Uchaguzi 2020 Ushauri muhimu sana kwa Tundu Lissu tukielekea Oktoba 2020

mwarobaini_,

Mleta mada Mbona hujielewi. Lissu jana kaongelea matatizo ya wakulima ya kuachwa wazalishwe kwa shida alafu wanapangiwa bei na mahali pa kuuza, hukusikia? Na alisema akiwa yeye raisi hilo halitakuwepo?

Lissu jana kaongelea maslahi duni ya watumishi wa afya na akasema akiingia madarakani ataboresha maslahi ya watumishi wa afya. Sio tu kujenga majengo na kununua vifaa. Hukusikia?

Lissu jana kasema ataboresha mahusiano ya kimataifa akiingia madarakani. Au haukusikia? Aliponda Sera za magufuli za kuwadhihaki marafiki zetu wa kweli na watu wanaotusaidia kweli. Wewe hukusikia hilo?

Kama una chuki na Lissu kanywe tu maji ila Lissu anapiga kunako!!! Jiandaeni tu!
 
Kwani usipomtaja mtu ndio hutajua anayezungumzwa ni nani! Kwahiyo unaruhusu yote yasemwe ila tusitajane majina!
Cha muhimu ni kujikita zaidi kwenye sera badala ya kumshambulia mtu.
Lakini ikilazimu kurusha vijembe kidogo (jambo ambalo sio zuri) basi asitaje majina ya watu.
 

Kwamba Lissu hajui kuwa anayehitajika ni:



?

Mbona itakuwa kutojitendea haki mwenyewe?

Kuwa Lissu hadi sasa hana wana mikakati mahiri wa caliber za akina Membe au kina Axelrod?

David Axelrod (political consultant) - Wikipedia

Mbona pia itakuwa ni kujilisha upepo?

Ingekuwa CCM tungesema CCM mbele kwa mbele.
 
Sina chuki na Lissu, na nimefurahia kurejea kwake. Lakini sote tunazijua siasa za Lissu, ndio maana tunashauri. Ushauri sio hukumu ya mahakama kwamba lazima ufuatwe.
 
Sina chuki na Lissu, na nimefurahia kurejea kwake. Lakini sote tunazijua siasa za Lissu, ndio maana tunashauri. Ushauri sio hukumu ya mahakama kwamba lazima ufuatwe.

Pamoja na yote si haba kutambua kuwa Lissu hawezi kuwa 'that cheap' kama wengine wanavyotaka kudhani na hata kufikiria kuwa wangeweza kuwa better.

Huyu bwana alishambuliwa kwa risasi na wanaomhofia. Kwa kuhofiwa kwake tu alishambuliwa. Kwa thamani yake jitihada zote zilifanyika kumwokoa.

Kwamba alirejea kama alivyo rejea, na sasa ndiyo huyo yuko hapo alipo, itakuwa kujidanganya mno kwa awaye yote kujidhania angeweza kuwa better kuliko Lissu. Au hata kuja na hoja nyepesi nyepesi kwa jina la ushauri.

Yasije kuwa ya Taifa Star kuishauri Brazil namna ya kuchukua kombe la dunia pamoja na kuwa ushauri si hukumu eti kuwa si lazima kuuchukua!
 
Namba 1 na 2 ndicho hasa Magu anastahili kufanyiwa. HasaHasa Ndicho kinachomstahili.
 
lazime amshambulie magufuri binafsi. si ndo mshindani wake, au unafiri magufuri anaposemaga serikali yake? urais wake? anakuwa kanywa pombe zake.
 

Hana uwezo wa kuliepuka hilo, na siku akiacha washabiki wake wataona anawasaliti,
Bila kumtaja magufuli hana kitu kingine anaweza kusema ambacho yeye atakuwa wa kwanza kukisema hapa duniani.

Anasema amgufuli anajenga bwawa na kwamba sio wa kwanza kujenga hilo bwawa, eti kuna mabwawa mengi yalijengwa, je yalimaliza matatizo?
Je yeye akiingia madarakani atatoa vitu vya kufanya hapa tanzania kutoka mbinguni ili vionekane tofauti na vilivyopo?

Ni kipi yeye atafanya ambacho hakipo tanzania au hapa duniani?
Je atajenga hospitali angani au?
Je atanunua ndege za kkukimbia ardhini bila kuruka?
Je yeye atafanya nni ambacho hakijafanyika hapa tanzania?
AU atahalalisha ushoga kwenye katiba?

Akumbuke kwamba hayo mabwawa yalijengwa na chama cha mapinduzi na magufuli anaendeleza kwa hali ya sasa na ijayo kulingana na mahitaji ya watu hivyo basi hakuna haja ya kuweka chama kingine kwa kuwa hakina jipya kitakacholeta kwenye ardhi hii hata wapate uongozi wataendeleza vilivyoanzishwa na CCM.

Hapa ni ushauli tu kama anataka vitu vipya basi akasome hapa
1, reli ya ndni ya maji
2 jutengeneza submarine ,
3 kutengenez hizo ndege tanzania
4, viwanda vikubwa vya magari
5, tecknorojia ya anga
6,mabarabara ndani ya maji.
7, nk
Hapo atweza kuonyesha utofauti na chma caha CCM.
 
ujinga haujaisha, tunataka kufuta ujinga wa namna yako kwanza,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…