USHAURI: Nini cha kufanya kama mwenza wako alikuficha kuwa ana mtoto, Ukaja kujua baada ya miaka zaidi ya 10 baadaye?

USHAURI: Nini cha kufanya kama mwenza wako alikuficha kuwa ana mtoto, Ukaja kujua baada ya miaka zaidi ya 10 baadaye?

Unaona ni kosa dogo?
Kosa sio tu kuzaa, kosa kubwa ni uwazi.

Hili jambo hufufua mambo mengi.

Huenda kuna nyakati alikuwa akiomba ruhusa asafiri aende mahali akidanganya kwa ndg....jamaa anakuja kuunga dots anagundua huenda alikuwa anaenda onana na mume wa awali.

Jambo moja hufufua mengi uliyoyasamehe....waza vizuri usikomenti kirahisi kama hujui umuhimu la hili
Una hoja. Kuficha kunaweza kuwa na sababu nyingi.
 
Mtoto anamika 20 yupo chuo.
Ni wakiume.
Atakuelewa kweli kama Baba wa kufikia?????
Inategemeana na approach yako kama Mzazi.

Binafsi ningeweza, mosi ilikuwa kumfanya kuwa huru nawe na akuzoee kama Baba yake

Pili kumjali na kumuhudumia kama Baba yake Mzazi

Then atakuheshimu na kukupa thamani ile ile kama Baba yake Mzazi
 
Habari wana JF.

Kuna Ndoa imevunjika hapa ndoa ya miaka 15.

Mke alizaa kabla ya ndoa, sasa mama huyu alimficha mtoto,

Huyu mtoto alikuwa anaishi na Baba yake.

Mume alijua kwa mawasiliano ya simu.

Mama alipokuwa anaongea na mwanae.

Na mtoto anaumri wa miaka 20.

Mume wa ndoa kazaa nae watoto 4.

Dawati la suruhisho walijaribu kuweka sawa ili wasiachana ila ilishindika. Hata wachungaji walishauri kuwa asamee tuu kwani hata mtoto kashakuwa mkubwa hakuna shida yoyote lkn ndo hivyo ndoa imevunjwa jana na mahakama.

Huyu mama alizaa kipindi anaumri wa miaka 21.

Sasa wanajamii hivi vitu vinatokana na nini mpk mmoja anaamua kuficha mtoto?

NI NINI CHA KUFANYA BAADA YA KUJUA HATA KWA MUME KAMA ALIFICHA KUWA ALIKUWA ANAMTOTO.
Kuficha mtoto ni ushamba.Waachane tu...
 
Alafu kuna kisa kimoja kimemtokea mwenzetu wa ofisini kimenishangaza kwa alivyo react ila nikasema acha nije nishirikishe na wanajamvi huku.

Huyu dada kakaa kwenye ndoa kama miaka mitatu hivi. Sasa anakuja kugundua mume wake aliwahi kuchepuka na ex wake tena sio mara moja kipindi wapo kwenye mahusiano. Yaani kabla ya ndoa. Yani wame date miaka saba, mwaka wa nne mwanaume akawa na mahusiano na ex wake wameenda kama miaka miwili na ex malavidavi kama yote ila huyu dada anasema hakuwahi kuhisi. Sasa mke mtu kaja kujua wakati wameshaoana. Anasema ye bado kinamuuma kwasababu alimuamini sana mme wake inakuwaje alimsaliti kipindi ambacho alimpenda na kumuamini.

Wengi tukamshauri aache yaliyopita wagange yajayo. Akauliza ingekua nyinyi mngesahau na kusamehe? Nikasema wanajamvi mpo kibao mna majibu em mshaurini na nyinyi.
Hapo inategemea kama mume wake hasimamiii majukumu yote ya nyumbani kifedha basi mwanamke waachane nae alale mbele. Lakini kama mwanaume anasimamia almost 90 percent ya majukumu abaki maana akiachana naye atakuwa anadanga.
 
Umekosa hoja unakimbilia personal attack, lol kama hujala nenda kale kwanza hii mada ni kubwa sana kwako sio kila kitu cha kuchangia,

Btw, Nimezaa nikiwa kwenye Ndoa, watoto watano (mapacha mara mbili na mmoja) wote kwa baba mmoja, nipo kwenye ndoa mwaka wa 11 huu, tunaposhauri masuala ya ndoa hatushauri kwa mihemko na hasira bali kwa kujenga kwani Ndoa ya halali ikivunjika ni dhambi kubwa sana pia tunawafikiria na watoto ambao hata hatujui ni umri gani,

Narudia tena, kula ushibe hii mada kwako ni kubwa sana ukizingatia hata ndoa huijui.
Sasa madam ikitokea ishu kama mwanaume unamshauri nini???
 
Shangaa na wewe, mijanaume ya Kiafrika hua ni mibinafsi sanaaa, hii habari ingekua ni mwanaume ndie kaleta mtoto na Mwanamke ndie kataka talaka ungeona vile wanamshambulia Mwanamke na kumuita majina yote ya ajabu,

Mambo ya mtu na mtoto wake wao wanaguswa na nini eti kwanini kanificha kwani aliwahi kuulizwa?
Unatetea upuuzi.
 
Hapo inategemea kama mume wake hasimamiii majukumu yote ya nyumbani kifedha basi mwanamke waachane nae alale mbele. Lakini kama mwanaume anasimamia almost 90 percent ya majukumu abaki maana akiachana naye atakuwa anadanga.
Mkuu una hoja. Ila kwa unavyoona mwanaume alizingua? Si tulimshauri akaushe ila ni kama haelewi
 
Sasa madam ikitokea ishu kama mwanaume unamshauri nini???
Mtoto ni mkubwa yupo chuo sidhani kama amekuja kusomeshwa au kupewa hifadhi yeye alitaka kumjua au kumuona mama ake, basi maisha yaendelee kama yalivyokua zamani, mtoto akiwa likizo ruksa kuja pale kumuona mama ake na ndugu zake, Mumewe asijiingize kwenye malezi ya aina yoyote ukizingatia Baba mtu yupo na amemlea miaka yote.....
 
Hahahaha ndio tunasema Wanaume wa Kiafrica ubinafsi mwingi, Mwanaume kusaliti hadi kuzaa nje ya ndoa ni sawa tu, mke hatakiwi kureact kisa akiachwa atadanga, ndio maana Wanaume mnakufa mapema sana, unaishi na mtu unadhani haumii unayomfanyia kumbe anakukorogea sumu ikuue taratiiiiiibu.
 
Mtoto ni mkubwa yupo chuo sidhani kama amekuja kusomeshwa au kupewa hifadhi yeye alitaka kumjua au kumuona mama ake, basi maisha yaendelee kama yalivyokua zamani, mtoto akiwa likizo ruksa kuja pale kumuona mama ake na ndugu zake, Mumewe asijiingize kwenye malezi ya aina yoyote ukizingatia Baba mtu yupo na amemlea miaka yote.....
Hahahahaha,unajitahidi inaoneshaa jinsi gani UMEGUSWA NA HILI ,ila bi mdada we unajibu kwa upande wako, walio wengi humu ni WANAUME na umeona MAJIBU yao ,tuko SAWA na mwamba huyo ...

Kikubwa kubali mwenzako kachemka mambo yenu ya SIRI yasizidi sana
 
Back
Top Bottom