Ushauri: Nataka kuacha kula wanga kwa mwaka mzima

Ushauri: Nataka kuacha kula wanga kwa mwaka mzima

kitakacho kudhuru sio wanga ni mafuta wanayopikia mitaani ni yapi?na yamepikiwa mara ngapi ? na rangi yake ikoje ? wengi watu huumia bila kujijua wanapokula nje.huwezi kuepuka kula chakula cha wanga kula ila punguza. mchele uoshe pia pikia maji mengi kisha ikichemka mwaga maji itakuwa umeiondoa wanga
Wanga na sukari zama zetu tunavila kupindukia na kupelekea miili kuhifadhi extra sugars as fats..na hii hupelekea kunenepa au mafutq kujaa kwenye internal organs. Hii hupelekea chronic inflammation ambayo huleta magonjwa mengi ya mtindo wa maisha.
 
Uko sawa...sukari ni sukari. Na mechanism ya digestion yake ni ile ile...iwe ya kiwandani au ya tunda sukari ni sukari na effect yake kwenye mwili ni the same.

Kuna mkanganyiko hapa ,tusubiri wataalamu wafafanue, lakini haingii akilini kulinganisha sukari ya kiwandani na inayopatikana kwenye matunda

Kwahiyo umehitimishaje hapo mkuu au point ni ipi? Maana nilichokuwa nasema mimi ni kwamba mwili hauwezi kubainisha ya kwamba hii ni sukari ya asili(matunda,asali n.k) na hii ni sukari ya kiwandani.
 
Yes inaweza. Kitambi ni fat deposits tu. So when your body starts metabolising energy from fats instead of carbohydrates automatically mafuta yote yanaunguzwa. Lakini ujue kwamba hiki sio kitu cha kuona matokeo ndani ya wiki moja. Consistency is the key kwenye this issue
Upo sahihi 100%
 
United States wanaongoza kulima mahindi karibu acres 90+M wanalima tu mahindi lakin ugali unaongoza kuliwa sana huko usukumani hamna hata maeneo ya kulima hayo mahindi ndo ujue kuwa ugali siyo kitu kizuri
Ugali unga wa mahindi una;

-Carbohydrate
-Vitamin B
-Iron
-Fat
-Unga wa mahindi una protein 12% , ngano 14%
-mahindi ya njano Yana vitamin C & A nyingi kuliko ngano.
-Mahindi Yana kiwango sawa Cha vitamin E & K na ngano.

Nutritions zinazo patikana kwenye unga hazitofautiani Sana na za kwenye mchela na ngano.

Hao waamereka ugali sio utamaduni wao kula ,lakini wanayatumia mahindi kutengeneza popcorn Sasa sijui anayekula ugali na huyo anetafuna popcorn wanatofauti gani.

Wewe kula ugali ndio chakula chako ,Cha muhimu ni kupangilia mboga nzuri na zenye nutritions
 
wana jamvi.

Kijana wenu nikiwa na umri wangu wa miaka 33 kamili, nimedhamiria kwa hiyari yangu mwenyewe, bila kushurutishwa wala kushawishiwa na mtu yeyote; kuacha kula kabisa vyakula vyenge wanga. Vyakula vyenye wanga kwa wingi ni kama mahindi, mpunga, mihogo, viazi, magimbi, ngano, mtama n.k

Inaaminika kisayansi vyakula hivi vikitumika kwa wingi vinasababisha sana kitambi na unene, kisukari na magonjwa ya moyo.

Juzi Jumatatu, 21.03.22 nikaanza movement yangu bila kuwa na mpango maalum. Asubuhi sikujua ntakula nini...mpaka imefika saa 5 sijala kitu. Sehemu za kula zote zina vitafunwa tulivyovizoea maandazi, chapati, vitumbua, mikate, viazi, mihogo and the likes. Ikafika saa 7 njaa inauma vibaya sana mpaka nikahisi kutetemeka mwili.

Nikajisemea cha kufia nini? Nikala zangu dona safi, nyama, maharage na spinach. Baadae nikawa nakunywa tu maji.

Sasa najiona kabisa sina plan na sielewi hii game inachezwaje. Najua humu kuna wazoefu wa haya mambo. Naomba mnisaidie wenzangu msiokula wanga ama heavy meals mnafanyaje?

Mnakula nini hasa? Na mliishindaje njaa hizi siku za mwanzo mpaka tumbo lizoee? Maana ile juzi nilihisi mpaka kizungu zungu.
Mimi napenda sana nyama iwe ya kuku, ng'ombe, mbuzi, kuku n.k. Ndio udhaifu wangu mkubwa.

Nipeni ushauri wadau. Hili ndio lengo la uzi.
Asanteni.
NB: sina ugonjwa wowote unaonizuia kula chochote.
Tafuta pesa utaona mambo
 
sijapitia comments zote kujua kama umesaidika ama la, Ila msome mtu anaitwa DR. Boaz Mkumbo ( md ) facebook na instagram anatoa ushauri mzuri sana na namna ya kupangilia sahani yako.
 
Asanteni nyote kwa michango yenu. Nimejifunza kitu na pia wengine wamejifunza.
Mungu awabariki sana.
 
Kuna mkanganyiko hapa ,tusubiri wataalamu wafafanue, lakini haingii akilini kulinganisha sukari ya kiwandani na inayopatikana kwenye matunda
Mkanganyiko upi? Nijuavyo kuna aina kuu tatu tu za sukari kwahiyo unatakiwa ujue ni aina gani ya chakula na kuna sukari gani ndani yake iwe kwenye matunda au kutoka kiwandani.
 
Kila la kheri.. usisahau mazoez kidogo na pia consistency. Fanya hata miez 6 uone changes ztakavokua. Pia dont be too strict with yourself, mara moja moja sana usisahau kuenjoy maisha
Sure boss
 
Habari wana jamvi.

Kijana wenu nikiwa na umri wangu wa miaka 33 kamili, nimedhamiria kwa hiyari yangu mwenyewe, bila kushurutishwa wala kushawishiwa na mtu yeyote; kuacha kula kabisa vyakula vyenge wanga. Vyakula vyenye wanga kwa wingi ni kama mahindi, mpunga, mihogo, viazi, magimbi, ngano, mtama n.k

Inaaminika kisayansi vyakula hivi vikitumika kwa wingi vinasababisha sana kitambi na unene, kisukari na magonjwa ya moyo.

Juzi Jumatatu, 21.03.22 nikaanza movement yangu bila kuwa na mpango maalum. Asubuhi sikujua ntakula nini...mpaka imefika saa 5 sijala kitu. Sehemu za kula zote zina vitafunwa tulivyovizoea maandazi, chapati, vitumbua, mikate, viazi, mihogo and the likes. Ikafika saa 7 njaa inauma vibaya sana mpaka nikahisi kutetemeka mwili.

Nikajisemea cha kufia nini? Nikala zangu dona safi, nyama, maharage na spinach. Baadae nikawa nakunywa tu maji.

Sasa najiona kabisa sina plan na sielewi hii game inachezwaje. Najua humu kuna wazoefu wa haya mambo. Naomba mnisaidie wenzangu msiokula wanga ama heavy meals mnafanyaje?

Mnakula nini hasa? Na mliishindaje njaa hizi siku za mwanzo mpaka tumbo lizoee? Maana ile juzi nilihisi mpaka kizungu zungu.
Mimi napenda sana nyama iwe ya kuku, ng'ombe, mbuzi, kuku n.k. Ndio udhaifu wangu mkubwa.

Nipeni ushauri wadau. Hili ndio lengo la uzi.
Asanteni.
NB: sina ugonjwa wowote unaonizuia kula chochote.
Aisee we jamaa niongeze nguvu tuwe wawili labda tutaweza maana peke yako Hilo zoezi utashindwa
 
Back
Top Bottom