Ushauri: Nataka kuacha kula wanga kwa mwaka mzima

Ushauri: Nataka kuacha kula wanga kwa mwaka mzima

No parachichi ni nzuri sana kwa mtu anaefanya diet. Good source of protein and also fiber.
Asubuhi huwa nakula nusu parachichi + mayai mawili ya kukaanga, bacon na slice moja ya brown bread nashushia na glass moja ya maziwa fresh.
Hapo nashinda siku nzima sijala kitu.
Nakunywa maji tu kwa wingi. Nimefanikiwa kupungua zaidi ya kilo ishirini + kitambi kimepotea kabisa
Bila Shaka utakuw unafanya mazoezi hiyo diet bila mazoezi kipengele
 
Niliacha kula wanga( mara mmoja mmoja nakula) nimepungua sana sana. Nakunywa capuchino asubuhi, mchana salads tofauti, nazitia Thunfisch, kuku au beef, yogurt matunda na maji mengi.
This is all I need. Kudos
 
Achana na mahindi mkuu, si unaona jinsi akili za watanzania zimekaa upande upande?
Ningekuwa na mamlaka ningezuia uuzaji wa unga wa mahindi iwe dona au sembe bila kuwa na mchanganyiko mwingine. Kuna wakat inabid uvuke mstari wa utash wa weng wajinga kuwasaidia wenyewe. Tatzo la utapiamlo mkoa wa iringa kuwa juu ni la kiufaham zaid kuliko ukosef wa nini kiliwe! Ndo mana nchi zinazohangaikia afya za akili za watu wao wako makin na ingredients za bidhaa kuliko uchu wa kodi. Hadi maji yanawekwa virutubisho vya IQ!

Unakuta mtu aba kipato lakin hajali familia inakula kwa malengo gan na bado anatumia bajet kubwa kula ovyo!
Elim ya afya na lishe ianzie chekechea mtoto ajue kila mlo anatakiwa mboga za majan nying kuliko chakula chenyewe!

Mtoto awe na kibustan chake hata kidogo, akuhudumie akitoka skuli, atajiongeza anavokua!
Mtu ana li eneo litoto halifanyag kitu had mchaichai ananunua! Wazaz wa sasa vijana kwa wazee ni wabinafs, hawatak uzao wao kujitegemea hata kifikra utadhan wanaish wakiwa wa mwisho!
 
Habari wana jamvi.

Kijana wenu nikiwa na umri wangu wa miaka 33 kamili, nimedhamiria kwa hiyari yangu mwenyewe, bila kushurutishwa wala kushawishiwa na mtu yeyote; kuacha kula kabisa vyakula vyenge wanga. Vyakula vyenye wanga kwa wingi ni kama mahindi, mpunga, mihogo, viazi, magimbi, ngano, mtama n.k
Jitahidi sana kupunguza kiwango,kama ni wali au ugali kula kidogo sana,usishibe na usiku kula matunda pekee.

Mimi nilikua na uzito 130 nikapewa maelekezo na daktali wa kazini kwetu,ndani ya miezi 2 tu nikapima uzito nikakuta ni 103,nimendelea mwezi mmoja nimekuta 96 lengo nifike 80 nisimamie hapo.

Ila sasa changa moto ni kubwa raia wana shangaa,wana niuliza kama ninaumwa au kuna taizo mbona nimepungua kwa Kasi sana nawajibu majukumu zamezidi.

Pia chai usinywe kabisa habari ya chai sahau kabisa, na soda pia. Kwa sasa najiona mwepesi naweza kutembea umbali mrefu bila kuchoka,nakula mbususu bila wasi kabisa ufanisi umeongezeka na akili Ina utulivu wa hali ya juu sana.
 
Upo sahihi.
Acha kula wanga, sukari, mafuta na ikitokea sasa umekula wanga jitahidi iwe mchana na kiasi kidogo.
Kula sana mbogamboga, protein, matunda.
Mie binafsi huwa nanenepa sana nikila wanga, sukari, na ma vya kula ya mafuta.
Lakini nikiacha kula hayo mavyakula napungua ninakula mcharooo na ninakuwa mwepesi sana.
Kama ujuavyo sisi wamama ndo wapishi wa familia, kwa kiasi fulani ni ngumu kucontrol mfano mchana ukiwa unalisha mtoto anataka mle wote(watoto wangu huwa wanataka tule wote, na wakiona nakula mboga mboga tu na wao eti wanagoma kula) usiku mume nae anataka mle wote au akulishe, wageni nao wakija ni noma kuanza kujieleza umewapikia eti wewe huli inabidi uzuge ule, ukienda ugenini napo changamoto maana kama mnajua sisi ni watanzania.
Changamoto ni nyingi sana kufikia malengo.

Ila all in all ni kupambana na hizo challenge, mfano sasa hivi nina mwezi wa 2 nimeacha mno kula wanga inatokea mara chache sana nikadokoa wali maharage vijiko 2, pilau kijiko 1, chapati robo(hivi vyote haizidi mara 1 kwa wiki)
Hii ni ratiba yangu.
Asubuhi nachemsha maji moto yakiwa na tangawizi, mchaichai abdalasini, kisha naweka limao.
Masaa 2 baadae nakunywa kikombe cha maziwa fresh labda mayai 2 kuchemsha, au maziwa matupu.
Mchana nakula parachichi, mchemsho wa mboga za majani, kama nikipata kitoweo iwe kuku, samaki au nyama choma au mchemsho poa(ni lazima kimojawapo nipate)
Usiku mara nyingi nakunywa mtindi, au smoothie ya mtindi&parachichi&,passion.
 
Niko wiki ya nne sasa bila ya kutumia chakula chochote cha wanga. Naomba nikupatie ratiba yangu ya chakula kwa siku.
Naamka saa 11, napata maji ya uvuguvugu yaliyotiwa ndimu. Napiga pushup kidogo kisha najiandaa kwenda ofcn.
Kwa kuwa nina usafiri wangu, mrs anakuwa ananifungashia juice ya kutosha anayotengeneza mwenyewe. Juice hii inakuwa ya mchanganyiko wa matunda mbalimbali na mboga mboga kama karoti, nyanya, parachichi, embe, apple, nk. Epuka matunda yanayotoka South Africa, mengi ni GMO.
Nakunywa juice hiyo around saa 2 asb na saa 4 asb.
Saa tano napata dafu.
Saa saba napata mboga za majani na matunda kama ndizi na parachichi.
Saa tisa napata tena juice (huwa nabeba ya kutosha na nahifadhi kwenye friji ofcn.
Naweza pia kuwa na snacks kama karanga au tende
Nikirudi nyumbani saa kumi na mbili napata juice au saladi ya mchanganyiko wa matunda na mboga mboga.
Wakati mwingine hiyo inakuwa imetosha kabisa na nakuwa sihitaji kupata kitu kingine zaidi ya chai ya mchanganyiko wa viungo iliyotiwa asali.
Siku nyingine naweza kula maboga yaliyochemshwa pamoja na vitu kama njugu mawe, choroko au kunde.
By the way mimi nimeamua kupunguza sana matumizi ya nyama ili kupunguza asidi mwilini.
 
Usemalo ni sahihi. Mara nyingi nakula samaki au nyama jioni na matunda. Bei ya samaki mjini hapa ni balaa. Mlo kama huo mdogo tu usioshibisha sometimes inazidi hadi elfu 5. Wakati kuna wali wa buku jero.
Japo mara nyingi mimi hula nyumbani. Lakini kwa sasa wife si mtu wa kukaa sana home. So ntakuwa naamua mwenyewe nikale wapi.
Mwenzako nilijitia naparamia GYM kufika Gym piga piga kama week hivi akaja GYM MASTER na ratiba lake la misosi,nikaona kbisa huyu mwamba ananichukulia mimi wa kishua sanaaa.

Sio kwa ratiba ile ya maprotini mjomba, Maziwa sasa nikahisi kama nakaribia kuanza kunyonya soon Nikasema ah weee niacheee GYM my Foot NIKAACHANA nayo, maana GYM huku daily ugali na ubwabwa tunadanganyana,ni kukomazana Mwili hauongezeki.

Ki ufupi kwenye hizi lifestyle maisha mengine tuyaache tu huko kwenye TV na ONLINE ila ukitaka ku act kama uonavyo kwenye TV hakikisha kibubu imejaaaa,

Tunaipenda sana miili yetu afya zetu ila ndio hivyo hali zetu za uchumi zimetupenda zaidi.
 
Hebu Lizzy tusaidie ratiba yako, Maana wewe sina mashaka kbsa na ratiba yako ya misosi Mama wa Kuonja...
 
wanauza mboga kama mboga tu hawana shida?

mimi nina changamoto hiyo,wanankatalia kuniuzia asee
Nashukuru hawa wanakubali kuniuzia mboga tu, bila wali au ugali.
Bahati mbaya sana jamii tunayoishi imekariri kuwa chakula ni wali, ugali au ndizi. Lakini inafaa watu wenye restaurant watambue kuwa mahitaji ya watu yanayofautiana. Mimi ningelifurahi kupata watu wanaotengeneza saladi tu na kuiuza hivyo hivyo
 
Hizi zinaitwa yo-yo diets sababu zipo too extreme na siyo sustainable in the long run. Bora kupunguza tu aina fulani ya virutubisho na siyo kuacha kula kabisa sababu binadamu hatujaumbwa hivyo unless wewe una uwezo wa kumuajiri personal chef nyumbani kwako kama Mo Dewji au P. Diddy. Mtu unakuwa na low energy levels mwilini kila saa unasikia njaa na kufikiria kula hata ubongo haufanyi kazi vizuri.
 
Napenda sana kuacha wanga lakini shida ipo kwwnye uchumi nilijaribu hiyo kitu nikaona ntaua familia acha niendelee tu na ugali nilichofanya ni kupunguza.
Nna kakitambi hakiishi naendelea kukilealea hata nifanye vp mazoezi shida najua ni hiyo hiyo wanga ndio mana hakiishi .
 
Jiandae Financialy uwe sawa sawa pia, Watumiaji wanga wengi pia Sababu kuu ni "saving" akitandika chapati na supu hapo mnakutana jioni kwenye ubwabwa. AU kama n familia Marage robo mahindi nusu,Makande haya hapa siku nzima na kesho yake chai yapo...

Ku replace wanga yakubidi kamfuko kakae vizuri maana kula mpk ushibie protini usipojipanga utalalamika mara 5 kuwa maisha n magumu,wakat ugali wa buku upo tena na mboga kama zoteeee.
We jamaa kama umeniona vile 😅
 
Huwezi pungua kupitia kuacha kula peke yake.

Naona wadau wengi wanasema wameacha wanga na mwili umepungua.

Mwili unapungua kwa mawili ama ufanyiwe operation au ufanye mazoezi. Intentional starvation itabackfire na ulcers na magonjwa mengine.

Halafu mazoezi ni ishu ndogo sana. Yaani wewe unayeruka kichura chura mara tano kila siku you are better off kuliko mimi ninayekesha nacheza PS.
 
Back
Top Bottom