Ushauri: Nataka kuacha kula wanga kwa mwaka mzima

Ushauri: Nataka kuacha kula wanga kwa mwaka mzima

Mkuu hiyo njia yako ya kula inaweza kukata kitambi?
Yes inaweza. Kitambi ni fat deposits tu. So when your body starts metabolising energy from fats instead of carbohydrates automatically mafuta yote yanaunguzwa. Lakini ujue kwamba hiki sio kitu cha kuona matokeo ndani ya wiki moja. Consistency is the key kwenye this issue
 
Yes inaweza. Kitambi ni fat deposits tu. So when your body starts metabolising energy from fats instead of carbohydrates automatically mafuta yote yanaunguzwa. Lakini ujue kwamba hiki sio kitu cha kuona matokeo ndani ya wiki moja. Consistency is the key kwenye this issue
Ntaanza maana nna ktamba
 
Upo sahihi.
Acha kula wanga, sukari, mafuta na ikitokea sasa umekula wanga jitahidi iwe mchana na kiasi kidogo.
Kula sana mbogamboga, protein, matunda.
Mie binafsi huwa nanenepa sana nikila wanga, sukari, na ma vya kula ya mafuta.
Lakini nikiacha kula hayo mavyakula napungua ninakula mcharooo na ninakuwa mwepesi sana.
Kama ujuavyo sisi wamama ndo wapishi wa familia, kwa kiasi fulani ni ngumu kucontrol mfano mchana ukiwa unalisha mtoto anataka mle wote(watoto wangu huwa wanataka tule wote, na wakiona nakula mboga mboga tu na wao eti wanagoma kula) usiku mume nae anataka mle wote au akulishe, wageni nao wakija ni noma kuanza kujieleza umewapikia eti wewe huli inabidi uzuge ule, ukienda ugenini napo changamoto maana kama mnajua sisi ni watanzania.
Changamoto ni nyingi sana kufikia malengo.

Ila all in all ni kupambana na hizo challenge, mfano sasa hivi nina mwezi wa 2 nimeacha mno kula wanga inatokea mara chache sana nikadokoa wali maharage vijiko 2, pilau kijiko 1, chapati robo(hivi vyote haizidi mara 1 kwa wiki)
Hii ni ratiba yangu.
Asubuhi nachemsha maji moto yakiwa na tangawizi, mchaichai abdalasini, kisha naweka limao.
Masaa 2 baadae nakunywa kikombe cha maziwa fresh labda mayai 2 kuchemsha, au maziwa matupu.
Mchana nakula parachichi, mchemsho wa mboga za majani, kama nikipata kitoweo iwe kuku, samaki au nyama choma au mchemsho poa(ni lazima kimojawapo nipate)
Usiku mara nyingi nakunywa mtindi, au smoothie ya mtindi&parachichi&,passion.
Safi sana,naomba unisaidie wazo,ndizi za kuchemsha Zina wanga mwingi?? No nzuri nikizila kwa wingi??
 
Fanya intermittent fasting na mazoezi kidogo itakusaidia.
Mimi nimenenepa mpaka sijipendi ila nimepunguza kula hovyo nafanya na mazoezi kidogo lakini nimeanza kuona napungua taratibu.
Pia ukiweza unafunga na vimazoezi hata nyumbani asubuhi na jioni kwa nusu saa.
Ila sijui kama inaapply kwa kila mtu au inategemea na mtu.
Hiyo kuacha wanga ilinishinda Mana kipato changu hakinuruhusu zaidi nitakuwa nafanyia kazi tumbo.
Maa shaa Allah al ustaadhaat. Barakallah fiiyk
 
Sasa wewe unajutafutia maradhi ambayo hukuwanayo yakiwemo vidonda vya Tumbo jiulize tangu udogowako Mama alikuwa anakupa chakula gani hadi sasa hivi unajifanya hupendi vyakula vya wanga? Angalia isiige Maisha
Mwezi Dec 2021 nilikua napata maumivu ya tumbo. Nilienda Agakhan nikawa diagnosed na hivyo vidonda. Nimepambana navyo na dawa za hospitali inaonekana ndio vilikua vinaanza. Nimepona. Nakula kila kitu.
Sema nini? Vidonda vya tumbo havisababishwi na kutokula.
 
Uko sawa...sukari ni sukari. Na mechanism ya digestion yake ni ile ile...iwe ya kiwandani au ya tunda sukari ni sukari na effect yake kwenye mwili ni the same.
Sikujua hili,nilijua ya kiwandani mbaya na ya matunda ni nzuri
 
Mwezi Dec 2021 nilikua napata maumivu ya tumbo. Nilienda Agakhan nikawa diagnosed na hivyo vidonda. Nimepambana navyo na dawa za hospitali inaonekana ndio vilikua vinaanza. Nimepona. Nakula kila kitu.
Sema nini? Vidonda vya tumbo havisababishwi na kutokula.
Shukrani,Nini husababisha? Funguka boss
 
Yes inaweza. Kitambi ni fat deposits tu. So when your body starts metabolising energy from fats instead of carbohydrates automatically mafuta yote yanaunguzwa. Lakini ujue kwamba hiki sio kitu cha kuona matokeo ndani ya wiki moja. Consistency is the key kwenye this issue
Asante Sana,nami naanza kupunguza wanga,matokeo ni km baada ya siku ngapi??
 
Ug
Pia to add on that, epuka kabisa sugars and processed foods. Hasa hasa soda. Pia product za ngano digestion yake hua inachukua muda so sio nzuri. Pendelea kukula vyakula vya asili kama ugali n.k.. Uandaaji pia ni suala lingine, the food should be nutritious zaidi kuliko ya kujaza tumbo tu
Ugali sio chakula cha asili...usimdanganye mwenzako
 
Well ni mfumo wa kula kwa baadhi ya masaa na ku-fast a.k.a kufunga kwa masaa yaliyobaki katika masaa 24. The one ambayo nimeitumia mara kwa mara ni ya 16/8 hrs. Yaani kwa masaa 16 nafunga, alaf masaa 8 nakula. So in essence mlo wangu wa kwanza unaanzia saa sita mchana na wa mwisho unatakiwa uwe by saa mbili usiku. Then after hapo hakuna ninachokula zaidi ya maji na kahawa (bila sukari), pia kahawa sio lazima. Kwenye hayo masaa 8 unaruhusiwa kula chochote (lakini kwa kiasi, sio unafukia kama unaenda kuchinjwa). Hvyo mlo wa kwanza unaeza kua a light meal, japo sio lazima kutegemeana na kipato. Personally hua huo mlo wa kwanza ni lunch. After hapo, jioni kama saa kumi na mbili unaeza pata dinner. After hapo hata ukipata maziwa before saa mbili n sawa pia. Hakuna rwstrictions. Do what works for you lakini tu muhimu iwe katika hiyo timeframe. Mwanzon itakua ngumu kucover hizo 16hrs but in 2 to 3 weeks mwili unazoea na unasahau kabisa suala la njaa.
Angalizo. Huo muda wa kuanza kula (the 8 hour block) sio lazima uanze saa sita kamili mchana, ni mapendeleo yako na shughuli zako. Cha muhimu uwe unakula in 8 hrs block na unafunga hozo nyingine.
Pia itategemea na kazi unayofanya,ikiwa heavy duty kama mafundi migodini au wajenzi ni vizuri mlo wa asubuhi usikose. Lakini kama ni ofisini hiyo ratiba pendekezwa ni sawa.
 
Shukrani,Nini husababisha? Funguka boss
Kwa miaka mingi sana jamii iliamini vidonda vya tumbo husababishwa na tumbo kukaa muda mrefu bila chakula.

Ukweli ni kwamba, vidonda husababishwa na bacteria waitwao Helicobacter Pylori au kwa kifupi H-pylori. Wadudu hawa huondoa ile layer ikaayo juu ya kuta za tumbo/utumbo. Hivyo basi sehemu hiyo huwa inakuwa imelika mfano wa sehemu ya barabara yenye pothole (kishimo).
Na kwa kuwa tumbo huachia acids ili kumeng'enya chakula, acids hizi zikigusa sehemu ile yenye kidonda ndipo mtu huhisi maumivu makali.
Njaa ina accelerate kuuma vidonda kwa sababu acids zikiachiwa na tumbo liko empty ina maana direct vitagusa sehem zenye vidonda.
H-pylori wanatibika.
 
Habari wana jamvi.

Kijana wenu nikiwa na umri wangu wa miaka 33 kamili, nimedhamiria kwa hiyari yangu mwenyewe, bila kushurutishwa wala kushawishiwa na mtu yeyote; kuacha kula kabisa vyakula vyenge wanga. Vyakula vyenye wanga kwa wingi ni kama mahindi, mpunga, mihogo, viazi, magimbi, ngano, mtama n.k

Inaaminika kisayansi vyakula hivi vikitumika kwa wingi vinasababisha sana kitambi na unene, kisukari na magonjwa ya moyo.

Juzi Jumatatu, 21.03.22 nikaanza movement yangu bila kuwa na mpango maalum. Asubuhi sikujua ntakula nini...mpaka imefika saa 5 sijala kitu. Sehemu za kula zote zina vitafunwa tulivyovizoea maandazi, chapati, vitumbua, mikate, viazi, mihogo and the likes. Ikafika saa 7 njaa inauma vibaya sana mpaka nikahisi kutetemeka mwili.

Nikajisemea cha kufia nini? Nikala zangu dona safi, nyama, maharage na spinach. Baadae nikawa nakunywa tu maji.

Sasa najiona kabisa sina plan na sielewi hii game inachezwaje. Najua humu kuna wazoefu wa haya mambo. Naomba mnisaidie wenzangu msiokula wanga ama heavy meals mnafanyaje?

Mnakula nini hasa? Na mliishindaje njaa hizi siku za mwanzo mpaka tumbo lizoee? Maana ile juzi nilihisi mpaka kizungu zungu.
Mimi napenda sana nyama iwe ya kuku, ng'ombe, mbuzi, kuku n.k. Ndio udhaifu wangu mkubwa.

Nipeni ushauri wadau. Hili ndio lengo la uzi.
Asanteni.
NB: sina ugonjwa wowote unaonizuia kula chochote.
Kiswahili bwana, yaani niliposoma unaacha kula wanga nikashikwa na butwaa kuja kusoma kulikoni unakula wachawi, kumbe ni wanga huu wa vyakula.
 
kitakacho kudhuru sio wanga ni mafuta wanayopikia mitaani ni yapi?na yamepikiwa mara ngapi ? na rangi yake ikoje ? wengi watu huumia bila kujijua wanapokula nje.huwezi kuepuka kula chakula cha wanga kula ila punguza. mchele uoshe pia pikia maji mengi kisha ikichemka mwaga maji itakuwa umeiondoa wanga
 
kitakacho kudhuru sio wanga ni mafuta wanayopikia mitaani ni yapi?na yamepikiwa mara ngapi ? na rangi yake ikoje ? wengi watu huumia bila kujijua wanapokula nje.huwezi kuepuka kula chakula cha wanga kula ila punguza. mchele uoshe pia pikia maji mengi kisha ikichemka mwaga maji itakuwa umeiondoa wanga
Sukari wanga na hayo vegetable oil vyote vina shida.
 
Back
Top Bottom