mbilitanotano
Member
- Mar 8, 2022
- 61
- 32
- Thread starter
- #41
Vipi, Milioni kumi wanatoa ?Inategemea na mtaji mnaotaka ni kiasi gani,
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vipi, Milioni kumi wanatoa ?Inategemea na mtaji mnaotaka ni kiasi gani,
Unapata mkuu, tena kwa halmashauri za dar unapata hata 50mVipi, Milioni kumi wanatoa ?
Ahaaah, kama kweli wanatoa hiyo ni vyema kupambana ili kuipata.Unapata mkuu, tena kwa halmashauri za dar unapata hata 50m
Jitahidi uwahi maana ukichelewa ni mpaka mwezi wa 3 tenaAhaaah, kama kweli wanatoa hiyo ni vyema kupambana ili kuipata.
Nashukuru kwa ushauri wako uwe hodari ila naogopa Kuoa, watoto (Kama Mungu atajalia wakapatikana) wasije kuishi maisha magumu sana. Mimi mwenyewe naishi kwa shida sana na niko peke yangu, sasa nikioa mtoto wa watu mmmmmh na dada yupi huyo anayetaka shida ? ngoja tuu niwe mpole.
Tatizo ni moja kwanza moyo wako bado haujui unataka nin.Wakubwa kwangu shikamoni, wadogo kwangu habari zenu ?
Hongereni kwa majukumu na afya njema, poleni mnaoumwa Mungu akawajaalie mpone.
Ndugu, Nilizaliwa miaka 31 iliyopita. nilipenda sana kuwa mwanajeshi wa jeshi la wananchi, sikufanikiwa kutokana na umri wangu kupita ule unaotakiwa, kukosa fani zinazotakiwa huko, na kutokuwa na mtu wa kunishika mkono kuingia huko. Nina shahada ya sayansi.
Kuna mahala serikalini nimejitolea kwa miaka minne sasa, walivyotoa ajira kupitia utumishi nimebwagwa kwenye usahili nikashindwa ! wakaajiriwa vijana wengine ambao hawakuwa wakijitolea pale. Nimefanya saili nyingi za kuomba kazi utumishi na kwingineko lakini sijafanikiwa kupata kazi.
Hapo Kibaruani wanatoa sh. 15000 kwa siku mtu atakayofanya kazi, (300,000 na kidogo kwa mwezi maana ijumaa pili hatufanyi kazi) hicho kiasi cha fedha kwa mkoa wa Dar es salaam kinaishia kulipa kodi, nauli za kwenda kibaruani, kununua umeme, kula kwa mama ntilie (2000 msosi mmoja), kulipia taka, kulipia ulinzi mtaani, sadaka kanisani, VOCHA na matumizi mengine; sijafanikiwa kuweza kuweka akiba. Sina mchumba, mke wala mtoto maana sina hela za kuniwezesha kuwahudumia, Ukinunua napo magonjwa lukuki .... ila homoni za mwili zenyewe zinafanya kazi yake hazielewi hali yako kiuchumi kwa hiyo ni shida tupu.
Huwa ninatamani sana kwenda jeshini lakini umri, fani na konekisheni ni changamoto
Ninatamani kuoa lakini sina kazi, nikifikiria kurudi kijijini kulima, sawa lakini mtaji wa kulimia na mashamba sina. Nafikiria kusoma 'post graduate diploma in education' ili niwe na taaluma ya ualimu badae niombe kazi serikalini kama mwalimu wa fizikia n.k lakini hela ya kulipia ada (milioni mbili) sina. Huwa ninapenda pia kufanya biashara ya stationery lakini mtaji nao sina !
Ninawaza kurudi chuo kusoma kozi za afya kwa diploma, ada sina ! Nipo njia panda ndugu ninaombeni mnishauri nifanyeje ili kupata hela, niache kujitolea niende chuoni kusoma, niajiriwe serikalini au taasisi binafsi au nifanye miradi hiyo, n.k maisha mengine yaendelee.
Ninatanguliza shukrani kwa ushauri wenu, ninawatakia mda mwema.
SawaJitahidi uwahi maana ukichelewa ni mpaka mwezi wa 3 tena
Kijijini.Mkuu umekulia mazingira ya kijijini au mjini?
Wanasema narrow your meditationNdugu unavitu vingi, unataka kuvifanya wakati mmoja. Chagua kimoja kifanyie kazi
Ndio maana ni talanta yangu. Mwenyezi Mungu amempatia kila mtu talanta yake hapa duniani, kuna uimbaji mziki wa kidunia, uimbaji nyimbo za injili, uimbaji kaswida, kuna madaktari, wakulima, boda boda madereva, walimu, makuli, mafundi umeme n.k mimi ninapenda kusoma.Yani mpaka dunia ya leo unawaza kusoma
Ninataka nipate hela ya kutosha kufanyia biashara au kufanya mambo hayo mengine. Namna ya kupata kiasi kingine cha fedha ndio nipo njia panda sasa. Kitu cha kufanya siyo shida, shida ni jinsi ya kupata hela ya kukifanyia hicho kituTatizo ni moja kwanza moyo wako bado haujui unataka nin.
Ukiona nyeupe unataka, nyeusi unataka, blue unataka.
Kuacha unajitolea na unapata hata hyo elf kumi na tano wenzio wanajitolea hawapati senti.
Ukijua unataka nin tofauti na hicho kias kidg Cha pesa utajua jinsi au namna gani ya kutengeza pesa nyingine ndogo ndogo nje na hyo sehem ya kujitolea au fursa nyingine hapo hapo kweny hyo ofis unayojitolea.
Gharama za maisha haziko hivyo ndugu. Ziko juu sana, kwa huu mpangilio wa matumizi siwezi kuishi hili eneo. Ningependa niweke akiba lakini ni ngumu.Any way kwa miaka uliyo nayo alafu unalia lia hapa as if huna kipato that is nonesense.
wewe unataka kusema unashindwa kabisa kufikiri utasave vipi 300k, weka 100K assume unalipwa 200K then ndiyo iwe kwenye matumizi iyo 200K.
200K imagine unalipa kodi plus maji na umeme 50K covered, inasalia 150K.
Assume unatumia 100K kila mwezi kwenye food. 50K iliyobaki ni mavazi na sabuni kwa kila mwezi.
Plan kuinvest 100K kwenye issues nyingine.
Unapata alafu unasema hupati.....😅😅
Sasa mkuu wewe acha kazi uone ilivo kazi kupata kazi, acha kazi ukiwa na plans, mkuu wewe pambana sana, maisha siyo marahisi kiivo.Gharama za maisha haziko hivyo ndugu. Ziko juu sana, kwa huu mpangilio wa matumizi siwezi kuishi hili eneo. Ningependa niweke akiba lakini ni ngumu.
Pesa haiji kimazingara.Ninataka nipate hela ya kutosha kufanyia biashara au kufanya mambo hayo mengine. Namna ya kupata kiasi kingine cha fedha ndio nipo njia panda sasa. Kitu cha kufanya siyo shida, shida ni jinsi ya kupata hela ya kukifanyia hicho kitu