Ushauri: Nataka kuacha kula wanga kwa mwaka mzima

Mkuu hiyo njia yako ya kula inaweza kukata kitambi?
Yes inaweza. Kitambi ni fat deposits tu. So when your body starts metabolising energy from fats instead of carbohydrates automatically mafuta yote yanaunguzwa. Lakini ujue kwamba hiki sio kitu cha kuona matokeo ndani ya wiki moja. Consistency is the key kwenye this issue
 
Ntaanza maana nna ktamba
 
Safi sana,naomba unisaidie wazo,ndizi za kuchemsha Zina wanga mwingi?? No nzuri nikizila kwa wingi??
 
Maa shaa Allah al ustaadhaat. Barakallah fiiyk
 
Sasa wewe unajutafutia maradhi ambayo hukuwanayo yakiwemo vidonda vya Tumbo jiulize tangu udogowako Mama alikuwa anakupa chakula gani hadi sasa hivi unajifanya hupendi vyakula vya wanga? Angalia isiige Maisha
Mwezi Dec 2021 nilikua napata maumivu ya tumbo. Nilienda Agakhan nikawa diagnosed na hivyo vidonda. Nimepambana navyo na dawa za hospitali inaonekana ndio vilikua vinaanza. Nimepona. Nakula kila kitu.
Sema nini? Vidonda vya tumbo havisababishwi na kutokula.
 
Uko sawa...sukari ni sukari. Na mechanism ya digestion yake ni ile ile...iwe ya kiwandani au ya tunda sukari ni sukari na effect yake kwenye mwili ni the same.
Sikujua hili,nilijua ya kiwandani mbaya na ya matunda ni nzuri
 
Shukrani,Nini husababisha? Funguka boss
 
Asante Sana,nami naanza kupunguza wanga,matokeo ni km baada ya siku ngapi??
 
Ug
Ugali sio chakula cha asili...usimdanganye mwenzako
 
Pia itategemea na kazi unayofanya,ikiwa heavy duty kama mafundi migodini au wajenzi ni vizuri mlo wa asubuhi usikose. Lakini kama ni ofisini hiyo ratiba pendekezwa ni sawa.
 
Shukrani,Nini husababisha? Funguka boss
Kwa miaka mingi sana jamii iliamini vidonda vya tumbo husababishwa na tumbo kukaa muda mrefu bila chakula.

Ukweli ni kwamba, vidonda husababishwa na bacteria waitwao Helicobacter Pylori au kwa kifupi H-pylori. Wadudu hawa huondoa ile layer ikaayo juu ya kuta za tumbo/utumbo. Hivyo basi sehemu hiyo huwa inakuwa imelika mfano wa sehemu ya barabara yenye pothole (kishimo).
Na kwa kuwa tumbo huachia acids ili kumeng'enya chakula, acids hizi zikigusa sehemu ile yenye kidonda ndipo mtu huhisi maumivu makali.
Njaa ina accelerate kuuma vidonda kwa sababu acids zikiachiwa na tumbo liko empty ina maana direct vitagusa sehem zenye vidonda.
H-pylori wanatibika.
 
Kiswahili bwana, yaani niliposoma unaacha kula wanga nikashikwa na butwaa kuja kusoma kulikoni unakula wachawi, kumbe ni wanga huu wa vyakula.
 
kitakacho kudhuru sio wanga ni mafuta wanayopikia mitaani ni yapi?na yamepikiwa mara ngapi ? na rangi yake ikoje ? wengi watu huumia bila kujijua wanapokula nje.huwezi kuepuka kula chakula cha wanga kula ila punguza. mchele uoshe pia pikia maji mengi kisha ikichemka mwaga maji itakuwa umeiondoa wanga
 
Sukari wanga na hayo vegetable oil vyote vina shida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…