Habar mimi naishi Dar nataka niombe mkopo wa million 30 kwajili ya biashara ya mahindi, nikachkue vijijini tani 32 nilete Dar kuuza kwani kwenye tani nyingi ndo faida ilipo. Mnashaurije wadau? Hilo la kwanza.
La pili : Soko nimepata nasikia Kibaha kwa wachina ukipeleka ni fasta tu na malipo ni siku 3 mpk 5 je ni kweli na je kuna changamoto yoyote?
La Tatu: Ninachoogopa mimi ni upande wa Quality nasikia kuna quality inayohitajika kwa mahindi ya zamani na mapya kuhusu unyevunyevu au moisture, sasa nitajuaje hiyo quality nasikia kuna kile kifaa je nitaweza kupima tani 32 kwa haraka haraka na kule kwenye soko je wanakata bei wakiona quality yako ndogo?
KAMA KUNA MTU ANAYEHUSIKA ANAYEFAHAMU ZAIDI JUU YA HILI ANICHEKI MSAADA WAKO MUHIMU
Unaweza KUCHUKUA mkopo na ukaanza biashara kwa mara ya kwanza na ukafanikiwa, ila itabidi uzingatie mambo haya.
1.hakikisha unakuwa sehemu ya hio biashara (uwe muhusika namba 1) na utambue ni wapi sehemu sahihi za kuchukua mzigo, na pia lazima ujue bei za mahindi kwa Kanda tofauti.
2.hakikisha unalijua soko lako nje ndani, yaani tambua kila kitu fanya uchunguzi wa kina kabisa (jipe muda katika tafiti za kina).
3.hakikisha usiwe na sehemu moja ya kuuzia mzigo wako, hapa itakubidi uwe mbunifu, na utambue wewe hautakuwa wa kwanza kufanya hio biashara, hivyo jifunze kwa waliotangulia. (Na uzuri mashine zipo nyingi kwa Dar hii ni fursa pia).
4.Baada ya kuzingatia hayo mambo matatu 3, hakikisha uwe unajua gharama za uendeshaji ni kiasi gani, na pia faida unaipataje.
5.Baada ya kujua faida unaipataje, aangalia changamoto zake ni zipi kuhusu hio biashara, na kwa kiasi gani utaweza kupambana nazo, hakikisha changamoto zote unazijua na uzuri zipo wazi tu.
6.kumbuka, kama ukiamua kuwa na soko zaidi ya moja itakubidi uwe na fremu ambayo haitakuwa mbali sana na soko lako ambapo hapo utaweka mzigo wako na itakuwa kama store...(unaweza kuiweka Manzese, Gongo la mboto, Chanika, Mbagala) maana ukumbuke wateja wako watakuwa ni watu wa mashine kama sisi, ukiachana na hao wachina...
7.Hakikisha uwe na vibali vya kufanya hio biashara, ili kuepusha kusumbuliwa na serikali.
8.Mpaka kufikia hapa najua utakuwa unajua uanze na kiasi gani, na kiasi gani kiwe kama balance.
9.Omba Mungu kwa imani yako, akusadie kwa kila hatua, na ndo iwe tabia yako.
10. ikiwa utahitaji kufanya kazi na mimi basi karibu sana 😀, maana biashara yangu nauza sembe na dona, sehemu za kupata mahindi nazifahamu unaweza kwenda kuchukua mzigo na kuleta ofisini kisha mimi nitatoa gharama za uendeshaji za huo mzigo ikiwemo kukoboa kusaga na kufanya packaging na kuusambaza unga, nembo itatumika yangu na leseni itatumika yangu... isipokuwa faida tutagawana 50 kwa 50.
Kila la kheri mdau...