USHAURI: Nini cha kufanya kama mwenza wako alikuficha kuwa ana mtoto, Ukaja kujua baada ya miaka zaidi ya 10 baadaye?

Daah leo ndio nimekuelewa...tukio kama hilo unaweza kuliita privacy?

Je ulizaa kabla ya ndo?
Sio kwa utetezi huu wenye ukakasi kiasi hiki
 
Excellent kabisa haya ndio maamuzi ya Mwanaume rijali, hakika hapa ndio tunaona tofauti kati ya waliotahiriwa hospital na waliotahiriwa porini.
 
Tupe uzoefu wako kama umekutana na kesi kama hio mliisolve kivipi.
Tupe madini.
 
Mume bwege huyo ana nyimbo yake kabisa apigwe mawe auawe
 
Huyo ni Mwanaume suruali, halijui jando, hajafudishwa chochote kuhusu ndoa walizoana zoana tu wakaapa basi,

Hakuna jambo kubwa la kuachana hapo unless alikua amemchoka ndio kapata sababu.
Tusijaribu kuhalalisha matakwa/uelewa wetu kuwa uhalisia wa kila mtu.

Huwezi kumuita mtu mwanaume suruali ikiwa kwa kipindi cha miaka 15 ameishi kwa kudanganywa, kuaminishwa kuwa yeye ndie baba watoto wa kwanza kwa mkewe halafu ghafla anaibuka kiumbe na kusemekana ni mtoto wa mkewe.

Haya ni maisha halisi sio tamthilia za Kikorea.

Usaliti katika ndoa sio lazima umvulie mtu mwingine nguo, kitendo cha kuficha jambo ambalo kujulikana kwake kunaweza kuwa na athari katika mahusiano; huo ni usaliti tosha.
 
Mimi nashauri kwa mwanamke kama mumeo anasimamia majukumu yake vizuri bila shida yoyote ukiletewa mtoto pokea. Ila kwa Mwanaume mkeo akijifungua mtoto sio wa kwako achana nae. Hakuna heshima hapo na ukiangalia wanaume tunapitia changamoto kubwa sana kwenye utafutaji. Yaani mtu unatumia hela zako kwake halafu anakupa shida. Ni sawa sawa mtu atumie hela zake anazotafuta kwa tabu na shida kununua matatizo.
 
Daah leo ndio nimekuelewa...tukio kama hilo unaweza kuliita privacy?

Je ulizaa kabla ya ndo?
Sio kwa utetezi huu wenye ukakasi kiasi hiki
Umekosa hoja unakimbilia personal attack, lol kama hujala nenda kale kwanza hii mada ni kubwa sana kwako sio kila kitu cha kuchangia,

Btw, Nimezaa nikiwa kwenye Ndoa, watoto watano (mapacha mara mbili na mmoja) wote kwa baba mmoja, nipo kwenye ndoa mwaka wa 11 huu, tunaposhauri masuala ya ndoa hatushauri kwa mihemko na hasira bali kwa kujenga kwani Ndoa ya halali ikivunjika ni dhambi kubwa sana pia tunawafikiria na watoto ambao hata hatujui ni umri gani,

Narudia tena, kula ushibe hii mada kwako ni kubwa sana ukizingatia hata ndoa huijui.
 
Umeishi na mtu kwa miaka 15, mmezaa watoto 4, unakuja kumuacha kisa hakukwambia kua aliwahi kuzaa kabla!!?

Ukisikia kutafutiana sababu ndio huko sasa.
Da. Inaonekana wewe pengine umeshawahi kufanya hivi. Hili ni doa kubwa sana kama hujui.
 
Watakuwa wanaendelea na mahusiano still.
Huyo mume ni msaliti tuu.

Haya mambo watu wanachukulia simple sana.
 
Mume wake anasemaje??
 
Wengine nao, hata mada hajaielewa maskini anaweka kachumbari na maharage,

Nacheka kama mazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…