Ushauri: Nifanyeje juu ya hali hii ya maisha yangu?

Omba tu usiugue, 15k kwa siku, ukiwa na nidhamu ya pesa utatoboa. Zamani nikiwa kijana, ugali ukibaki ni mkate wa asubuhi, kande zikichacha naweka maziwa mtindi kuondoa harufu ya kuchacha. Ila swala la wanawake nilikuwa nasikia tu kwenye Bomba, mpaka nikaitwa hanisi na sikujali. Kumbuka tu mchumia juani hulia kivulini.
 
Mkuu mbilitanotano umefanya la maana kushea humu hio scenario yako. Hata mimi pia napitia same situation kama ya kwako. Nadhani tunaweza wasiliana tuone tunafanyaje kukabiliana na hali ila tu kwa ushauri kidogo mkuu ondoa kabisa mentality ya kuomba ushauri wa kukabiliana na maisha yako mwenyewe mtandaoni.

Hapo tu ndio umekosea mkuu. Wewe ni msomi so act kisomi walau. Usikubali kuanika life yako halafu then una anza kushauriwa na sample ya watu wengine hata kujishauri wao hawawezi lakini humu watajifanya wanakushauri wewe, some of them hawawezi hata kuandika vizuri lakini humu ndio watakucheka kuwa wewe ni looser😂...

Be smart mkuu. Maisha yako yatafakari mwenyewe tena Room ukiwa umejifungia pasi na kelele yoyote utapata Jibu sahihi la kufanya. Ikishindikana hapo unamfata mtu unae mtrust zaidi kwenye maisha yako, kazini au hata jirani yako ndio unamueleza ili naye akupe mtazamo wake. Hatimaye unapata solution ni nini ufanye then you go for it.
 
USHAURI WAKO NI MWIBA,TENA UNACHOMA.WEWE ENDELEA KUJIFUNGIA HALAFU MADHARA YAKE UTAYAONA.
 
USHAURI WAKO NI MWIBA,TENA UNACHOMA.WEWE ENDELEA KUJIFUNGIA HALAFU MADHARA YAKE UTAYAONA.
Mkuu ni Suala la Perception tu ikiwa kama na wewe una mawazo kama ya mleta mada it's OK. Kila mtu yuko huru kuwa na mtazamo wake.
 
Hakuna maisha rahisi Tanzania ndugu yangu kwa sasa,watu wanabebana

Nakushauri oa hiyo laki tatu inatosha

Chagua mwanamke mwenye kujua maisha mkapange uswekeni na yeye mpe nradi wa kupika vitumbua awe anauza nyumbani apo
Kidogo kidogo utaona
ila homoni za mwili zenyewe zinafanya kazi yake hazielewi hali yako kiuchumi kwa hiyo ni shida tupu.
To yeye
mtaalamu kuna tatizo huku. Njoo kwa haraka kuna mtu yuko kwenye harakati za kujitoanuhai au aende bushi kulima au asioe au asome basi ni tafrani
 
Ondoka hapo ulipo nenda shule ya Inspire Kibaha kwa Mzee Bizulu kaombe kifundisha physics.Akikuelewa ujw kunishukuru.
 
Yaani hata kukusaidia nashindwa kwa sababu umeonesha udhaifu mkubwa sana na kuwaza yasiyowazika

Umekazana jeshi jeshi kama umri umeenda acha kuwaza tena ila kama unapenda sana na lazima uwe jeshini zipo nchi nyingi unaweza kuajiriwa au voluntarily

Kuhusu kuoa hapo napo unatuangusha tusiowaza kesho itakuwaje maana anaepanga sio mimi wala wewe

Oa tu na riziki anatoa Maanani huenda huyo mke ndio akawa wa kukuongoza na akaja na bahati yake
Tena ukipata mtoto ndio kabisa na riziki inakuja kwa kila kiumbe

Acha kuwaza hayo ya nani ataweka msosi kinywani

Pambana mpaka kieleweke
Nilioa bado mdogo sana ila sijutii wewe una over 30 unalalamika
 
Wewe muoga wa maisha,tuna miliki vitu vingi alafu hata hatuna vyeti
 
Asante kwa Ushauri Battor
 
Bora umekumbuka kuugua kupo, japo kuna na mambo mengine mengi yanatokea na ni ya kutumia hicho hicho kiasi kidogo cha pesa ambacho mtu anapata.
 
Pamoja sana Hardbody asante kwa ushauri wako. Nimeleta humu maana huwa nawaza mpaka kichwa kinataka kuungua kwa mawazo nikiwa mwenyewe chumbani, marafiki nilio nao huwa tunashauriana pia. Ninaamini humu kuna watu ni wasomi, tena wanye hekima sana japo kuna wengine pia sio wasomi, hawana hekima ya kushauri mtu, na wana mambo mengine ambayo siyo mazuri. Hao ndugu ninaofanya nao kazi ni wanafiki tuu, sasa mimi sina urafiki na hata mmojawapo maana huwa sina urafiki na watu wanafiki. Ni salamu tuu na kazi, ikiisha kwaheri. Kwanza ukipata matatizo ndio mwenzio anafurahia, ukifanikiwa japo kidogo mwenzio roho inamuuma kwa hiyo bora hata mwingine anaweza kukushauri ila siyo hao wa kufanya nao kazi. Huu ushauri naopata humu mwingine uko vizuri sana, napata kitu flani cha kunijenga akili na kuniipa mawazo chanya. Kaka huu utambulisho usio halisi unaficha mengi, najua humu kuna maprofesa, madaktari, watumishi wa Mungu, wasiosoma, wasomi, wezi, vibaka, madereva, wakulima, wachawi n.k. Shukrani sana ndugu.
 
If you'd had studied law ,ningekupa nafasi at my law firm ,Ila pole Sana kwa mapito yako ,in life seek chances usingoje zikufuate , case inpoint Kuna boda anayenifanyia delivery hapa dar alikuja mpaka ofisini kuomba apewe kazi za delivery ,wiki ya kwanza alifukuzwa na secretary na mlinzi ,Ila hakuvunjika moyo ,alinitime one day akaomba, jamaa hata kwa siku kulingana naye aliniambia hakosi laki na kitu juu ,ofisi zingine these days zampa kazi huyu bingwa ....ukingoja ajira afrika hii utakufa maskini ,Toka nje tafuta niche` ,jitume ,all the best my freind
 
Mkuu hujasema umesomea nini ili mtu ajue pa kuanzia.
 
Unalalamika kipato Tsh 300,000 akitoshi na bado unatoa Sadaka, una matatizo mahali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…