Ushauri: Nitumie mbinu gani kuongea na baba aachane na mchepuko wake?

sepema mtafte mzee ongea nae kistaarabu...mwambie unajua anamchepuko ...

basi achepuke kwa akili asimkere bi mkubwa, kama vp bi mkubwa akipata tatizo lawama zitamwangukia yeye
Asante kwa Ushauri.Kila anaenishaur naona anamsaada mzuri.Changamoto ni wadau kutofautiana msimamo.Wengine wanashaur niongee na mzee huku wengine wakisema nisithubutu.
 
Huu ni mfano bora sana; mambo ya mahusiano hasa ya wazazi wako ni ya kuyakalia mbali sana.

Mimi binafsi baada ya kuona memnhi duniani; huwa siingilii wala kutoa ushauri kwa mahusiano ya mtu yoyote yule.

Kuna visa na ugomvi wa mambo ya ajabu sana kwenye mahusiano.
 
Hili lakuhonga pia lipo mkuu.Unaambiwa kun wakat mzee anachota mchele,maharage,na unga anampa huyo mchepuko Yaani maza wangu kakasirishwa na mengi
 
Pole sana mkuu. Mimi nitakupa experience yangu nilichofanya. Nikipata taarifa kama hizi kuwa mzee ana mahusiano na mmama fulani na mahusiano yale yalianza kuathiri ustawi wa familia yetu. Baada ya kupata ushahidi usiotia shaka nikafanya ka urafiki wa kinafiki na yule mama.

Kuna siku nikapita kazini kwake muda ambao alikuwa anafunga kuelekea kwake. Kwa kuwa hakuwa na gari nikajipendekeza kumpa lifti nikidai nami naelekea maeneo ya kwake. Kwenye gari linikuwa na wana watatu ambao "wameshiba" kwelikweli.

Kuingia tu akawekwa mtu kati. Hapo ndipo nikamweleza A-Z na nikamwambia wana wangeweza kumfanya chochote wanasubiri amri yangu tu.

Bi mmama alilia sana na kuomba msahama kuwa hatarudia na akaahidi kumwacha mzee kwa namna yoyote. Baada ya msamaha wake nikamwambia nikisikia hiyo habari kuwa amemwambia mzee atakutana na jambo baya mno maana wale mwana wameshamfahamu na wanajua kazini kwake.

Hii mbinu ilisaidia sana kuokoa mahusino ya pale home maana bi mmama alimwacha mzee na ananiogopa mpaka kesho.
 
My hypothesis kwa hilo tukio

1. Mume wa huyo mama ana kisukari na uzee tayari so has got nothing to loose as far as mkwanja wa mshua wako una flow he doesn't bother to ask anything

2. Mshua wako na huyo mzee wote wamerogwa na huyo mmama
 
Hilo sio lako... Kaa kimya kwani umeshalipokea...Ukiona unahitaji kufanya kitu lipeleke kwa mzee wa heshima rafiki yake au ndugu yake mkubwa ndio afanyie kazi
 
Maoni mujarabu....Mtoa mada asidhani katika miaka 30 ya ndoa hilo ndio jambo la kwanza kuwatokea wazazi wake....Yamepita mengi kwa hiyo hata hilo asidhani yeye anaweza kulibeba kwa busara zake...
 
Hili lakuhonga pia lipo mkuu.Unaambiwa kun wakat mzee anachota mchele,maharage,na unga anampa huyo mchepuko Yaani maza wangu kakasirishwa na mengi



Duuuh [emoji2357][emoji2297][emoji2296] jamani! [emoji24]

Fikiria inauma kiasi gani ?! Mama yako ana kila sababu ya kujisikia vibaya juu ya hayo mahusiano ya baba yako na huo mchepuko.

Hata Vijana wengine huwa wanachukua vyakula, mafuta ya kupikia , sukari , sabuni, n.k. nyumbani kwa wazazi wao kwenda kuhonga mademu na kuibia hela wazazi wao na wanachuo wenzao kwenda kuhonga mademu zao.

Wengine wanaibia wanachuo wenzao hadi laptops wakauze wahonge mademu.

Inauma sana Yani mama yako namuelewa tu.
 
Mbinu ya kutumia ni kumpa pongezi baba yako na kumpa big up nyingi kwamba ameopoa pisi kali, baba atafurahi sana. Usiwe fala..ukifanya hivyo utakua kipenzi cha baba.
 
My hypothesis kwa hilo tukio

1. Mume wa huyo mama ana kisukari na uzee tayari so has got nothing to loose as far as mkwanja wa mshua wako una flow he doesn't bother to ask anything

2. Mshua wako na huyo mzee wote wamerogwa na huyo mmama
Hii namba2 namimi nimehisi hvy.
Namba1 Sina uhakika na afya ya yule mzee kwamb anasukari au la.Hilo la mchepuko kupewa mkwanja namzee wangu silipingi.
 
Ulitumia umafia mzuri.
 
Mbinu ya kutumia ni kumpa pongezi baba yako na kumpa big up nyingi kwamba ameopoa pisi kali, baba atafurahi sana. Usiwe fala..ukifanya hivyo utakua kipenzi cha baba.
Vipi nikiwa kipenzi Cha baba alafu nikampoteza mama?
Unashauri nimwite baba kabisa ili nimpongeze kwa hilo?
Hata hvy nashukur kwa Ushauri wako.
 
Vipi nikiwa kipenzi Cha baba alafu nikampoteza mama?
Unashauri nimwite baba kabisa ili nimpongeze kwa hilo?
Hata hvy nashukur kwa Ushauri wako.
Baba yako kama ni mstaafu tayari muache ale mema mzee. Mwanaume hajaumbiwa mwanamke mmoja, hizi kanuni wameleta tu watawala wa dunia.
 
Hahahahha hili biti la kitoto utampiga mwanamke mtu mzima ambaye ananufaika kifedha na hazina ya babaako πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚?

Kitachofuata siku ya mechi ijayo huyo mchepuko ataropoka yote na wote watakupuuza tu. Mzee atakuona boya kwa sababu lazma umeambiwa hio ishu na maza ako
 
Tena ukifa ndo anahamia kabisa pale home..!! Sasa sijui atafoka..!?
 
Sometimes tunaendekeza midomo sana,
Hapo naunga mkono hoja..!! Unajuwa huyo mtaka kumshauri babaake ana stori ya kwa mama yake tu..!! Hajui nini kimemfanya baba aamue hayo..!! Na kwa bahati mbaya, kwa jinsi wanaume tulivyo, AKIMUULIZA atazuga tu, wala hatasema chanzo halisi..!! Usikute mwamba kabaniwa unyumba miaka kadhaa, sasa jambo kama hili anaweza akamwambia mwanae?
 
Its simple tu,mwambie mama ako ampe baba ako anachopewa na mchepuko, ndoa haina mazoea akazane na awe romantic aache kujifanya mtu mzima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…