Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ongeza na samaki wa kuchoma, nyama chomaNiko wiki ya nne sasa bila ya kutumia chakula chochote cha wanga. Naomba nikupatie ratiba yangu ya chakula kwa siku.
Naamka saa 11, napata maji ya uvuguvugu yaliyotiwa ndimu. Napiga pushup kidogo kisha najiandaa kwenda ofcn.
Kwa kuwa nina usafiri wangu, mrs anakuwa ananifungashia juice ya kutosha anayotengeneza mwenyewe. Juice hii inakuwa ya mchanganyiko wa matunda mbalimbali na mboga mboga kama karoti, nyanya, parachichi, embe, apple, nk. Epuka matunda yanayotoka South Africa, mengi ni GMO.
Nakunywa juice hiyo around saa 2 asb na saa 4 asb.
Saa tano napata dafu.
Saa saba napata mboga za majani na matunda kama ndizi na parachichi.
Saa tisa napata tena juice (huwa nabeba ya kutosha na nahifadhi kwenye friji ofcn.
Naweza pia kuwa na snacks kama karanga au tende
Nikirudi nyumbani saa kumi na mbili napata juice au saladi ya mchanganyiko wa matunda na mboga mboga.
Wakati mwingine hiyo inakuwa imetosha kabisa na nakuwa sihitaji kupata kitu kingine zaidi ya chai ya mchanganyiko wa viungo iliyotiwa asali.
Siku nyingine naweza kula maboga yaliyochemshwa pamoja na vitu kama njugu mawe, choroko au kunde.
By the way mimi nimeamua kupunguza sana matumizi ya nyama ili kupunguza asidi mwilini.
Joannah hujawahi kuniangusha kamwe kwa vituko ulivyonavyo [emoji12][emoji16]Kwani kitambi kinauma?kwa Nini mateso yote hayo?mbinguni hamna wanga utaukumbuka!
Mawatu yanjitesa hadi naamua kuyashangaa tu badala ya kuyaonea huruma [emoji28]Huwezi pungua kupitia kuacha kula peke yake.
Naona wadau wengi wanasema wameacha wanga na mwili umepungua.
Mwili unapungua kwa mawili ama ufanyiwe operation au ufanye mazoezi. Intentional starvation itabackfire na ulcers na magonjwa mengine.
Halafu mazoezi ni ishu ndogo sana. Yaani wewe unayeruka kichura chura mara tano kila siku you are better off kuliko mimi ninayekesha nacheza PS.
Kisukari ni kibaya sana...Kwani kitambi kinauma?kwa Nini mateso yote hayo?mbinguni hamna wanga utaukumbuka!
😂😂😂Wanga mtamu bwana.yaani aache wali mwaka mzima kisa kitambi!Joannah hujawahi kuniangusha kamwe kwa vituko ulivyonavyo [emoji12][emoji16]
Soda, nyama nyekundu, nyama za kwenye makopo/beef sausage,kuku wa kizungu na mayai ya kizungu, sembe, ngano iliyokobolewa, maziwa ya ng'ombe wa kisasa, chipsi mayai feki, piza, baga, chai ya rangi ni hasara na ujinga mtupu wa Mtu kujitakia [emoji6]Ni kweli asiache sukari kabisa, atumie kidogo kwenye chai na matunda ya sukari ale tu Wala hayana shida, ila soda ndo anaweza kuacha Ili kuzuia kujaza mwili sukari ya ziada angekuwa bonge ndo ningemshauri ale nini na hiyo kufunga Ili apungue ila kutokula wanga kabisa simshauli kuacha ila kula kidogo sana na upande wa vegetables ndo uwe sana pamoja na matunda, niliacha sukari kwa muda wa miaka miwili madhara niliyopata bila kujua mpaka Leo najuta hivyo Kila kitu kwenye mwili ni muhimu ila kwa vipimo sahihi na kuzidi au kupungua ndo kunakoleta matatizo kiafya.
Upo sahihi..haya mambo yanakwenda na genes za muhusika.Haya mambo ya unene na ulaji naonaga labda tu ni asili ya mtu si wengine tunabugia kila kitu na bado hatuwi mabonge.
Bila shaka kwa ratiba hii huna kitambi. Mwenye vidonda vya tumbo hii ratiba haiwezi.Well ni mfumo wa kula kwa baadhi ya masaa na ku-fast a.k.a kufunga kwa masaa yaliyobaki katika masaa 24. The one ambayo nimeitumia mara kwa mara ni ya 16/8 hrs. Yaani kwa masaa 16 nafunga, alaf masaa 8 nakula. So in essence mlo wangu wa kwanza unaanzia saa sita mchana na wa mwisho unatakiwa uwe by saa mbili usiku. Then after hapo hakuna ninachokula zaidi ya maji na kahawa (bila sukari), pia kahawa sio lazima. Kwenye hayo masaa 8 unaruhusiwa kula chochote (lakini kwa kiasi, sio unafukia kama unaenda kuchinjwa). Hvyo mlo wa kwanza unaeza kua a light meal, japo sio lazima kutegemeana na kipato. Personally hua huo mlo wa kwanza ni lunch. After hapo, jioni kama saa kumi na mbili unaeza pata dinner. After hapo hata ukipata maziwa before saa mbili n sawa pia. Hakuna rwstrictions. Do what works for you lakini tu muhimu iwe katika hiyo timeframe. Mwanzon itakua ngumu kucover hizo 16hrs but in 2 to 3 weeks mwili unazoea na unasahau kabisa suala la njaa.
Angalizo. Huo muda wa kuanza kula (the 8 hour block) sio lazima uanze saa sita kamili mchana, ni mapendeleo yako na shughuli zako. Cha muhimu uwe unakula in 8 hrs block na unafunga hozo nyingine.
Welcome to the club mkuu..Habari wana jamvi.
Kijana wenu nikiwa na umri wangu wa miaka 33 kamili, nimedhamiria kwa hiyari yangu mwenyewe, bila kushurutishwa wala kushawishiwa na mtu yeyote; kuacha kula kabisa vyakula vyenge wanga. Vyakula vyenye wanga kwa wingi ni kama mahindi, mpunga, mihogo, viazi, magimbi, ngano, mtama n.k
Inaaminika kisayansi vyakula hivi vikitumika kwa wingi vinasababisha sana kitambi na unene, kisukari na magonjwa ya moyo.
Juzi Jumatatu, 21.03.22 nikaanza movement yangu bila kuwa na mpango maalum. Asubuhi sikujua ntakula nini...mpaka imefika saa 5 sijala kitu. Sehemu za kula zote zina vitafunwa tulivyovizoea maandazi, chapati, vitumbua, mikate, viazi, mihogo and the likes. Ikafika saa 7 njaa inauma vibaya sana mpaka nikahisi kutetemeka mwili.
Nikajisemea cha kufia nini? Nikala zangu dona safi, nyama, maharage na spinach. Baadae nikawa nakunywa tu maji.
Sasa najiona kabisa sina plan na sielewi hii game inachezwaje. Najua humu kuna wazoefu wa haya mambo. Naomba mnisaidie wenzangu msiokula wanga ama heavy meals mnafanyaje?
Mnakula nini hasa? Na mliishindaje njaa hizi siku za mwanzo mpaka tumbo lizoee? Maana ile juzi nilihisi mpaka kizungu zungu.
Mimi napenda sana nyama iwe ya kuku, ng'ombe, mbuzi, kuku n.k. Ndio udhaifu wangu mkubwa.
Nipeni ushauri wadau. Hili ndio lengo la uzi.
Asanteni.
NB: sina ugonjwa wowote unaonizuia kula chochote.
Upo sahihiJe una sukari? Je una carbohydrate intolerance?
Kuadapt keto diet ni lazima upike, pia sio unaacha kabisa sukari, unaipunguza na kuongeza fats na proteins.
Yeah ni kweli inagharimu sio sawa na kula wangaJiandae Financialy uwe sawa sawa pia, Watumiaji wanga wengi pia Sababu kuu ni "saving" akitandika chapati na supu hapo mnakutana jioni kwenye ubwabwa. AU kama n familia Marage robo mahindi nusu,Makande haya hapa siku nzima na kesho yake chai yapo...
Ku replace wanga yakubidi kamfuko kakae vizuri maana kula mpk ushibie protini usipojipanga utalalamika mara 5 kuwa maisha n magumu,wakat ugali wa buku upo tena na mboga kama zoteeee.
Mboga ndio nzuri pia mkuuAsante mkuu. Vipi kuhusu mboga mboga?
HahhahaWe furahia maisha death is a necessary end
Ni kweli mkuu.. Na ajipange kubeba otherwise ni changamotoMaisha yetu ya kitanzania wanga ndio main dish kuanzia asubuhi mpaka jioni. Ukiacha wanga labda uwe unajipikia mwenyewe maana ni ngumu sana kupata chakula kisicho na wanga mtaani.
Uwanja wako huu. Nimekutxt toka juzi msg pending mkuuNi kweli mkuu.. Na ajipange kubeba otherwise ni changamoto
Well ni kweli, kimeisha. Nilikua obese plus plus, but kimeisha. Sema shida ni kwamba kila nikijisahau kidogo (especially on vacations) kinarudi. Na ukigain weight unanotice kabisa mwili umekua mzembemzembeBila shaka kwa ratiba hii huna kitambi. Mwenye vidonda vya tumbo hii ratiba haiwezi.
Miili ya watu inatofautiana sana. Kuna mtu anakula sana yaani huwezi kumkuta hali labda kama kalala, ila cga ajabu hana tumbo liko flat.