Ushauri: Rais Samia kata deal mapema na upinzani kabla ya mazito kuja!

Ushauri: Rais Samia kata deal mapema na upinzani kabla ya mazito kuja!

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Nilishauri haya mwaka jana lakini naona kama Raisi anachukulia ukarimu wa Mbowe vibaya na kumweka kwenye wakati mgumu kwa kukaa mwaka mzima bila kuanza mchakato wa katiba. Jaji Mutungi hakuna mtu hata mmoja anamwamini !! Raisi Samia msifanye watu watoto ! Je Mnataka katiba au mnataka kufanya Watanzania kama watoto!

Namshauri Rais Samia kukaa chini na kufikiria vizuri kuhusu siasa kwa ujumla wake. Upinzani hasa CHADEMA nilipopitia mitandao ya majadiliano na navyoona huku USA Mbowe anavyopokelewa ni vizuri kwa manufaa ya nchi Rais awapuuze hao wanaofikiri wakati wa Magufuli utawezekana tena.

Vikao wanavyofanya Mbowe , Lissu na Lema si vidogo na vimejipanga kuhakikisha wakianza kudai katiba na mikutano wana uhakika wa support ya nchi hasa za Magharibi zinazotusaidia. Je, kwanini tusipuuze haya.

Tukipuuza tutakuwa kama Magufuli ambaye mwisho wa miaka yake mitano ndiyo aligundua makosa na kuanza kurekebisha.

Kosa kubwa ni kukopa kwenye bank binafsi kwa muda mfupi na kwa riba ya juu. Mfano bank ya Dunia ili tupa mkopo wa $1.4B kwa riba ya 3% kwa miaka 20 wakati Magu alichukuwa mkopo kutoka bank wa $1.5B kwa riba ya 8.5% kwa miaka 6.

Malipo ya mkopo wa Magu kwa mwaka yalikuwa makubwa kiasa kwamba kati ya mkopo wetu wa $1.4B walichukuwa nusu $700M na kwenda kupunguza mkopo wa Magu wa $1.5B mbao bila kufanyiwa mabadiliko uingekuwa Tsh 700B kwa mwaka.

Sasa je nani anatupa mikopo ya bei rahisi? Nani anatupa $500M kwenye afya kila mwaka? ni hao wadau. Sasa kama Rais ni kupima kama maandamano ya katiba na ndiyo kukosoa Serikali ni sawa na faida nyingi ambazo tunapata kwa wananchi wa kawaida.

Lakini je nani hasa ananufaika na kubana watu au kuzuia wapinzani kuongea? sio Rais Samia bali ni mafisadi pekee ndiyo wanafaidika.

Tuogope sana utulivu kuliko fujo wapinzani kwa muda wametulia na haina maana ni wajinga.

Kinana kwa wale wa Arusha tunamjua ni mfanyabiashara atakuwaacha kweupe.
 
Magu alichukuwa mkopo kutoka bank wa $1.5B kwa riba ya 8.5% kwa miaka 6. Malipo ya mkopo wa Magu kwa mwaka yalikuwa makubwa kiasa kwamba kati ya mkopo wetu wa $1.4B walichukuwa nusu $700M na kwenda kupunguza mkopo wa Magu wa $1.5B mbao bila kufanyiwa mabadiliko uingekuwa Tsh 700B kwa mwaka. Sasa je nani anatupa mikopo ya bei rahisi?
Hii ni tuhuma nzito sana!, please substanciate ni benki gani, na ni lini tulikopa WB na kuzitumia hizo pesa za WB kulipia mkopo wa bank binafsi?. Kati ya fedha ngumu kuwa diverted ni fedha za WB!. Kila mkopo wana u ring fence kwanza, kisha a length procedure za approval, mpaka zipate no objection ndipo zitoke na zitafanya kile tuu kilichokubaliwa!. Naomba ufafanuzi hapa hilo liliwezekana vipi?.
P
 
..kuna hotuba moja ya Dr.Ssh anazungumzia suala hilo la mkopo mmoja kutumika kulipa mkopo mwingine, au fedha za uviko kutumika kulipa madeni.

..nadhani mtoa mada anazungumzia hiki anachokieleza Rais Dr.Ssh hapa ktk video.

Cc bagamoyo
 
Fujo ataleta nani? Watanzania wangapi wako tayari kujitoa muhanga kuingia barabarani kuandamana na kudai madadiliko? Wachache sana ambao ni rahisi kwa vyombo vya usalama kuwashughulikia na kuzima hizo fujo mapema sana.
 
MaCHADEMA yanaacha shida za wananchi hapa yanazurura ulaya kujifunza ushoga. Pumbavhu saaanaaa
 
Namshauri Raisi Samia kukaa chini na kufikiria vizuri kuhusu siasa kwa ujumla wake. Upinzani hasa Chadema nilipo pitia mitandao ya majadiliano na navyo ona huku USA Mbowe anayopokelewa ni vizuri kwa manufaa ya nchi Raisi awapuuze hao wanaofikiri wakati wa Magufuli utawezekana tena.

Vikao wanavyofanya Mbowe , Lissu na Lema si vidogo na vimejipanga kuhakikisha wakianza kudai katiba na mikutano wana uhakika wa support ya nchi hasa za Magharibi zinazotusaidia. Je kwanini tusipuuze haya. Tukipuuza tutakuwa kama Magufuli ambaye mwisho wa miaka yake mitano ndiyo aligundua makosa na kuanza kurekebisha. Kosa kubwa ni kukopa kwenye bank binafsi kwa muda mfupi na kwa riba ya juu. Mfano bank ya Dunia ili tupa mkopo wa $1.4B kwa riba ya 3% kwa miaka 20 wakati Magu alichukuwa mkopo kutoka bank wa $1.5B kwa riba ya 8.5% kwa miaka 6. Malipo ya mkopo wa Magu kwa mwaka yalikuwa makubwa kiasa kwamba kati ya mkopo wetu wa $1.4B walichukuwa nusu $700M na kwenda kupunguza mkopo wa Magu wa $1.5B mbao bila kufanyiwa mabadiliko uingekuwa Tsh 700B kwa mwaka. Sasa je nani anatupa mikopo ya bei rahisi? Nani anatupa $500M kwenye afya kila mwaka? ni hao wadau. Sasa kama Raisi ni kupima kama maandamano ya katiba na ndiyo kukosoa serikali ni sawa na faida nyingi ambazo tunapata kwa wananchi wa kawaida. Lakini je nani hasa ananufaika na kubana watu au kuzuia wapinzani kuongea? sio Raisi Samia bali ni mafisadi pekee ndiyo wanafaidika.

Tuogope sana utulivu kuliko fujo wapinzani kwa muda wametulia na haina maana ni wajinga. Kinana kwa wale wa Arusha tunamjua ni mfanyabiashara atakuwaacha kweupe.
Hi nchi ni ngumu sanaa

Mtuu anaweza kaa mahala akanywa kiroba chake akanza kutunga uongo .
Na kwa sababu watawala ni kam Mimi Kibori hatujibu hii kashafa kubwa namna hii.

Check kama huyu

Anatoa tuhuma nzito kiasi hikii and na niuongoo

Hili la akina CHADEMA kufanya mikutano ni sara yao ya CHAMA Chao

Mbona CCM husemi na wamekuwa na mikutano yao na chama washirika wao

Mfano jana tuu kuna mtu amewaita chama cha mambuziiiiii tena alimaanisha maana alitamka mara 5 zaidi.

Tena kuna sijui raisi kavaa zile Nguo za Alshababu mbona hukutoa bandiko kuhusu hii.

Bii Shangazi anaenda uarabuni hadi kukutuna na ndugu zake hukoo na mavikao na hata majamaa yavaa vilemba kama na mavizu kiunoni hukuongeaaa

Ovyooo lenyewe umeandika hadi mimacho yanakutokaa.

ACT wanafanya vikao huko njee wal domo hukufungua
 
Hii ni tuhuma nzito sana!, please substanciate ni benki gani, na ni lini tulikopa WB na kuzitumia hizo pesa za WB kulipia mkopo wa bank binafsi?. Kati ya fedha ngumu kuwa diverted ni fedha za WB!. Kila mkopo wana u ring fence kwanza, kisha a length procedure za approval, mpaka zipate no objection ndipo zitoke na zitafanya kile tuu kilichokubaliwa!. Naomba ufafanuzi hapa hilo liliwezekana vipi?.
P
Pascal Mayalla, wakati mwingine jaribu angalau kuficha ujinga na unafiki wako la sivyo utazeeka ukiwa mchawi.
 
Nashangaa sana kwamba kuna watu wanaishabikia CCM pamoja na hovyo yote inayoendelea! Nafikiri wengi ni vichaa ama wachawi.
Poleni sana na personal interests zenu

Kuna raia wapo nje huko wanasubiri uchaguzi ukaribie ndipo waje nchini ili wapate kura za kuonewa huruma

Endeleeni kuzunguka Ulaya na Marekani watawapigia Kura Wala msijali 😁😁

Endeleeni kuota

MaCHADEMA yanaacha shida za wananchi hapa yanazurura ulaya kujifunza ushoga. Pumbavhu saaanaaa
 
..kuna hotuba moja ya Dr.Ssh anazungumzia suala hilo la mkopo mmoja kutumika kulipa mkopo mwingine, au fedha za uviko kutumika kulipa madeni.

..nadhani mtoa mada anazungumzia hiki anachokieleza Rais Dr.Ssh hapa ktk video.

Cc bagamoyo

Yeah, Nakukumbuka pia tena Mwigulu ndiyo alimshauri Dkt Samia, mkopo mmoja ulipe mkopo
 
Tatizo la nchi hii si katiba mpya Bali Ni watu wenyewe.Uganda wanna katiba bora kabisa Ila Sasa Museven anaifanya anavyotaka.Africa katiba haijawahi kuwa Msaada.Wananchi wa kuisimamia katiba hamna
 
Nashangaa sana kwamba kuna watu wanaishabikia CCM pamoja na hovyo yote inayoendelea! Nafikiri wengi ni vichaa ama wachawi.
Sasa utashabikia Wapinzani wasiojielewa hao? Wapinzani njaa Nani awashabikie? Tumeona enzi za Jiwe kilichotokea na wengi waliounga mkono juhudi walinufaika na jasho na rasilimali zangu directly.

I will never repeat tena
 
..kuna hotuba moja ya Dr.Ssh anazungumzia suala hilo la mkopo mmoja kutumika kulipa mkopo mwingine, au fedha za uviko kutumika kulipa madeni.

..nadhani mtoa mada anazungumzia hiki anachokieleza Rais Dr.Ssh hapa ktk video.

Cc bagamoyo

Laughable; yaani alikaa na Mwigulu wakaamua wao wawili;
Nchi hata Think Tank moja haina; lo, what a country!
Kenya wana Think Tanks 57; sisi ZERO! Yaani ndiyo maana CCM hawataki kuachia Nchi, madudu mengi mno!
 
Wameanza kukiri wenyewe bila shuruti kuwa nchi inaongozwa na mbumbumbu
 
..kuna hotuba moja ya Dr.Ssh anazungumzia suala hilo la mkopo mmoja kutumika kulipa mkopo mwingine, au fedha za uviko kutumika kulipa madeni.

..nadhani mtoa mada anazungumzia hiki anachokieleza Rais Dr.Ssh hapa ktk video.

Cc bagamoyo

Mikuu JokaKuu asante kwa hii, hii Ndio nimeisikia Leo, na pia kusikia mkopo usio na riba!. Ule mtindo wa JPM kuingia na mafaili chumbani na kuwapigia simu mawaziri usiku mkubwa, sasa hawa chawa wa JPM, wanataka kuuleta uchawa huu kwa Samia!, saa za kulala kwa nini umpigie simu rais usiku na kumkatisha usingizi wake kwa jambo ambalo sio emergency?!.
P
 
Back
Top Bottom