Upo sahihi.
Acha kula wanga, sukari, mafuta na ikitokea sasa umekula wanga jitahidi iwe mchana na kiasi kidogo.
Kula sana mbogamboga, protein, matunda.
Mie binafsi huwa nanenepa sana nikila wanga, sukari, na ma vya kula ya mafuta.
Lakini nikiacha kula hayo mavyakula napungua ninakula mcharooo na ninakuwa mwepesi sana.
Kama ujuavyo sisi wamama ndo wapishi wa familia, kwa kiasi fulani ni ngumu kucontrol mfano mchana ukiwa unalisha mtoto anataka mle wote(watoto wangu huwa wanataka tule wote, na wakiona nakula mboga mboga tu na wao eti wanagoma kula) usiku mume nae anataka mle wote au akulishe, wageni nao wakija ni noma kuanza kujieleza umewapikia eti wewe huli inabidi uzuge ule, ukienda ugenini napo changamoto maana kama mnajua sisi ni watanzania.
Changamoto ni nyingi sana kufikia malengo.
Ila all in all ni kupambana na hizo challenge, mfano sasa hivi nina mwezi wa 2 nimeacha mno kula wanga inatokea mara chache sana nikadokoa wali maharage vijiko 2, pilau kijiko 1, chapati robo(hivi vyote haizidi mara 1 kwa wiki)
Hii ni ratiba yangu.
Asubuhi nachemsha maji moto yakiwa na tangawizi, mchaichai abdalasini, kisha naweka limao.
Masaa 2 baadae nakunywa kikombe cha maziwa fresh labda mayai 2 kuchemsha, au maziwa matupu.
Mchana nakula parachichi, mchemsho wa mboga za majani, kama nikipata kitoweo iwe kuku, samaki au nyama choma au mchemsho poa(ni lazima kimojawapo nipate)
Usiku mara nyingi nakunywa mtindi, au smoothie ya mtindi¶chichi&,passion.