Ushauri, niwahusishe watoto wangu wa nje ya ndoa kwenye urithi?

Njia nyingine ya ku deal na hii ishu ni kuwajengea maisha hao watoto wa nje huko huko waliko wao na mama zao. Mfano unaweza kumfungulia mama yao biashara na ukawajengea mji wao, ili wajitegemee huko wasije kudai urithi uliochuma na mke wa ndoa.
Hii ndo mzuri kuna baba mmoja alifanya hivyo.
Watoto wa nje wakawa na mali zao.
Na wa ndani ya ndoa wakawa na mali zao hawakuingiliana kabisa.
 
Yaani nawashangaa wanawake wanaoolewa siku hizi, kwanini uolewe? Kwanini unakubali kwa akili zako timamu kumpa mtu mwingine Uhuru wa kukuumiza kihisia na kukosa furaha maisha yako yote? Yaani kwanini?? Huwa naelewa nikiona wale ambao maisha kidogo yamekua magumu naona labda anataka wa kumlisha na kumhudumia, Ila mtu una kazi una weza kujihudumia kila kitu kwanini unajiingiza kwenye jehanamu inayoitwa ndoa?? Ndoa ni tamu Sana kwa mwanaume Ila kwa wanawake hahah dah ni huzuni Ila oleweni wenyewe mnasema ndoa ni heshima, sijawahi kuelewa logic ya ndoa kabisa zaidi ya kujitafutia maumivu ya kihisia, stress, pressure in your 30s, na kufa mapema kwa magonjwa ya kuletewa.
 
Agawane mali na mkewe nusu kwa nusu, halafu nusu yake aigawe kwa familia ya ndoa na ya nje ya ndoa.

Kwanini jasho la mwanamke wa ndoa ligawanwe na wa nje ya ndoa? Huyo mama wa nje ya ndoa akifariki atawagawia mali watoto wa ndoani?
 
Duuuu
 
Atafute mwanasheria, andike mgawanyo wa mali zake, Ndugu wa karibu wawe na taarifa uwepo wa usia na mwanasheria pia atambulishwe ni nani hasa wa kukabidhiwa huo usia wa mgawanyo wa mali, ili kwa siku za usoni kusiwe na shida kuhusu mali, watoto wote wapate haki zao stahiki.

Chukua hili mfikishie mgonjwa.
 
Mfano naomba ufafanuzi agawe kivipi mkuu
 
Mfano naomba ufafanuzi agawe kivipi mkuu
Mwenye mali ndiye anajua kwamba mali hii na hii iende kwa mtoto huyu na yule, aweke kwa mandishi kwa msaada wa mwanasheri, iwe ni sehemu ya usia wake.

Kwa sasa cha muhimu ni kuangalia kesho ya watoto wote, wa ndoa na hao walio nje ya ndoa.

Muhimu: Hili alifanye mapema na iwe siri yake na mwanasheria, na hao ndugu wanaofahamu hali halisi.
 
Mi ni mhanga wa hilo.

Nilimchukua kijana wa nje wa mme wangu. Alipokuwa mkubwa alihakikisha ndoa imesambaratika.

Mme alipokufa ilikuwa shida, nilifukuzwa msibani yaani yule kijana alihakikisha naondoka pale, sikulala.

Ndugu wa mme wakawa upande wa mtoto wa nje.

Ninachoshukuru nilikuwa nimemwambia mme wangu asiandike wosia, alisikia, cheti cha ndoa kilinisaidia kupambana mahakamani.

Nyumba ikauzwa, na pia alikuwa na watoto wengine wengi nje.

Kila mmoja akapata kiasi.

Mtoto wa nje ni tatizo.

Nilihangaika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…