Ushauri: Nataka kuanza kula nyama ya kenge

Kenge analiwa kuna jamaa flani tulikuwa nao kitaa walikuwa wana wala sana....wana mafuta na wamenona kama kuku kama ni mgeni huwezi kutofautisha kati ya nyama ya kuku na kenge...we kula tu tena unamchoma fresh.
Kuna mpemba mmoja alikuwa mwanajeshi alikuwa ana wala sana...jamaa walikuwa wanawawinda sana...wana wasaka mpaka kwenye vichaka wakiona kenge kakimbilia shimoni mtu anaingiza mkono na anamchomoa mzima mzima yaani walikuwa wanawachululia kama kuku tu.
Jina maarufu walikuwa wanawaita "Salasa"
Hiyo mitaa unaweza kukatiza mtaani unakutana na dogo kabeba kenge mzima au wako wanamchuna.
Madogo walikuwa wanatoroka shule wanaenda kuwinda kenge...wakiwakamata wanawapika wanakula na ugali mkubwa sana kisha wanashushia na Widi...sikuwahi kuona mtu amedhurika kwa kula Salasa.
WE ANZA KUWALA HIYO NI MBOGA MKUU.
 
aiseee hahhahaaaaa Daaaa Nimecheka Sana!
 
Hilo jina sio "Kuku makucha"
Nafikiri ni hilo.. Kuna siku niliona kikundi kipo bize wanapiga kitu nikajongea na nilidhan wanaua nyoka namimi nikapige nafika ani nimekuta bonge la kenge.. Ule ubize wao ungedhani wanua nyoka mla kuku.

KichWa bOX
 
Nyama ya kenge ina mafuta.mengi sana usitumie moto mwingi kuichoma.

inataka kuendana na ya kiboko
 
Kuku mach
Kuku makucha
 
Nyama ya mamba inaliwa na inauzwa ghali Sana kg 1 ni 30,000/= pale kibaha kwa mzungu Sasa mamba na kenge ni ndugu je Kuna tatizo naomba ushauri.

Naishi pembeni ya mto Kuna kenge wengi Sana.
Kwani ulipoanza kula mamba napo uliomba ushauri?
 
Kenge hakimbiagi mvua anakimbiaga radi, kenge na radi haviivi lazima radi imlipue.
 
Hahaa!! Hiyo ndo tunatafsiri wanakimbia mvua kuogopa kuloa wanaingia mtoni
Ila mimi walikuwa wananitesa machungani hao! anamfunga mbuzi mzazi miguu ya nyuma kwa mkia wake alafu anakausha maziwa yooooote, jioni nikirudisha kundi nyumbani ndama wa mbuzi wanakosa maziwa, inabidi niwanyweshe maziwa ya ng'ombe kwa chupa ya mtoto. Ila ngozi za kenge mali kweli kweli.
 
Haujawahi kuwaza kuanza kuwala nawe!
 
sijawahi kula kenge ila niliwahi kuona anachunwa kwa ajili ya kuvunwa mafuta yake alikuwa amenona kinoma
Mafuta ya kenge ni dawa nzuri sana ya masikio kama ukiua kenge nyumbani kwako usimtupe Chuna toa mafuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…