USHAURI: Nani asimame kati ya Baba mlezi na Baba mzazi kwenye send off na harusi!!

Kulikuwa na ndoa kati yao baba mzazi na mama?.Kama ndoa ilikuwepo ndiyo yeye akazaliwa,atakuwa baba mzazi ndiye mwenye haki.Ila kama hakukuwa na ndoa,basi baba mzazi ni ganda la muwa tu.
 
Mtu haitwi baba kisa amekulea kama ni hivyo wajomba kibao wangestahili hiyo Title.

Mtu anaitwa baba ikiwa amekusababishia wewe kuwepo duniani kifupi mbegu imetoka kiunoni mwake.

Sasa unajiuliza nini peleka kwa baba mwenyewe afurahie uwepo wako
Sasa mbona Diamond ushauri huu hamumpi!?.
 
Baba mlezi apewe credit.
 
Ungevaa viatu vya waliolelewa bila baba ungeelewa. Baba anakula bata alafu mtoto akikua akumbukwe wee katu
 
Mwache atoe tuu siku ya sendoff tena mbele ya baba yake mzazi ili nae aone uchungu wa mtoto wake kumwomba hela halafu anamzumgusha. Msitake kufanya mambo kama yapo kawaida jamani
Mimi kama baba mzazi, kwenye sendoff yake napelekwa nini?

Hiyo harusi yake afanye kama sehemu ya yeye kupata familia siyo kwa ajili ya kumlingishia baba mzazi, haimsaidii chochote na wala baba mzazi haimpunguzii chochote.
 
Watu kama nyie ndio mnachangia ongezeko LA watoto wa mtaani.
Kabisa. Baba zembe tu halilei ulionee huruma. Kwani huyo mama anayeachwa na mimba au mtoto alee mwenyewe ye hawezi kumtelekeza, ni kwa sababu Hana jinsi. Ni kama msalaba wa Yesu msalabani alijitwisha. Mama anakuwa Hana jinsi.
 
Hivi hiz send off ni lazima?na huu utamaduni ulitoka wapi
 
Kusalenda sio tatizo. Ila uende mazima. Sio ukiona mambo yamekuwa mazuri unaanza kujileta leta
Yani baba mzazi mnamkandia kama vile anahitaji hiyo alphad na mahali.
Jamaa amekaa zake Iringa wala hana shida na mtu
 

Nafasi ya baba mzazi ipo pale pale
 
Kuna Dada nilizaa nae.....tulikuwa na malengo mazuri ila baadae mambo yangu yakakwama....yule Dada akawa amempata MTU mwingine....wakaoana. Mawasiliano yalikuwa mazuri kati yangu na mama mtoto....tukawa tumekubaliana mtoto akikua amrudishe kwao ili nipatacho tunagawana na Ivan wangu,na wazazi wake hasa mama alijua hayo makubaliano.
Baada ya muda yule Dada akanipigia simu kuniambia mtoto sio wangu alinisingizia.
Nikawaza sana..ila as a man nikaamua kumtafuta mama mtoto wangu private anithibitishie kuhusu uamuzi wake. Hakuja na akaenda mbali zaidi kumwambia mamake kuhusu yeye kunisingizia.

Nikaamua kuachana na hilo suala...baada ya miaka miwili siku moja napigiwa simu na huyo mwanamke akiniomba matumizi ya mtoto. Nilimpandishia sana na tulifikishana mbali.
Najua IPO siku Ivan wangu ataambiwa nilimkataa. Maybe!!
so tusiwe wepesi wa kumponda baba mzazi na kumtetea baba mlezi. Huenda baba mlezi ndo kachangia uhusiano wao kuvunjika.
Mahari apewe baba mzazi ni haki yake.
Gari apewe baba mlezi.

Baba mzazi ashirikishwe fully kwenye mipango ya ndoa ndiye mwenye kutamka BARAKA. Asante.
 
Umezungumza kitu kikubwa mnooo
 
Ivan sio wako lakini
 
Pole

Huenda ni kweli mtoto sio wako.
 
Pole

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwa kuwa
1. Baba amehusika katika malezi kiasi fulani
2. Na binti alikuwa anaenda likizo kwa baba mzazi
3. Na baba mlezi karuhusu aende akafanyie Send-off kwa baba mzazi

Binti aende kwa baba mzazi tu ili kuweka mambo sawa. Baba mlezi ji mtu muungwana sana. Pia huwezi jua kwa nini baba mlezi kamruhusu huenda kuna mambo anaepusha. Hizi familia za kiafrika zi madudu mengi sana . Kama anampenda baba mlezi basi ahakikishe anasikiliza maoni yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…