Ushauri: Nahitaji kuchukua mkopo wa milioni 30 kwajili ya biashara ya mahindi

Tani 32 unadhani unafika tu unanunua unaondoka na unafika nazo dar unapata faida..? Haha
Kwa Tani 32 nnae mtu ambae kwa wiki tutajaza gari 2kwaiy tani 64 kwa wiki nae nampa chake tukimaliza msimu wote sio kila round , ni jamaa yangu dalali wa mazao na mzoefu
 
Umeongea mengi ila hapo hakuna litakalofanya afanikiwe kwenye hio biashara.
Atafute wafanyabiashara wa hio kazi akae nao awafanyie kazi hata miezi miwili, atakuwa ashaelewa kila kitu
 
Kwa Tani 32 nnae mtu ambae kwa wiki tutajaza gari 2kwaiy tani 64 kwa wiki nae nampa chake tukimaliza msimu wote sio kila round , ni jamaa yangu dalali wa mazao na mzoefu
Muongo huyo, labda kama lengo ni upate tu mahindi hata kwa bei ambayo hautapata nayo faida, haha
Hii biashara naifanya nina miaka 10, haipo rahisi kiasi hicho
 
Umeongea mengi ila hapo hakuna litakalofanya afanikiwe kwenye hio biashara.
Atafute wafanyabiashara wa hio kazi akae nao awafanyie kazi hata miezi miwili, atakuwa ashaelewa kila kitu
Hapana nimeanza biashara ya vitunguu maji na Alhamdulillah sjakaa na hao wafanyabiashar kuwafanyia kaz na kumbuka ile pia ni mali kuoza na mpk saiv naendelea nayo vzur na nshakua vzur kuliko ata wenyeji , nimejifunz kupitia huko huko makosa nlioanza nayo
 
Muongo huyo, labda kama lengo ni upate tu mahindi hata kwa bei ambayo hautapata nayo faida, haha
Hii biashara naifanya nina miaka 10, haipo rahisi kiasi hicho
Sawa kiongoz nipe njia mbadala ila sio kuacha kuifanya hii kaz , nipe njia
 
Mkuu achana na huo usengerema utakuja nishikuru,Bwana Bashe kazuia mahindi kwenda Malawi Kuna gari imebeba mzigo hapa tunahaha kutafuta mteja boder Dili limekua dilisha!
Ndio nimeona hio habar...ila m nauzia hapa hapa nchini sio nje na sio leo mwez kuanzia sasa
 
Mm sikushauri uchukue mkopo kwa ajili ya kuanza biashara ambayo hauna uelewa nao vizuri.Asante
nakazia hapa, angalau faida au mshahara anayopata awe ananunua na kuweka store au aanze na mtaji kidogo ili aielewe vyema biashara ndo aje ajiripue baadae
 
nakazia hapa, angalau faida au mshahara anayopata awe ananunua na kuweka store au aanze na mtaji kidogo ili aielewe vyema biashara ndo aje ajiripue baadae
Ndio imebidi nianze kwnz ata tani 5 kisha badae nkiwa mzoefu ntaifanya kiukamilifu , swez kuita kujilipua kwsbb saiyo ntakua najua nnachokifanya kwa uhakika mkubwa hata ikifeli ghafla ntajua natakiwa nfanyaje saiyo
 
Mkuu soko la mahindi umelipata ila unasikia ni kibaha wachina wananunua "Umesikia"?

Plan B yako ni ipi ikiwa hilo soko halijakidhi matarajio yako?

Plan C yako ni ipi ikiwa umenunua mahindi ambayo sio mazuri kutokana na kutokuwa na uzoefu wa biashara hiyo.

Plan D yako ni ipi ikiwa pesa uliyokopa 30 Millions ukashindwa kuirudisha.

Fanya research ya kutosha mkuu harafu pia kama utaanza basi usianze na msingi wote huo wa 30 Millions kwa mara moja.

Anza na kiasi kidogo ambacho you can afford to lose then baada ya biashara kuwa na uhakika nayo ndio unaingia mazima.
 
Bei 53000 mikoani vijijini hasa mbeya songwe na rukwa kwa gunia lenye ujazo wa 108 kgs

Mosture nitatizo kwa Sasa sababu mahindi ni mapya hivyo ningeku shauri kuanzia mwezi wa Saba mkuu japo kwa Sasa una weza kupeleka lakini kwa kuanika kwanza

Ambalo kutapelekea kupungua kwa idadi ya gunia

Kibaha kweli Kuna soko la mahindi na siku tatu zilizo pita Lili kuwa 800 per kg

Lakini Jana na Leo naskia limeshuka na yote nikutokana na mzigo kuingia kwa kasi

Kwasasa wekeza mda kufanya utafiti wa masoko Kisha kuanzia mwezi wa Saba unaweza kuanza kazi

Na kuhusu kiasi mil kumi inatosha mkuu mahindi sio Bei Sana πŸ™πŸ™πŸ™
 
Hakuna mfanyabiashara mwenye uzoefu unaoutaja anakuja hapa jf kuandika upuuzi ulioandika hapa
 
Huu ndio u
HUu ndio ushauri sio watu wamekazana tu ooh usifanye biashara kwa pesa ya kukopa je kama hana option ya kupata pesa bila kukopa?

Chaku mshauri zaidi atumie akili aanze kidogo kidogo huku akiusoma mchezo asiingie miguu yote miwili.

Ila kwa ushauri wangu aingie kusini lindi huko chimbo akusanye ufuta apeleke ghalani hiyo hela inaweza ku double akicheza vzr.
 
Sawa nashjuru brother...nd niko kweny hayo maswali pia.... Soon ntaenda apo kibaha kifatilia na nshapata mwenyeji ,, Plan B kuhusu Soko ikiwa halijakidhi ntahakikisha nannua kile kifaa Cha kupima kwasbb nshapewa tayar details za mzgo kukidhi basi ukiwa na hicho kifaa ni uhakika kwsbb unaanzia shambn kupima , pia kama itakua sivyo niko pia natafta masoko mengn ya kuuzia kama manzese n.k , Pia kuhusu pesa kushindwa kuirudsha nimeeka kiwanja kikubwa bond inaogopesha ila ndoivo lazm utake risk πŸ˜‚
 
apo kaka information tosha bro , Naomba nije inbox
 
Hakuna mfanyabiashara mwenye uzoefu unaoutaja anakuja hapa jf kuandika upuuzi ulioandika hapa
Nipo siendi mahali, nimeanzisha hii thread na ntaimaliza mm na nkifeli ntawaambia nimefeli na nkifaulu mtaona progress , Apo nimeandika uhalisia kuwa nimefanya mali kuoza kwann niogope mahindi wakati ni low risk tofaut na vtunguu maji ??? au wap hujaelewa , na huku nimekuja kutfta research zaidi najua utaulza kwnn umekuja huku kama n low risk
 
yahh kwakwel bro.. Sina namna ya kuifanya zaidi ya kukopa pesa na ushaur wenu naufanyia kaz kuanza kidg kidg ata tani 5 au 10

Na nlidokezwa kuhusu ufuta ila sa uzoefu huo nd sina kbsaaa amna hata ndg yangu anaejua huko ntapata hasara kubwa napaogopa πŸ˜‚πŸ˜‚


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…