Ushauri: Nahitaji kuchukua mkopo wa milioni 30 kwajili ya biashara ya mahindi

Ushauri: Nahitaji kuchukua mkopo wa milioni 30 kwajili ya biashara ya mahindi

Tani 32 unadhani unafika tu unanunua unaondoka na unafika nazo dar unapata faida..? Haha
Kwa Tani 32 nnae mtu ambae kwa wiki tutajaza gari 2kwaiy tani 64 kwa wiki nae nampa chake tukimaliza msimu wote sio kila round , ni jamaa yangu dalali wa mazao na mzoefu
 
Unaweza KUCHUKUA mkopo na ukaanza biashara kwa mara ya kwanza na ukafanikiwa, ila itabidi uzingatie mambo haya.

1.hakikisha unakuwa sehemu ya hio biashara (uwe muhusika namba 1) na utambue ni wapi sehemu sahihi za kuchukua mzigo, na pia lazima ujue bei za mahindi kwa Kanda tofauti.

2.hakikisha unalijua soko lako nje ndani, yaani tambua kila kitu fanya uchunguzi wa kina kabisa (jipe muda katika tafiti za kina).

3.hakikisha usiwe na sehemu moja ya kuuzia mzigo wako, hapa itakubidi uwe mbunifu, na utambue wewe hautakuwa wa kwanza kufanya hio biashara, hivyo jifunze kwa waliotangulia. (Na uzuri mashine zipo nyingi kwa Dar hii ni fursa pia).

4.Baada ya kuzingatia hayo mambo matatu 3, hakikisha uwe unajua gharama za uendeshaji ni kiasi gani, na pia faida unaipataje.

5.Baada ya kujua faida unaipataje, aangalia changamoto zake ni zipi kuhusu hio biashara, na kwa kiasi gani utaweza kupambana nazo, hakikisha changamoto zote unazijua na uzuri zipo wazi tu.

6.kumbuka, kama ukiamua kuwa na soko zaidi ya moja itakubidi uwe na fremu ambayo haitakuwa mbali sana na soko lako ambapo hapo utaweka mzigo wako na itakuwa kama store...(unaweza kuiweka Manzese, Gongo la mboto, Chanika, Mbagala) maana ukumbuke wateja wako watakuwa ni watu wa mashine kama sisi, ukiachana na hao wachina...

7.Hakikisha uwe na vibali vya kufanya hio biashara, ili kuepusha kusumbuliwa na serikali.

8.Mpaka kufikia hapa najua utakuwa unajua uanze na kiasi gani, na kiasi gani kiwe kama balance.

9.Omba Mungu kwa imani yako, akusadie kwa kila hatua, na ndo iwe tabia yako.

10. ikiwa utahitaji kufanya kazi na mimi basi karibu sana 😀, maana biashara yangu nauza sembe na dona, sehemu za kupata mahindi nazifahamu unaweza kwenda kuchukua mzigo na kuleta ofisini kisha mimi nitatoa gharama za uendeshaji za huo mzigo ikiwemo kukoboa kusaga na kufanya packaging na kuusambaza unga, nembo itatumika yangu na leseni itatumika yangu... isipokuwa faida tutagawana 50 kwa 50.

Kila la kheri mdau...
Umeongea mengi ila hapo hakuna litakalofanya afanikiwe kwenye hio biashara.
Atafute wafanyabiashara wa hio kazi akae nao awafanyie kazi hata miezi miwili, atakuwa ashaelewa kila kitu
 
Kwa Tani 32 nnae mtu ambae kwa wiki tutajaza gari 2kwaiy tani 64 kwa wiki nae nampa chake tukimaliza msimu wote sio kila round , ni jamaa yangu dalali wa mazao na mzoefu
Muongo huyo, labda kama lengo ni upate tu mahindi hata kwa bei ambayo hautapata nayo faida, haha
Hii biashara naifanya nina miaka 10, haipo rahisi kiasi hicho
 
Umeongea mengi ila hapo hakuna litakalofanya afanikiwe kwenye hio biashara.
Atafute wafanyabiashara wa hio kazi akae nao awafanyie kazi hata miezi miwili, atakuwa ashaelewa kila kitu
Hapana nimeanza biashara ya vitunguu maji na Alhamdulillah sjakaa na hao wafanyabiashar kuwafanyia kaz na kumbuka ile pia ni mali kuoza na mpk saiv naendelea nayo vzur na nshakua vzur kuliko ata wenyeji , nimejifunz kupitia huko huko makosa nlioanza nayo
 
Muongo huyo, labda kama lengo ni upate tu mahindi hata kwa bei ambayo hautapata nayo faida, haha
Hii biashara naifanya nina miaka 10, haipo rahisi kiasi hicho
Sawa kiongoz nipe njia mbadala ila sio kuacha kuifanya hii kaz , nipe njia
 
Mkuu achana na huo usengerema utakuja nishikuru,Bwana Bashe kazuia mahindi kwenda Malawi Kuna gari imebeba mzigo hapa tunahaha kutafuta mteja boder Dili limekua dilisha!
Ndio nimeona hio habar...ila m nauzia hapa hapa nchini sio nje na sio leo mwez kuanzia sasa
 
Mm sikushauri uchukue mkopo kwa ajili ya kuanza biashara ambayo hauna uelewa nao vizuri.Asante
nakazia hapa, angalau faida au mshahara anayopata awe ananunua na kuweka store au aanze na mtaji kidogo ili aielewe vyema biashara ndo aje ajiripue baadae
 
nakazia hapa, angalau faida au mshahara anayopata awe ananunua na kuweka store au aanze na mtaji kidogo ili aielewe vyema biashara ndo aje ajiripue baadae
Ndio imebidi nianze kwnz ata tani 5 kisha badae nkiwa mzoefu ntaifanya kiukamilifu , swez kuita kujilipua kwsbb saiyo ntakua najua nnachokifanya kwa uhakika mkubwa hata ikifeli ghafla ntajua natakiwa nfanyaje saiyo
 
Mkuu soko la mahindi umelipata ila unasikia ni kibaha wachina wananunua "Umesikia"?

Plan B yako ni ipi ikiwa hilo soko halijakidhi matarajio yako?

Plan C yako ni ipi ikiwa umenunua mahindi ambayo sio mazuri kutokana na kutokuwa na uzoefu wa biashara hiyo.

Plan D yako ni ipi ikiwa pesa uliyokopa 30 Millions ukashindwa kuirudisha.

Fanya research ya kutosha mkuu harafu pia kama utaanza basi usianze na msingi wote huo wa 30 Millions kwa mara moja.

Anza na kiasi kidogo ambacho you can afford to lose then baada ya biashara kuwa na uhakika nayo ndio unaingia mazima.
 
Bei 53000 mikoani vijijini hasa mbeya songwe na rukwa kwa gunia lenye ujazo wa 108 kgs

Mosture nitatizo kwa Sasa sababu mahindi ni mapya hivyo ningeku shauri kuanzia mwezi wa Saba mkuu japo kwa Sasa una weza kupeleka lakini kwa kuanika kwanza

Ambalo kutapelekea kupungua kwa idadi ya gunia

Kibaha kweli Kuna soko la mahindi na siku tatu zilizo pita Lili kuwa 800 per kg

Lakini Jana na Leo naskia limeshuka na yote nikutokana na mzigo kuingia kwa kasi

Kwasasa wekeza mda kufanya utafiti wa masoko Kisha kuanzia mwezi wa Saba unaweza kuanza kazi

Na kuhusu kiasi mil kumi inatosha mkuu mahindi sio Bei Sana 🙏🙏🙏
 
Hakuna mfanyabiashara mwenye uzoefu unaoutaja anakuja hapa jf kuandika upuuzi ulioandika hapa
Sawa nimeelwa ila Nd maana natafta hizo ABC nkishamaliza naanza kazi...Am 24 nimemaliz chuo nimefanya Kaz za vitunguu majinvery high risk mashamban na mvua na unajua vitunguu natoa mang'ola napeleka dar , singida , iringa uko nyanzwa , njombe , moshi kote nimeingy kwaiy mahindi naona kwangu risk ndogo ila ndoivo natfta kwanz nyie viongoz wangu mnipe maelekezo muhim
 
Huu ndio u
30m kama ndio jiwe lako huna option nyingine cheza nayo defensive game usiwe unashambulia muda wote.

Unapaswa kuilinda Kwa kufanya biashara ambazo ni non-risk/ au risk ni ndogo lakini ni low profit wakati unausoma mchezo.
Angalia unauzoefu wa nini? aanza kidogokidogo hata na 10m
HUu ndio ushauri sio watu wamekazana tu ooh usifanye biashara kwa pesa ya kukopa je kama hana option ya kupata pesa bila kukopa?

Chaku mshauri zaidi atumie akili aanze kidogo kidogo huku akiusoma mchezo asiingie miguu yote miwili.

Ila kwa ushauri wangu aingie kusini lindi huko chimbo akusanye ufuta apeleke ghalani hiyo hela inaweza ku double akicheza vzr.
 
Mkuu soko la mahindi umelipata ila unasikia ni kibaha wachina wananunua "Umesikia"?

Plan B yako ni ipi ikiwa hilo soko halijakidhi matarajio yako?

Plan C yako ni ipi ikiwa umenunua mahindi ambayo sio mazuri kutokana na kutokuwa na uzoefu wa biashara hiyo.

Plan D yako ni ipi ikiwa pesa uliyokopa 30 Millions ukashindwa kuirudisha.

Fanya research ya kutosha mkuu harafu pia kama utaanza basi usianze na msingi wote huo wa 30 Millions kwa mara moja.

Anza na kiasi kidogo ambacho you can afford to lose then baada ya biashara kuwa na uhakika nayo ndio unaingia mazima.
Sawa nashjuru brother...nd niko kweny hayo maswali pia.... Soon ntaenda apo kibaha kifatilia na nshapata mwenyeji ,, Plan B kuhusu Soko ikiwa halijakidhi ntahakikisha nannua kile kifaa Cha kupima kwasbb nshapewa tayar details za mzgo kukidhi basi ukiwa na hicho kifaa ni uhakika kwsbb unaanzia shambn kupima , pia kama itakua sivyo niko pia natafta masoko mengn ya kuuzia kama manzese n.k , Pia kuhusu pesa kushindwa kuirudsha nimeeka kiwanja kikubwa bond inaogopesha ila ndoivo lazm utake risk 😂
 
Bei 53000 mikoani vijijini hasa mbeya songwe na rukwa kwa gunia lenye ujazo wa 108 kgs

Mosture nitatizo kwa Sasa sababu mahindi ni mapya hivyo ningeku shauri kuanzia mwezi wa Saba mkuu japo kwa Sasa una weza kupeleka lakini kwa kuanika kwanza

Ambalo kutapelekea kupungua kwa idadi ya gunia

Kibaha kweli Kuna soko la mahindi na siku tatu zilizo pita Lili kuwa 800 per kg

Lakini Jana na Leo naskia limeshuka na yote nikutokana na mzigo kuingia kwa kasi

Kwasasa wekeza mda kufanya utafiti wa masoko Kisha kuanzia mwezi wa Saba unaweza kuanza kazi

Na kuhusu kiasi mil kumi inatosha mkuu mahindi sio Bei Sana 🙏🙏🙏
apo kaka information tosha bro , Naomba nije inbox
 
Hakuna mfanyabiashara mwenye uzoefu unaoutaja anakuja hapa jf kuandika upuuzi ulioandika hapa
Nipo siendi mahali, nimeanzisha hii thread na ntaimaliza mm na nkifeli ntawaambia nimefeli na nkifaulu mtaona progress , Apo nimeandika uhalisia kuwa nimefanya mali kuoza kwann niogope mahindi wakati ni low risk tofaut na vtunguu maji ??? au wap hujaelewa , na huku nimekuja kutfta research zaidi najua utaulza kwnn umekuja huku kama n low risk
 
Huu ndio u

HUu ndio ushauri sio watu wamekazana tu ooh usifanye biashara kwa pesa ya kukopa je kama hana option ya kupata pesa bila kukopa?

Chaku mshauri zaidi atumie akili aanze kidogo kidogo huku akiusoma mchezo asiingie miguu yote miwili.

Ila kwa ushauri wangu aingie kusini lindi huko chimbo akusanye ufuta apeleke ghalani hiyo hela inaweza ku double akicheza vzr.
yahh kwakwel bro.. Sina namna ya kuifanya zaidi ya kukopa pesa na ushaur wenu naufanyia kaz kuanza kidg kidg ata tani 5 au 10

Na nlidokezwa kuhusu ufuta ila sa uzoefu huo nd sina kbsaaa amna hata ndg yangu anaejua huko ntapata hasara kubwa napaogopa 😂😂


 
Back
Top Bottom