maana alipata kura moja (1) kule Kawe.
 
Hawajafukuzwa Ubunge, Bali uanachama. Kama wanataka Ubunge waende bungeni waendelee na vikao vya bajeti maana chadema iliwadukuza uanachama, kuhusu Ubunge watajuana wao na spika wao. Mbona kamati kuu iliwafukuza lakini wakaendelea na Ubunge.

Kamati kuu haijawai kukaa kikao zaid ya jana
 
Ukiona mtu anatetea Malaya Malaya wa kisiasa ujue hata yeye ni Malaya. Huyo Pascal hajitambui ni njaa kali inamla. Anafikiri kwa kutumia Makalio akizani Watanzania bado wajinga Kama yeye na hao vibaraka wao Covid19.

Kama hao akina Mdee waliteuliwa kihalali walishindwa nini kuleta ushahidi wao Mbele ya Kamati kuu walipo itwa awali au ktk Baraza kuu la Chama lililo keti Jana? Wao si walikata rufaa Sasa hizo rufaa si huwa unaweka na sababu na ushahidi?
Kwa nini walihudhuria kikao Cha Baraza kuu huku wakijua kuwa ni kikao Cha Wahuni na maamuzi yangekuwa ya kihuni?
Pascal umepitwa na wakati huu sio wakati wenu tena pumzika umesha zeeka hizo siasa za Karne ya 15 usituletee wakati huu.
Umemaliza mkuu.
 
Halima si mjinga kiasi hicho,hawezi kwenda Mahakamani anajua akienda huko atawaingiza Mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi na Bunge mahali pagumu.

Waliomsaidia kutenda uovu lazima wana uwezo wa kumwambia sasa basi. Mungu wa Chato hayupo kupindisha sheria na kuvunja katiba.

Ngongo kwa sasa Uganda.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji3]
 
Na kwa sababu wanampenda sana Mbowe na Mnyika hizo nyaraka wameshindwa kuzitoa mpaka leo? Na wmahakamani wataenda kuomba zuio dhidi ya Bunge? Chadema haina mamlaka yeyote ya kuwanyang'anya ubunge. Mamlaka yao yameishia kwenye uanachama wao.

Amandla...

Wewe nae kiaz huna chama umekua vipi mbunge [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom