Ushauri: Nataka kuacha kula wanga kwa mwaka mzima

Ushauri: Nataka kuacha kula wanga kwa mwaka mzima

Upo sahihi.
Acha kula wanga, sukari, mafuta na ikitokea sasa umekula wanga jitahidi iwe mchana na kiasi kidogo.
Kula sana mbogamboga, protein, matunda.
Mie binafsi huwa nanenepa sana nikila wanga, sukari, na ma vya kula ya mafuta.
Lakini nikiacha kula hayo mavyakula napungua ninakula mcharooo na ninakuwa mwepesi sana.
Kama ujuavyo sisi wamama ndo wapishi wa familia, kwa kiasi fulani ni ngumu kucontrol mfano mchana ukiwa unalisha mtoto anataka mle wote(watoto wangu huwa wanataka tule wote, na wakiona nakula mboga mboga tu na wao eti wanagoma kula) usiku mume nae anataka mle wote au akulishe, wageni nao wakija ni noma kuanza kujieleza umewapikia eti wewe huli inabidi uzuge ule, ukienda ugenini napo changamoto maana kama mnajua sisi ni watanzania.
Changamoto ni nyingi sana kufikia malengo.

Ila all in all ni kupambana na hizo challenge, mfano sasa hivi nina mwezi wa 2 nimeacha mno kula wanga inatokea mara chache sana nikadokoa wali maharage vijiko 2, pilau kijiko 1, chapati robo(hivi vyote haizidi mara 1 kwa wiki)
Hii ni ratiba yangu.
Asubuhi nachemsha maji moto yakiwa na tangawizi, mchaichai abdalasini, kisha naweka limao.
Masaa 2 baadae nakunywa kikombe cha maziwa fresh labda mayai 2 kuchemsha, au maziwa matupu.
Mchana nakula parachichi, mchemsho wa mboga za majani, kama nikipata kitoweo iwe kuku, samaki au nyama choma au mchemsho poa(ni lazima kimojawapo nipate)
Usiku mara nyingi nakunywa mtindi, au smoothie ya mtindi&parachichi&,passion.
Mchana ukiwa kazini unewezaje kupata parachichi, mchemsho wa mboga mboga unavichemshia wapi?

Nataka nipungue kidogo, ila mazingira ya kazini najikuta ni wali na chips. Usiku nilikuwa nimeweza kula mboga mboga na matunda na maziwa ila nikaja pata dalili za amoeba, nikajua ni ma mboga.

Nimeacha kula usiku ila bado sijapungua. Mimi sio mnene nina mwili wa kawaida ila naona kama kuna ka kitambi kanakuja kwa mbali.

Kuna rafiki yangu mchana ugali anaokula mkubwa nusu sahani jion bonge la sahani ya wali, cha ajabu hana tumbo hata kidogo haya maisha.

Kufanya diet yataka moyo, najikalia zangu ndani najilia nyanya chungu parachichi na ka ugali kadogo mara shoga yangu anaingia na kitimoto, najisemea moyoni sili, mara naonja moja, mara mbili kweli yataka moyo.
 
Well ni kweli, kimeisha. Nilikua obese plus plus, but kimeisha. Sema shida ni kwamba kila nikijisahau kidogo (especially on vacations) kinarudi. Na ukigain weight unanotice kabisa mwili umekua mzembemzembe
Kwahiyo wewe hufanyi mazoezi una deal na misosi tu?
 
Ndugu dawa ya kukata kitambi ni kupunguza kula wanga tu. Kula protein kwa wingi na health fat bila kusahau mboga za majani na matunda.
Nakukubalia maoni yako.

Ila Mimi kama gym goer nakubishia.
 
Upo sahihi.
Acha kula wanga, sukari, mafuta na ikitokea sasa umekula wanga jitahidi iwe mchana na kiasi kidogo.
Kula sana mbogamboga, protein, matunda.
Mie binafsi huwa nanenepa sana nikila wanga, sukari, na ma vya kula ya mafuta.
Lakini nikiacha kula hayo mavyakula napungua ninakula mcharooo na ninakuwa mwepesi sana.
Kama ujuavyo sisi wamama ndo wapishi wa familia, kwa kiasi fulani ni ngumu kucontrol mfano mchana ukiwa unalisha mtoto anataka mle wote(watoto wangu huwa wanataka tule wote, na wakiona nakula mboga mboga tu na wao eti wanagoma kula) usiku mume nae anataka mle wote au akulishe, wageni nao wakija ni noma kuanza kujieleza umewapikia eti wewe huli inabidi uzuge ule, ukienda ugenini napo changamoto maana kama mnajua sisi ni watanzania.
Changamoto ni nyingi sana kufikia malengo.

Ila all in all ni kupambana na hizo challenge, mfano sasa hivi nina mwezi wa 2 nimeacha mno kula wanga inatokea mara chache sana nikadokoa wali maharage vijiko 2, pilau kijiko 1, chapati robo(hivi vyote haizidi mara 1 kwa wiki)
Hii ni ratiba yangu.
Asubuhi nachemsha maji moto yakiwa na tangawizi, mchaichai abdalasini, kisha naweka limao.
Masaa 2 baadae nakunywa kikombe cha maziwa fresh labda mayai 2 kuchemsha, au maziwa matupu.
Mchana nakula parachichi, mchemsho wa mboga za majani, kama nikipata kitoweo iwe kuku, samaki au nyama choma au mchemsho poa(ni lazima kimojawapo nipate)
Usiku mara nyingi nakunywa mtindi, au smoothie ya mtindi&parachichi&,passion.
Mimi kazi yangu 80% ni off office-field. Naweza pata matunda na mboga. Ishu ni namna ya kuziandaa.
Ila ni kitu kizuri sana. Ngoja niendelee hivi hivi.
 
Sio
Huwezi pungua kupitia kuacha kula peke yake.

Naona wadau wengi wanasema wameacha wanga na mwili umepungua.

Mwili unapungua kwa mawili ama ufanyiwe operation au ufanye mazoezi. Intentional starvation itabackfire na ulcers na magonjwa mengine.

Halafu mazoezi ni ishu ndogo sana. Yaani wewe unayeruka kichura chura mara tano kila siku you are better off kuliko mimi ninayekesha nacheza PS.
Sio kweli
 
Mkuu naona unachanganya kati ya watu wanaoshinda njaa, ili wapungue.

Na walioacha kula wanga haimaanishi kuwa unatakiwa kushinda njaa.

Mtu akiacha kula vyakula vya wanga kabisa lazima uzito upungue.

Kiasi cha sukari kinapungua..
Mwili utakuwa ni rahisi ku butn calories, sababu kwa kuacha wanga Energy nyingi itatoka katika vyakula vya healthy fat..na protein pamoja vitamins
So bro umeacha kula wanga ili uburn calories? Hufanyi hata zoezi la kupanda ngazi na utachoma calories?
 
Niko wiki ya nne sasa bila ya kutumia chakula chochote cha wanga. Naomba nikupatie ratiba yangu ya chakula kwa siku.
Naamka saa 11, napata maji ya uvuguvugu yaliyotiwa ndimu. Napiga pushup kidogo kisha najiandaa kwenda ofcn.
Kwa kuwa nina usafiri wangu, mrs anakuwa ananifungashia juice ya kutosha anayotengeneza mwenyewe. Juice hii inakuwa ya mchanganyiko wa matunda mbalimbali na mboga mboga kama karoti, nyanya, parachichi, embe, apple, nk. Epuka matunda yanayotoka South Africa, mengi ni GMO.
Nakunywa juice hiyo around saa 2 asb na saa 4 asb.
Saa tano napata dafu.
Saa saba napata mboga za majani na matunda kama ndizi na parachichi.
Saa tisa napata tena juice (huwa nabeba ya kutosha na nahifadhi kwenye friji ofcn.
Naweza pia kuwa na snacks kama karanga au tende
Nikirudi nyumbani saa kumi na mbili napata juice au saladi ya mchanganyiko wa matunda na mboga mboga.
Wakati mwingine hiyo inakuwa imetosha kabisa na nakuwa sihitaji kupata kitu kingine zaidi ya chai ya mchanganyiko wa viungo iliyotiwa asali.
Siku nyingine naweza kula maboga yaliyochemshwa pamoja na vitu kama njugu mawe, choroko au kunde.
By the way mimi nimeamua kupunguza sana matumizi ya nyama ili kupunguza asidi mwilini.
We have so many locally produced fruits in Tz
 
  • Thanks
Reactions: len
Kuna mtu namfahamu yeye kila siku jan to December anakula wali ,hana kitambi ana mwili mzuri tu.

Ndugu yangu jilie tu mbinguni hakuna hotel, kule ni kuimba mapambio tu.
Sasa mbingu yahusika nini na namna ya ulaji wangu? Ndio kusema naogopa kifo?
I'm a pro biker na siogopi road chaos.
 
Ofisini asubuhi natoka hime nishakunywa maji moto, maziwa na mayai, so hapo mwendo wa maji au maziwa mtindi, mchana nakula choma yoyote iwe kuku,ng'ombe au mbuzi.
Uzuri katika wiki nina siku 2 tu za kukaa ofisini japo huwa nasikia njaa sana kwa hiyo kula choma ni lazima.
Mchana ukiwa kazini unewezaje kupata parachichi, mchemsho wa mboga mboga unavichemshia wapi?

Nataka nipungue kidogo, ila mazingira ya kazini najikuta ni wali na chips. Usiku nilikuwa nimeweza kula mboga mboga na matunda na maziwa ila nikaja pata dalili za amoeba, nikajua ni ma mboga.

Nimeacha kula usiku ila bado sijapungua. Mimi sio mnene nina mwili wa kawaida ila naona kama kuna ka kitambi kanakuja kwa mbali.

Kuna rafiki yangu mchana ugali anaokula mkubwa nusu sahani jion bonge la sahani ya wali, cha ajabu hana tumbo hata kidogo haya maisha.

Kufanya diet yataka moyo, najikalia zangu ndani najilia nyanya chungu parachichi na ka ugali kadogo mara shoga yangu anaingia na kitimoto, najisemea moyoni sili, mara naonja moja, mara mbili kweli yataka moyo.
 
Welcome to the club mkuu..

Mie huu mwezi wa pili sasa... Naona naendelea vizuri tu. Huwa nabeba kila kitu asubuhi nahakikisha nina lunch na breakfast. Mie hupendelea zaidi karoti, matango, mayai ya kuchemsha, parachichi na white meat na wakati mwingine maharage kiasi etc. So ni rahisi tu wala huwezi pata njaa.
Nitajaribu na Mimi.
 
Achana nao wapuuzi tu hao.

Wazee wwtu zamani walikula sana wanga hawakuwa na maobesity na visukari vilikuwa vichche.

Wazee wetu zamani walikunywa sana miti shamba na wala figo hazikupata shida ndio maana waliishi miaka mingi sana.
Zamani ipi mkuu?
 
Hebu Lizzy tusaidie ratiba yako, Maana wewe sina mashaka kbsa na ratiba yako ya misosi Mama wa Kuonja...
Mie siunaonaga sahani yangu haikosi ugali/wali/ndizi/chapoo na ndugu zao wengine. Nnachozingatia ni kiwango tu...ambapo hainipi shida kwavile mwili ushazoea.

Ngoja na mimi ntajaribu kuondoa wanga kwenye diet yangu mwezi ujao. Ntafanya for about a week nione itakuwaje....
 
Huwezi pungua kupitia kuacha kula peke yake.

Naona wadau wengi wanasema wameacha wanga na mwili umepungua.

Mwili unapungua kwa mawili ama ufanyiwe operation au ufanye mazoezi. Intentional starvation itabackfire na ulcers na magonjwa mengine.

Halafu mazoezi ni ishu ndogo sana. Yaani wewe unayeruka kichura chura mara tano kila siku you are better off kuliko mimi ninayekesha nacheza PS.
Kuna wengine wanafanya mazoezi ya nguvu ila hawapungui na sababu ni chakula wanachokula.
 
Back
Top Bottom